Hili suala la utumbuaji majipu bila kutengeneza mfumo halimpeleki mbali Rais Magufuli

Mkulima wa Kuku

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
1,270
534
Nazungumzia suala la kuongoza nchi kwa vitisho na hofu nyingi bila kutengeneza mfumo wa kukomesha uchafu huo. Yeye mwenyewe ni shahidi kwa aliyoyakuta BoT jana.

Kinachotakiwa ni badiliko la mfumo litakalofanya watu wachukie kutenda uovu na si kuwatisha watu. Mungu alipoweka Amri 10 kwa wanadamu kupitia Musa aliona wazi kuwa haiwezekani kutekeleza akaamua kubadili mfumo kwa kumleta Yesu na kuweka mfumo wa wokovu kwa njia ya Neema inayopatikana kwa njia ya imani.

Sasa sisi tukiishi kwa vitisho vikali na hofu kubwa ndani ya mioyo yetu kwa uongozi...suppose ameondoka leo yule tunayemwogopa, itakuwaje kwa ufisadi?

Nashauri kama walivyosema wengine mfumo uangaliwe, uundwe upya ubadilishwe ili kulisaidia taifa letu permanently.
 
Nazungumzia suala la kuongoza nchi kwa vitisho na hofu nyingi bila kutengeneza mfumo wa kukomesha uchafu huo. Yeye mwenyewe ni shahidi kwa aliyoyakuta BoT jana. Kinachotakiwa ni badiliko la mfumo litakalofanya watu wachukie kutenda uovu na si kuwatisha watu. Mungu alipoweka Amri 10 kwa wanadamu kupitia Musa aliona wazi kuwa haiwezekani kutekeleza akaamua kubadili mfumo kwa kumleta Yesu na kuweka mfumo wa wokovu kwa njia ya Neema inayopatikana kwa njia ya imani. Sasa sisi tukiishi kwa vitisho vikali na hofu kubwa ndani ya mioyo yetu kwa uongozi...suppose ameondoka leo yule tunayemwogopa, itakuwaje kwa ufisadi?
Nashauri kama walivyosema wengine mfumo uangaliwe, uundwe upya ubadilishwe ili kulisaidia taifa letu permanently.
Kwa hiyo watu hawatendi dhambi tena?..wacha siasa za fisi,ramli na uchawi kuomba mabaya yatokee ili useme...kama rais lazima aonyeshe dhamira
 
Labda anaendelea kutumbua majipu huku pia akiendelea kutengeneza misingi ya utendaji kazi kwa ufanisi
 
Tueleweshe kwanza mfumo ni nini na unaubadili vipi, na afanyeje ili kuutoa na kupachika mpya. ?
Kuna kipindi Mizengo Pinda aliwahi kuzungumzia mfumo wa utendaji kazi wa serikali ni mbovu na inabidi uangaliwe upya,ulijua kuwa alikuwa anazungumzia mfumo upi.Lakini pia sheria na katiba yetu bado ni legelege
 
Unataka mfumo gani. Mbona kipindi kilichopita hukutaka mfumo? Nyie ndo wale wale!
 
Kinachoshangaza huu wimbo wa mfumo umeshika kasi lakini ukiwauliza maana yake ni nini hawana jibu.

Siasa za Tanzania niza ajabu sana!

Tunadhani tunauelewa wa kila hoja wakati hatufahamu au tunafahamu kiduchu!
 
