Hili suala lina uhusiano gani na vifo vya watu

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
6,860
12,291
Kwanza kbs natanguliza salam kwa kila mwanachama mwenzang hapa JF, na pia nawatakia heri ya xmass na mwaka mpya ujao.

Niende sasa kwenye mada kuhusu mambo ambayo nimeyaona na kuyasikia kwa watu mbalimbali, lkn kwa kuokoa muda leo nitazungumzia matukio mawili ambayo nimeyashuhudia kwa macho yangu. Kuna rafiki yang ambae amefariki juzi ambapo kabla ya kufariki alianza kwanza kuumwa kwa kipindi cha wiki 1.

Ugonjwa wake ulianza siku ya jumanne ya wiki iliyopita ambapo alianza kusikia maumivu ya tumbo chini ya kitovu. Mwanzo mwanzo alitumia dawa ya kupunguza maumivu akidhani labda maumivu yale yangeisha lkn kadri muda na siku zilivyokwenda maumivu yalizidi kuongezeka, japo alipokuwa anameza dawa yalikuwa yanapoa kwa masaa kadhaa baadae yanaendelea tena zaidi ya ilivyokuwa mwanzo.

Alipoona maumivu yanazidi, Jumatatu ya wiki hii ikabidi ndugu zake wampeleke hospitali ambapo wakamfanyia vipimo na kumpa dawa nyingine za kupunguza maumivu, ila inasemekana daktari alilaumu kwa kuchelewa kwao kumpeleka mgonjwa wao hospitali.

Jamaa wakamrudisha nyumbani kuendelea na dozi zake. Siku ya J4 wiki hii nilikwenda kumuona kwa kweli jamaa alikuwa na hali mbaya sana na hata kuongea nae kulikuwa kwa shida. Ktk kumdadisi jamaa nikamuuliza labda kuna kitu ambacho anaweza kuwa alikula kikamu affect mpaka kumsababishia maumivu yale ndipo jamaa akanambia kwamba alilala na mwanamke fulani ambae alikuwa ametoka kutoa mimba siku chache kabla ya kukutana na rafiki yangu na kwamba hicho kitendo cha kulala na yale mwanamke aliyetoa mimba siku chache ndio kilichomletea ugonjwa ule na akadai kwamba kwa hali aliyofikia hawezi tena kupona.

Nikampa moyo lkn pia nikakumbuka miezi 6 iliyopita tulimzika ndugu yangu ambae na yeye aliumwa na kufa kwa style ile ile ya rafiki yangu. I mean na yeye alilala na mwanamke aliyetoa mimba kesho yake akaanza kuhisi maumivu ya tumbo chini ya kitovu baada ya siku 5 akafariki.

Sasa baada ya kushuhudia vifo hivi pamoja na habari nyingine nilizowahi kuzisikia kuhusu aina hii ya vifo ningependa kujua ni kitu gani ambacho humsababishia mwanaume tu peke yake maumivu na hatimaye kifo chake huku muhusika aliyetoa mimba(mwanamke) akibaki mzima wa afya?

Pia inasemekana kwamba ukiupata ugonjwa huu inatakiwa uanze kupata tiba kabla ya siku 3 kupita, tena inasemekana tiba yake inapatikana kwa dawa zetu za kienyeji.

Inasemekana ukizidisha tu siku tatu basi kama ni Muislam uanze kuandaa sanda na usia kbs na kama ni mkristo uandae sanduku na usia maana uwezekano wa kuendelea kuishi ni mdogo mno yani ni sawa sawa na kupitisha treni kwenye daraja la mbao.

Mwenye kuelewa zaidi mambo haya au kama uliwahi kushuhudia vifo vya aina hii unakaribishwa.
 
Summary ya uongo....
Ni kweli kwa sababu nimeshuhudia kwa watu wawili. Si kwamba mwanamk akishatoa mimba hauruhusiwi kunaniiu, unaruhusiwa ila inatakiwa ukutane nae angalau baada ya mwezi au siku 40 kupita. Sasa hawa inaonekana waliwaingilia baada ya siku 1 au 2 toka siku waliyotolea mimba
 
Baada ya siku moja au mbili si utakutana na Damu Mkuu?
Nahisi hiyo damu ndio huwa na bacteria ambao hukimbilia kushambulia kibofu cha mkojo na baadae utumbo then umauti unakukuta. Haya ni mawazo yang tu
 
Hakuna mahusiano yoyote kati ya hayo mambo,na mpaka sasa hakuna research yoyote inayoonyesha mahusiano kati ya hayo mambo.

Haya ni matatizo tu ya afya ya mhusika mwenyewe.
 
Kuna sababu nyingine ya hivyo vifo
Nimelala na mwanamke aliyetoka kutoa mimba siku mbili tu zilizopita yani katoa mimba Kama juzi me nikalala nae Leo na sio Mara moja nimekaa nae wiki nzima
 
Nikiwa mdogo kuna house boy wetu alimgegeda house girl akiwa kwenye bleed aliumwa kama ulivoelezea ila cha zaid yeye mashine na pumbu zilivimba mpaka akashindwa kutembea na ikawa zikiguswa tu anapiga yowe balaa

Jamaa alipelekwa hospital akatibiwa na kupona kabisa, sasa najiuliza sijui alikua anaumwa ugonjwa gani maana na mimi nikiwa mtu mzima hivi mwaka juzi nilimgegeda demu wangu akiwa kwenye bleed tena kavu kavu na wala sikupatwa na kitu chochote

Sio kwamba sikua nakumbuka kile kilichomtokea house boy wetu miaka hiyo ila tu nilikua na fantasy hiyo na huyo demu akiwa kwenye bleed hua anagenye sana kwahiyo tulipokutana ilikua kama positive na negative sides of magnetic bars na pia nilipita Google kwanza kujiridhisha iwapo kuna madhara yoyote kufanya hivyo.
 
Kingine kama ushauri mwanamke yoyote kabla hujakutana naye mpimiane, au tumia condom au muwe mnameza ant biotic kwanza .ila uhusiano kati ya aliyetoa mimba jana na ksexy naye kesho yake huo ni ujinga wa kutojitambua,mtu bado Ana uchafu chini alafu unafanya kitu kama hicho ni upumbavu na kutojitambua kama mwanaume yaani upo upo tu.
 
Back
Top Bottom