Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,428
Mada hii imechangiwa na mawazo ya wana jf kadhaa akiwemo FaizaFoxy na wenzake ambao washawahi kuyatoa huko nyuma katika nyakati na mazingira tofauti tofauti.
===============
Beberu “Mbuzi dume aliyekomaa”. Sina uhakika kama walioita nchi zilizoendelea kiuchumi jina hili walifikiri kwa kina, na kama walifikiri kwa kina ni vigumu kuelewa walilenga nini kuwaita jina hili.
Hivi siku mzungu akakusikia unamuita beberu, akakuuliza, what is the meaning of “Beberu” ?utamuauambia “Matured male goat”? akikuuliza “Why you call us “Matured male goats? And if we are matured male goat, what we may call you?” utajibu nini?
Kumbuka kila kitu kina kinyume chake, unapomchagulia mtu jina anaweza pia kukuchagulia jina na wakati mwingine hata asipokuchagulia jina, unaweza kujichagulia mwenyewe bila kukusudia na pengina bila kujua.
Ni sawa na unawaambia watu 'yule jamaa tunalingana kimri ila yeye ni kijogoo'. Au unasema 'huyu mtu tulisoma naye ila yeye ana akili', au unasema 'sote wanaume ila huyu yeye ana nguvu' au unasema 'huyu jamaa ni mwamba' n.k ijapokuwa unakuwa unamwelezea yeye; bila kukusudia pia unakuwa unajielezea wewe.
Nashauri hii lugha ya mabeberu ni bora tukaangalia kama inafaa kuiacha. Lugha hii inatuathiri zaidi sisi tunaoitumia kuliko wale tunaowaita. Inatujengea unyonge usio wa lazima. Nashauri ni bora tu kuwaita 'nchi zilizoendelea kiuchumi…….. (kisha unaendelea unachotaka kusema)'
Ila atakayeona ushauri huu si sahihi, anaweza kuendelea kuwaita mabeberu ila ajue wakati anafanya hivyo, anasababisha mambo mengine mawili bila kukusudia; Kwanza na yeye anakuwa anajiweka kwenye kundi fulani bila kukusudia wala kutamka na pia kujijengea unyonge wa kifikra. Ni ushauri tu ndugu zangu.