GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,544
- 108,871
Nimegundua ya kwamba 85% ya Wasomi wa Tanzania na hasa ambao wanafanya Kazi Serikalini au ni Watumishi wa Serikali wana tatizo kubwa sana ' Public Speaking ' na wana Kiwango cha chini mno cha ' Confidence ' mbele ya Wakubwa wao hali ambayo inashangaza na kusikitisha mno.
Haiingii akilini kabisa unakuta Mtu ni Bosi fulani katika ngazi ya Kiserikali lakini akipewa wasaa wa Kuzungumza na ' hadhira ' husika au hata tu Kujieleza utaona anajiumauma, anababaika na kutetemeka mno hali ambayo imenifanya nijiulize maswali mengi kwamba ina maana huko Vyuo walikopita walikuwa hawana ' debating classes ' ili ziweze kuwajenga na kuwapika vyema hasa katika ' Public Speaking ' na kuwa na ' Confidence ' ya kutosha.
Kwa jinsi wanavyotetemeka na kubabaika huku wakijiumauma naogopa katika Kuongea / Kujieleza kuna Siku Mtu ( Kiongozi ) tutashuhudia ama Kiongozi fulani anajikojolea mbele au anajinyea / anaukweka mbele ya hadhira kwa hofu kubwa mbele ya Watu.
Nitoe RAI kwa Vyuo Vikuu nchini Tanzania tafadhalini hebu lifanyieni Kazi hili tatizo kwani sasa linazoeleka halafu linakera pia kwa Watu ambao ni makini. Haiwezekani Mtoto wa Shule ya Msingi tu wa nchini Kenya na Uganda anaweza Kuongea mbele ya ' hadhira / umma ' bila Uwoga / Hofu lakini unalikuta Jitu Zima / Zee Zima lina Cheo katika Halmashauri au Manispaa au Wizara au Kurugenzi au Wilaya au Mkoa halafu akipewa ' mic ' na Mkuu au Mteule wake anabaki ' Kujambajamba ' tu pale mbele japo bahati nzuri ' ushuzi ' wake huwa haunuki.
Wasomi badilikeni katika hili kwani linatudhalilisha na kuwafanya majirani zetu watucheke na waidharau hadi Elimu yetu hii.
Nawasilisha.