Nia ya JPM ni kurudisha mfumo kwa kuendesha shughuli za serikali kwa sheria na haki mpaka jipu linakua jipu maana yake lilitoka nje ya mfumo kwamba mambo yake hayakuwa ya haki wala kisheria sasa JPM anavyoyatumbua ni kwamba anarejesha mfumo uende kama ilivyotakiwa kuhusu swala la uoga napinga vikali sidhani kama ukiwa unafanya kazi kwa haki na sheria utamuogopa mtumbua jipu binafsi naibariki kazi ya Rais mpaka wote watanyooka
 
Nazungumzia suala la kuongoza nchi kwa vitisho na hofu nyingi bila kutengeneza mfumo wa kukomesha uchafu huo. Yeye mwenyewe ni shahidi kwa aliyoyakuta BoT jana. Kinachotakiwa ni badiliko la mfumo litakalofanya watu wachukie kutenda uovu na si kuwatisha watu. Mungu alipoweka Amri 10 kwa wanadamu kupitia Musa aliona wazi kuwa haiwezekani kutekeleza akaamua kubadili mfumo kwa kumleta Yesu na kuweka mfumo wa wokovu kwa njia ya Neema inayopatikana kwa njia ya imani. Sasa sisi tukiishi kwa vitisho vikali na hofu kubwa ndani ya mioyo yetu kwa uongozi...suppose ameondoka leo yule tunayemwogopa, itakuwaje kwa ufisadi?
Nashauri kama walivyosema wengine mfumo uangaliwe, uundwe upya ubadilishwe ili kulisaidia taifa letu permanently.

Hii inaitwa mfadhaiko lazima umeguswa.....
 
Nimesoma kwa makini uzi wako huu, lakini maoni yangu (kama pia MKRISTO RC) ni kama ifuatavyo: Ni kweli mfumo unahitajika na ni wazi kuwa JPM na serikali yake ni lazima wanalishughulikia hili.

Inawezekana uko sahihi Mungu alibadili mfumo kwa kumleta YESU lakini pamoja na ujio wa YESU, maovu katika jamii hayakuisha na mpaka leo hii hayajaisha ndiyo maana bado wizi unaendelea kama wa BOT, TRA, BANDARI na kadhalika. Uasi, usaliti, umalaya, wizi, ujambazi, unyang'anyi, vita, mauaji na kadhalika ndiyo kwanza vinazidi kupamba moto katika pembe zote za dunia.

Anayeishi kwa vitisho ni mwovu na huyo ndiye anayeogopa mkono wa sheria. Watu wa kawaida, wavuja jasho na walalahoi hawaogopi mkono wa sheria. Walalahoi wanapenda hatua zichukuliwe dhidi ya waovu, na ndiyo maana watanzania wengi wanapenda hatua anazochukua Magufuli na serikali yake dhidi ya waovu kama wa TRA, BANDARI, TRA na kadhalika.

Watu wachache tu ndani ya JF na kwingineko ndio wanaoona kuwa hatua za MAGUFULI na serikali yake ni vitisho. Wananchi wengi kwa mamilioni nchi nzima wanafurahia hatua za MAGUFULI na serikali yake.

Wananchi walio wengi wanafurahia wezi waendelee kuishi kwa hofu, waisome namba kama 'watoto wa mjini' wanavyosema, na wanyang'anywe mali.

Kama unashauri uundwe mfumo hilo ni jambo jema kabisa. Ni vizuri pia ushauri kwa kueleza mfumo huo uweje.
 
Hapa cha kufanya haraka ni Kuleta Katiba mpya ya nchi, ili isotoe mianya ya rushwa Na mtu kufanya anavotaka. Kama alivosema mleta mada hii Kwa Kama yeye kiongozi akizoea kufanya haya atajitengenezea Chuki kubwa Kwa viongozi wenzako Na badala yake hawezi kufika mbali.

Waswahili wana misemo Yao wanasema binadamu havumi inayovuma ni ngoma, hii misemo ukiifatilia inafanya kazi sana.
Akileta Katiba mpya yenye Tija Kwa Taifa atakuwa Hana haja ya kutumia nguvu kubwa kupita maofisini hata akitulia ikulu nchi itajiendesha yenyewe Kwa remoted Na kila mtu atajua wajibu wake Na hakuna atae kumuona mbaya. Huo Ndio mfumo.
 
