Hili ni tatizo gani? Nikimaliza kuoga nawashwa sana

charrote

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
914
1,000
Habari za alasiri,

Kama nilivyoeleza hapo juu ,nimekuwa nikwashwa kila ninapomaliza kuoga. Muwasho huu huchukua takribani nusu saa ndipo nakuwa kawaida. Mwanzoni nilifikiri ni sabuni ninayotumia nikabadili na nimeshabadili sabuni za aina nne tofauti lakini bado nawashwa.

Nikijikuna hakuna alama yoyote inayotokea,


Naoga maji safi na muwasho unatokea kabla sijapaka mafuta/ losheni. Mwenye kuelewa tatizo hili anisaidie .

Sent using Jamii Forums mobile app

MAONI YALIYOTOLEWA NA MDAU

Yawezekana tatizo lako likawa ni aquagenic urticaria hii inatafasiriwa kwamba una allergy ya maji. Wataalamu wanasema tatizo hili halina tiba, lakini unaweza kulipunguza sana kwa kuoga maji ya moto au vuguvugu. Pia hakikisha unaoga kwa muda mfupi kadiri iwezekanavyo na jitahidi ukishamaliza tu kuoga hakikisha mwili umeufunika vizuri usipate upepo au baridi.

Pia ni vizuri ukanunua bathrobe. Na ikiwa adha ya muwasho itaongezeka tafuta strong anti allergies kama Loratidine ama nyingine kama hiyo.
 

Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
26,671
2,000
Kwanza naomba nikukumbushe kwamba, sio kila maji safi ni salama.

1. Je unaongea maji ya bomba ama kisima?

2. Je upo mkoa/ wilaya gani?

3. Je mkoa/ wilaya uliopo, unauhakika maji hayana chumvi?

4. Je unauhakika kama maji unayo yaoga hayapo contaminated na chochote?
 

Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
26,671
2,000
Maji ya bomba, chanzo ziwa Victoria

Sent using Jamii Forums mobile app
Yawezekana tatizo lako likawa ni aquagenic urticaria hii inatafasiriwa kwamba una allergy ya maji. Wataalamu wanasema tatizo hili halina tiba, lakini unaweza kulipunguza sana kwa kuoga maji ya moto au vuguvugu. Pia hakikisha unaoga kwa muda mfupi kadiri iwezekanavyo na jitahidi ukishamaliza tu kuoga hakikisha mwili umeufunika vizuri usipate upepo au baridi.

Pia nivizuri ukanunua bathrobe. Na ikiwa adha ya muwasho itaongezeka tafuta strong anti allergies kama LORATIDINE ama nyingine kama hiyo.
 

SMART PASSENGER

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
550
500
Una matatizo kwenye immune system, ngozi ndiyo first line ya immune system kuwasha inategemea histamine zinaachiwa kupambana na vitu ambavyo mwili wako haukubaliani navyo inaleta allergy reaction au immune system inapungua na histamines inatolewa kupambana.
Kwa nini iwe ni baada ya kuoga tu kama tatizo ni immune system

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Swet-R

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
3,430
2,000
Hiyo hali ilikuwa inanitokea zamani,lakini ikapotea yenyewe. Ilikuwa nikimaliza kuoga najifuta haraka na kupaka mafuta,inaacha. Lakini baadae ikapotea kabisa. Na ukiifikiria hiyo hali ndio inazidi. Kwanza usioge maji ya mvua ndio unaweza kuwashwa sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom