Hili ni tatizo kwa vijana wengi wa Kitanzania, nimesikitishwa sana. Serikali iangalie jambo hili

Bill Lugano

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
1,186
6,402
Habarini. Nimefika jumamosi kutoka Sweden, Canada, Spain, UK, USA, Egypt na Botswana. Safari hii sikuzunguka sana.

Leo Jumatatu huwa mara nyingi natumia JEEP so nimetoka zangu home kwenda Ofisini asubuhi hii ikatokea ajali ndogo tu. Toyota Vits imegonga Gari VW kiasi tu imechubuka.

Nakumbuka huko nyuma nlishawahi pendekeza Serikali iangalie hili suala la hivi vidude kuingia Mjini. Waendeshaji wake huwa muda wote wanaamini wana haraka na wasumbufu sana.

Kilichonivutia kutaka sikiliza maongezi yao ni jinsi yule kijana ambavyo alikuwa anaomba hadi kupiga magoti. Ni sawa alikosea kumgonga mwenzie but haikuwa sahihi kupiga magoti kumbembeleza.

Nliposikiliza kumbe kijana gari lake halina Bima. Nilishangaa sana. Ana Simu ambayo nadhani ni zile ambazo si mbaya za bei ya chini kama 700,000 - 1,000,000 anashindwaje kukata Bima?

Nikawaza sana. Nikakumbuka vile ambavyo mimi ikikaribia week moja tu kuisha navyopigiwa simu kukumbushwa na Kampuni ya Bima kuwa wanaomba wanikatie Bima waniletee popote nilipo.

Mimi nakata Bima ambayo ndani yake pia kuna Bima ya Maisha kwa mwathirika. Yaani ikitokea nikakugonga ndugu zako au familia yako watashukuru sana wakija gundua kuwa wanakuja lipwa Mil 500.

Fikiria mwenyewe. Wakati upo hai ulikuwa unawapa tu mzigo kuomba omba pesa,kudoea chakula n.k sasa umekufa wanalipwa Mil 500 na Bima.hii ni ndani ya masaa 24 tu wala haina mjadala. Kikitolewa tu cheti cha kifo na report ya Traffic. Waliobaki wataulizwa tu Account number basi.

So utagundua kwa kifo chako wao wanapona. Hili huwa sipendi waambia wengi sababu najua wanaweza wakawa wanajigongesha makusudi. Imagine ndo mkeo anajua kuwa sababu ya wewe kufa yeye analipwa na watoto mil 500? Si atakuombea sana uwekwe mahali pema peponi?

Lakini pia najua hata ile chuki ya kuwa nimegonga na kuua mume/mzazi n.k itakuwa haipo. Zaidi anaweza nishukuru. Familia nyingine wanaweza wakawa wanataka niwe nawagonga tu kadiri niwezavyo.

Haya maisha kuna watu wanaishi kwa shida. Mtu anafanya kazi mpaka jumamosi mwisho wa mwezi analipwa tsh 2,000,000. Unajiuliza Mil mbili ataishije huyu na ana mtoto na mke? ana ndugu, jamaa na marafiki? Na Serikali itakusanyaje mapato hapo?huwa nawaza sana.

Sasa ikatokea bahati mbaya mtu kama huyu ndo kapata ajali. Ndugu zake wanaweza shukuru baada ya kuambiwa wakasaini check ya mil 500.

Jamani Bima si kwa ajili ya Traffic. Ni muhimu sana kukata Bima. Bima zenyewe si gharama sana kwa huo usafiri wenu. Mimi huwa Bima inakatwa moja kwa moja naletewa tu na kubandikiwa kwenye Kioo. hapo baada ya Mkurugenzi kunipigia simu kunijulisha kuwa anaomba ajue nilipo aje yeye mwenyewe kunibandikia ile sticker maana hawaamini sana vijana wake kama watabandika vizuri ikawa smart. Anakuja anabandika ananishukuru anaondoka.

Tusiache kukata Bima ndugu zanguni.nlimsaidia yule Bwana mdogo kwa kumchangia Tsh 400,000 ampe jamaa aliyekwaruzwa ambaye alitaka tsh 200,000 kurudia rangi kasehemu husika. Njiani nimewaza sana. Nikasema niwaambie ndugu zanguni ukiweza kukata na Bima ya maisha ni vyema. Unalipia Mil 100 kwa mwaka kwa ile ndogo tu. Hapo ukipata ajali au ukiumwa ukafa familia yako inakuja lipwa Bil 1. Si mbaya. Mimi nimekata kubwa zaidi ya hiyo. Si lazima ukate yangu ya kulipia tsh Mil 500 kwa mwaka
 
Huyu mwandishi kama sijakosea aliwahi kuja na uzi wake kuwa alikwenda na Ranger yake kununua samaki wa shilingi 700,000 ferry kwaajili ya matumizi ya nyumbani, yote hiyo ilikuwa ni hasira baada ya kuona muuzaji amemwacha yeye na kumhudumia mwanamke wa kimanga🤣😂
 
Naombeni kuuliza kama hao jamaa walogongana hapo bima inapaswa kufanya nn? bima ya aina gani hapo inakua na faida kama umekwaruzwa /kugongwa na hili suala la kulipana juuu kwa juu eneo la tukio likoje ilihali mtu alishakata bima?? na kukatia bima gari si suala la lazima hapa tz?
 
Mkuu nunua basi na Hizi gari Bugatti Chiron na Veyron, Ferrari laferrari, Ferrari F8 Tributo, Ferrari Enzo na Ferrari 488 Pista Spider,Gordon Murray TS50, Aston Martin, Lamborghini SVJ Aventador, Lamborghini perfomante na Lamborghini Evo spyder, Maserati, Koenigsegg Rigera na Koenigsegg Jesko, Pagani huayra, Audi R8, McLaren 600lt, McLaren 720s, McLaren Senna na McLaren P1, Mercedes benz SlR convirtable. Rolls-Royce phantom, roll Royce Ghost na Rolls-Royce Wraith.

Pia mkuu wasaidie serikali kuwanunulia ndege hizi ndogo za casenna ziwasaidie kunyunyuzia dawa za kuua nzige huko Arusha na Kilimanjaro. Hawana kabisa
 
Naombeni kuuliza kama hao jamaa walogongana hapo bima inapaswa kufanya nn? bima ya aina gani hapo inakua na faida kama umekwaruzwa /kugongwa na hili suala la kulipana juuu kwa juu eneo la tukio likoje ilihali mtu alishakata bima?? na kukatia bima gari si suala la lazima hapa tz?
Wewe unamuuliza kiduku lilo maswali magumu hivyo wakati ana mambo mengi ya kimsingi ya kufanya ili kukuza uchumi?
 
Back
Top Bottom