Hili suala la Wamachinga kuondolewa pembezoni mwa barabara linatupa wakati mgumu zaidi. Tumesimama katikati

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,353
11,496
Tunashindwa kusema Serikali imekosea na tunashindwa kusema Wamachinga walikosea.

Kwa kweli hapa hata wapinzani tunapoulizwa tunajikuta tunajibu swali ambalo halikuulizwa. Muulize tu mpinzani akupe jibu.

Je, Serikali kuwaondoa Wamachinga pembezoni mwa barabara ipo sahihi au imekosea. Utasikia jibu lake

Hili limekuwa gumu hata kuanzishia space na mijadala kule clubhouse. Maana linauma kote kote.
 
Hivi Machinga ndio watu wenye Haki Nchi hi kuliko makundi mengine?

Tafuteni till namber mfanye biashara halali

Kuna makundi kibao Sana hayapati haki zake ambazo zipo kisheria Kama wanafunzi vyuo vikuu kukosa mikopo.

Watu hawakuongezewa mishahara miaka 5

Leo mnafanya kazi bila kufuata sheria but bado mnataka kuwa special.
 
Kwani wapinzani ndo waliwapa ruhusa machinga kufanya biashara popote? Mpaka ifikie hatua mtake ushauri kutoka kwao mataga mlivyo na shida Kuna siku mtakuja kusema suala la kuondolewa machinga mjini ni mipango ya wapinzani
 
Kwa upande wangu nahisi wanataka kuwabana wafanya biashara wakubwa wenye maduka kulipa Kodi Sasa ili kusiwepo malalamiko sijui machinga wapo mbele yetu tunashindwa kuuza kazi Moja sasa lipa Kodi
 
Tunashindwa kusema Serikali imekosea na tunashindwa kusema Wamachinga walikosea.

Kwa kweli hapa hata wapinzani tunapoulizwa tunajikuta tunajibu swali ambalo halikuulizwa. Muulize tu mpinzani akupe jibu.

Je, Serikali kuwaondoa Wamachinga pembezoni mwa barabara ipo sahihi au imekosea. Utasikia jibu lake

Hili limekuwa gumu hata kuanzishia space na mijadala kule clubhouse. Maana linauma kote kote.
Ni mtu mjinga mjinga tu atafikiri machinga wana haki ya kufanya chochote wanachotaka jijni.

Miji haikujengwa kwa ajili ya machinga, na eneo la watembea kwa miguu na mitaro si maeneo ya biashara.
Mbaya zaidi machinga halipi kodi wala kuchangia maendelo ya Taifa zaidi ya kuwa kero.
Sijui kizazi hiki kilicholaaniwa mtaelewa lini mantiki hiyo?
 
Mqenyekiti wenu alikuwa anasema machinga waachwe wafanye biashara zao maana walimchagua.

Kati ya waliokuwa wanamshangilia mwenyekiti wenu ni wewe .
Leo hii umemgeuka tayari kisa hayupo duniani?

Amakweli tenda wema nenda zako.
 
Tunashindwa kusema Serikali imekosea na tunashindwa kusema Wamachinga walikosea.

Kwa kweli hapa hata wapinzani tunapoulizwa tunajikuta tunajibu swali ambalo halikuulizwa. Muulize tu mpinzani akupe jibu.

Je, Serikali kuwaondoa Wamachinga pembezoni mwa barabara ipo sahihi au imekosea. Utasikia jibu lake

Hili limekuwa gumu hata kuanzishia space na mijadala kule clubhouse. Maana linauma kote kote.
Wamachinga waondoke kabisa hawatakiwa hapo. Watu watakafanya vipi biashara za barabarani?
 
Kwa upande wangu nahisi wanataka kuwabana wafanya biashara wakubwa wenye maduka kulipa Kodi Sasa ili kusiwepo malalamiko sijui machinga wapo mbele yetu tunashindwa kuuza kazi Moja sasa lipa Kodi
Wala sio sababu hiyo kwani , kwani siku zote walikuwa wanalipa kodi, hiyo sababu eti machinga yupo mbele yangu ki kodi haina mashiko, kwani kodi hutozwa kulingana na mauzo yako.Kwani miaka hiyo 5, ya mwendazake si walikuwa wakilipa kodi tu licha ya vulugu za machinga?japo kwa tabu sana!!
 
Mqenyekiti wenu alikuwa anasema machinga waachwe wafanye biashara zao maana walimchagua.

Kati ya waliokuwa wanamshangilia mwenyekiti wenu ni wewe .
Leo hii umemgeuka tayari kisa hayupo duniani?

Amakweli tenda wema nenda zako.
Ule wa mwendazake ni utapeli wa kisiasa na si endelevu.
Onyesha nilipomshangilia, kwani mi Skm gang?
Pamoja na kuwa mskm?
 
Jeshi la polisi lina kauli mbiu ya "tii sheria bila shuruti"
Wamachinga waliachiwa wakati wanavunja sheria, sasa inaonekana wanaonewa, hali hi ipo kwa bodaboda wanavyovunja sheria bila kuchukuliwa hatua, nina hakika mbeleni kutakuwa na mtafaruku mkubwa atakapopatikana mtu wa kusimamia sheria za barabarani.
 
Tunashindwa kusema Serikali imekosea na tunashindwa kusema Wamachinga walikosea.

Kwa kweli hapa hata wapinzani tunapoulizwa tunajikuta tunajibu swali ambalo halikuulizwa. Muulize tu mpinzani akupe jibu.

Je, Serikali kuwaondoa Wamachinga pembezoni mwa barabara ipo sahihi au imekosea. Utasikia jibu lake

Hili limekuwa gumu hata kuanzishia space na mijadala kule clubhouse. Maana linauma kote kote.
UGUMU upo wap broo?
we huoni DAR inavyopendeza kwa sasa?
si wametegewa eneo? waende huko...
 
Back
Top Bottom