Hili Ni Somo Kwa Viongozi Wa "Tanzania" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hili Ni Somo Kwa Viongozi Wa "Tanzania"

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mjunguonline, Jun 21, 2011.

 1. mjunguonline

  mjunguonline Member

  #1
  Jun 21, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mahakama ya Tunisia imemtupa jela aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Zine al- Abidine Ben Ali.

  Adhabu hii hataitumikia peke yake kwani mahakama hiyo ilionelea haitakuwa vibaya akiambatana na mkewe, Leila. Wawili hawa wamehukumiwa kufuatia makosa yao ya ufujaji wa mali za umma.

  Wawili hawa walitimkia nchini Saudi Arabia mwezi Januari kufuatia mapinduzi ya umma yaliyowakimbiza kutoka katika kiti cha neema. Wamepigwa pia faini ya dolari za Kimarekani 66 Milioni.

  Mahakama hii ilifikia uamuzi wake kufuatia kesi iliyoendesha kwa siku moja ambayo ilihusiana na dolari milioni 27 na vito vya thamani ambavyo vilikamatwa katika baadhi ya makasri waliyokuwa wakiishi.

  Kesi nyingine ilikuwa ikimhusu Ben Ali peke yake, kesi ambayo inahusiana na umiliki wake wa madawa ya kulevya na silaha. Kesi hii ilipigwa kalenda.

  Mwanasheria wa Ben Ali alisema uamuzi uliotolewa na mahakama hiyo umekuwa wa kisiasa zaidi, na alifikia hatua ya kuuita 'a Joke'.

  Mwandishi wa habari wa BBC, Jon Leyne, ambaye yuko nchini Tunisia amesema ni ndoto kufikiria kwamba Saudi Arabia watamrejesha kwa nguvu Ben Ali kutumikia adhabu yake.
   
Loading...