Tueleweshe kwanza mfumo ni nini na unaubadili vipi, na afanyeje ili kuutoa na kupachika mpya. ?
Watu wanakariri tu kuondoa mfumo kuondoa mifumo. Nani asiyejua kuwa Tanzania ina mifymo mizuri sana. Nanai asiyejua kuwa Tanzania ina mikakati mizuri sana.

Tatazo tu ni utekelezaji. Ila huenda kuna mifumo unaifahamu ni mibovu name them!!!!!Sema mfano mfumo huu si mzuri nami napendekeza uwe hivi sio tu kukaririshwa na kuimba mifumo bila kutolea mifano!
 
Nimesoma kwa makini uzi wako huu, lakini maoni yangu (kama pia MKRISTO RC) ni kama ifuatavyo: Ni kweli mfumo unahitajika na ni wazi kuwa JPM na serikali yake ni lazima wanalishughulikia hili. Inawezekana uko sahihi Mungu alibadili mfumo kwa kumleta YESU lakini pamoja na ujio wa YESU, maovu katika jamii hayakuisha na mpaka leo hii hayajaisha ndiyo maana bado wizi unaendelea kama wa BOT, TRA, BANDARI na kadhalika. Uasi, usaliti, umalaya, wizi, ujambazi, unyang'anyi, vita, mauaji na kadhalika ndiyo kwanza vinazidi kupamba moto katika pembe zote za dunia. Anayeishi kwa vitisho ni mwovu na huyo ndiye anayeogopa mkono wa sheria. Watu wa kawaida, wavuja jasho na walalahoi hawaogopi mkono wa sheria. Walalahoi wanapenda hatua zichukuliwe dhidi ya waovu, na ndiyo maana watanzania wengi wanapenda hatua anazochukua Magufuli na serikali yake dhidi ya waovu kama wa TRA, BANDARI, TRA na kadhalika. Watu wachache tu ndani ya JF na kwingineko ndio wanaoona kuwa hatua za MAGUFULI na serikali yake ni vitisho. Wananchi wengi kwa mamilioni nchi nzima wanafurahia hatua za MAGUFULI na serikali yake. Wananchi walio wengi wanafurahia wezi waendelee kuishi kwa hofu, waisome namba kama 'watoto wa mjini' wanavyosema, na wanyang'anywe mali. Kama unashauri uundwe mfumo hilo ni jambo jema kabisa. Ni vizuri pia ushauri kwa kueleza mfumo huo uweje.

Jamani umemaliza Mkuu! kama unafuata sheria hofu ya nini?
 
Nazungumzia suala la kuongoza nchi kwa vitisho na hofu nyingi bila kutengeneza mfumo wa kukomesha uchafu huo. Yeye mwenyewe ni shahidi kwa aliyoyakuta BoT jana. Kinachotakiwa ni badiliko la mfumo litakalofanya watu wachukie kutenda uovu na si kuwatisha watu. Mungu alipoweka Amri 10 kwa wanadamu kupitia Musa aliona wazi kuwa haiwezekani kutekeleza akaamua kubadili mfumo kwa kumleta Yesu na kuweka mfumo wa wokovu kwa njia ya Neema inayopatikana kwa njia ya imani. Sasa sisi tukiishi kwa vitisho vikali na hofu kubwa ndani ya mioyo yetu kwa uongozi...suppose ameondoka leo yule tunayemwogopa, itakuwaje kwa ufisadi?
Nashauri kama walivyosema wengine mfumo uangaliwe, uundwe upya ubadilishwe ili kulisaidia taifa letu permanently.
Mkulima wa kuku,nadhani unachanganya vitu,amri 10 zipo pale pale hazikuondolewa na Yesu,isipokuwa amri zipo kama kioo,kioo kinakuonesha uchafu,lakini haiwezi kukufuta hivyo wewe unachukua hatua,amri 10 zipo kutuonesha dhambi zetu then sisi tunatafuta toba kupitia Yesu kiristo
 
Back
Top Bottom