Hili ni tatizo gani? Nikimaliza kuoga nawashwa sana

Dah mkuu linawasha sana mm kwa wiki naogea dodoki mara moja tu kwa kuvizia kuepuka hiyo adha.

Kwani sabuni peke yake si inatosha mkuu ukipaka ukaoga si fresh tu mkuu au?
sabuni tosha sana mkuu. Sema mara moja kwa wiki ukiwa na muda unatumia then full kugala gala kitandani na muwasho. Ila kuna kitu nimejifunza juzi pia, taulo lilikuwa safi ndiyo natumia kwa mara ya kwanza toka lifuliwe na nilitumia dodoki halikuwasha kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani taulo bei gani? Badilisha ukipona leta mrejesho ukibadili ikiwa bado tuambie hapa wengi wanaelimika. Mimi ghafla nilipata kuwashwa na hasa mgongoni na ubavuni. Ilinichukua muda kujua ni taulo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yawezekana tatizo lako likawa ni aquagenic urticaria hii inatafasiriwa kwamba una allergy ya maji, na wataalamu wanasema tatizo hili halina tiba, lakini unaweza kulipunguza sana kwa kuoga maji ya moto au vugu vugu na pia hakikisha unaoga kwa muda mfupi kadiri iwezekanavyo na jitahidi ukishamaliza tu kuoga hakikisha mwili umeufunika vizuri usipate upepo au baridi.
Pia nivizuri ukanunua bathrobe. Na ikiwa adha ya muwasho itaongezeka tafuta strong anti allergies kama LORATIDINE ama nyingine kama hiyo.
Asante kwa ushauri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dokta moja aliwahi kuniambia muwasho baada ya kuoga unaweza kusababishwa na kujisugua na madodoki au kujifuta na taulo mpaka panatokea michubuko midogo sana isiyoonekana kwa macho... Kwahiyo nikushauri usijifute na taulo wala usijikwangue na dodoki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mtu aliwahi kuniambia kwamba njia nzuri ya kujifuta maji kwa taulo sio kupurula puu kama unafuta.bali uwe kama unapamba hivi au unaweka nukta hapo hapatotokea mchubuko

Lakini taulo jepesi dah haiwezekani.
 
Back
Top Bottom