Hili ni tatizo kwa vijana wengi wa Kitanzania, nimesikitishwa sana. Serikali iangalie jambo hili

uberimae fidei

JF-Expert Member
Dec 16, 2016
2,077
2,000
Naombeni kuuliza kama hao jamaa walogongana hapo bima inapaswa kufanya nn? bima ya aina gani hapo inakua na faida kama umekwaruzwa /kugongwa na hili suala la kulipana juuu kwa juu eneo la tukio likoje ilihali mtu alishakata bima?? na kukatia bima gari si suala la lazima hapa tz?
Apo kama walikwanguana kidogo hivyo bima hawata coter, halipwi chuchote, ili ulipwe kuna asilimia za kiwango cha ajali na thamani ya gari.ndo maana wameamua kulipana juu kwa juu
 

HUNIJUI SIKUJUI

JF-Expert Member
Apr 4, 2015
1,301
2,000
Apo kama walikwanguana kidogo hivyo bima hawata coter, halipwi chuchote, ili ulipwe kuna asilimia za kiwango cha ajali na thamani ya gari.ndo maana wameamua kulipana juu kwa juu
na kama uyo jamaa aliegongwa ana bima kubwa ni sahihi kumkomalia jamaa aliemgonga ampe kitu?
 

Dumas the terrible

JF-Expert Member
Jan 20, 2021
1,756
2,000
Haahaahaaa kiduku Lilo on the beat,
Nimecheka hapo et unaishije na mke na watoto kwa mshahara wa million mbili ? Aisee we jamaa umefanya nijitafakari sana sie wengine tunahangaikia mshahara wa 1k kwenye kampuni za wahindi na tunafamilia halafu unauliza unaishije anaelipwa milion?

Leteni chai wadau kuna kaubalidi flani nakahisi japo nitie tumbo joto

Nadanganya wadau
 

plan z

JF-Expert Member
Jun 10, 2019
1,087
2,000
Nimesoma huu uzi nikafikia mahali mtoa mada anasema Mil 2 kwa mwezi mtu anaishije, kisha nikarudi juu kuangalia jina la mtoa mada nikakuta ni KIDUKU LILO, baada ya hapo nikarudi kumalizia kuusoma uzi wote.
 

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
43,084
2,000
Habarini. Nmefika jumamosi kutoka Sweden, Canada, Spain, UK, USA, Egypt na Botswana. Safari hii sikuzunguka sana.

Leo Jumatatu huwa mara nyingi natumia JEEP so nimetoka zangu home kwenda Ofisini asubuhi hii ikatokea ajali ndogo tu. Toyota Vits imegonga Gari VW kiasi tu imechubuka.

Nakumbuka huko nyuma nlishawahi pendekeza Serikali iangalie hili suala la hivi vidude kuingia Mjini. Waendeshaji wake huwa muda wote wanaamini wana haraka na wasumbufu sana.

Kilichonivutia kutaka sikiliza maongezi yao ni jinsi yule kijana ambavyo alikuwa anaomba hadi kupiga magoti. Ni sawa alikosea kumgonga mwenzie but haikuwa sahihi kupiga magoti kumbembeleza.

Nliposikiliza kumbe kijana gari lake halina Bima. Nilishangaa sana. Ana Simu ambayo nadhani ni zile ambazo si mbaya za bei ya chini kama 700,000 - 1,000,000 anashindwaje kukata Bima?

Nikawaza sana. Nikakumbuka vile ambavyo mimi ikikaribia week moja tu kuisha navyopigiwa simu kukumbushwa na Kampuni ya Bima kuwa wanaomba wanikatie Bima waniletee popote nilipo.

Mimi nakata Bima ambayo ndani yake pia kuna Bima ya Maisha kwa mwathirika. Yaani ikitokea nikakugonga ndugu zako au familia yako watashukuru sana wakija gundua kuwa wanakuja lipwa Mil 500.

Fikiria mwenyewe. Wakati upo hai ulikuwa unawapa tu mzigo kuomba omba pesa,kudoea chakula n.k sasa umekufa wanalipwa Mil 500 na Bima.hii ni ndani ya masaa 24 tu wala haina mjadala. Kikitolewa tu cheti cha kifo na report ya Traffic. Waliobaki wataulizwa tu Account number basi.

So utagundua kwa kifo chako wao wanapona. Hili huwa sipendi waambia wengi sababu najua wanaweza wakawa wanajigongesha makusudi. Imagine ndo mkeo anajua kuwa sababu ya wewe kufa yeye analipwa na watoto mil 500? Si atakuombea sana uwekwe mahali pema peponi?

Lakini pia najua hata ile chuki ya kuwa nimegonga na kuua mume/mzazi n.k itakuwa haipo. Zaidi anaweza nishukuru. Familia nyingine wanaweza wakawa wanataka niwe nawagonga tu kadiri niwezavyo.

Haya maisha kuna watu wanaishi kwa shida. Mtu anafanya kazi mpaka jumamosi mwisho wa mwezi analipwa tsh 2,000,000. Unajiuliza Mil mbili ataishije huyu na ana mtoto na mke? ana ndugu, jamaa na marafiki? Na Serikali itakusanyaje mapato hapo?huwa nawaza sana.

Sasa ikatokea bahati mbaya mtu kama huyu ndo kapata ajali. Ndugu zake wanaweza shukuru baada ya kuambiwa wakasaini check ya mil 500.

Jamani Bima si kwa ajili ya Traffic. Ni muhimu sana kukata Bima. Bima zenyewe si gharama sana kwa huo usafiri wenu. Mimi huwa Bima inakatwa moja kwa moja naletewa tu na kubandikiwa kwenye Kioo. hapo baada ya Mkurugenzi kunipigia simu kunijulisha kuwa anaomba ajue nilipo aje yeye mwenyewe kunibandikia ile sticker maana hawaamini sana vijana wake kama watabandika vizuri ikawa smart. Anakuja anabandika ananishukuru anaondoka.

Tusiache kukata Bima ndugu zanguni.nlimsaidia yule Bwana mdogo kwa kumchangia Tsh 400,000 ampe jamaa aliyekwaruzwa ambaye alitaka tsh 200,000 kurudia rangi kasehemu husika. Njiani nimewaza sana. Nikasema niwaambie ndugu zanguni ukiweza kukata na Bima ya maisha ni vyema. Unalipia Mil 100 kwa mwaka kwa ile ndogo tu. Hapo ukipata ajali au ukiumwa ukafa familia yako inakuja lipwa Bil 1. Si mbaya. Mimi nimekata kubwa zaidi ya hiyo. Si lazima ukate yangu ya kulipia tsh Mil 500 kwa mwaka
Game Changer and The Entertainer.
 

cocastic

JF-Expert Member
Nov 30, 2019
21,789
2,000
Huyu mwandishi kama sijakosea aliwahi kuja na uzi wake kuwa alikwenda na Ranger yake kununua samaki wa shilingi 700,000 ferry kwaajili ya matumizi ya nyumbani, yote hiyo ilikuwa ni hasira baada ya kuona muuzaji amemwacha yeye na kumhudumia mwanamke wa kimanga
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom