Hili neno 'Mungu si Athumani'

Luhungu

JF-Expert Member
Sep 5, 2013
816
232
Wanajanvi,

Hebu leo nijuzeni.

Neno Mungu si Athumani, ni msemo wa tangu na tangu.

Naomba kujua, huyu Athumani ni nani, asili yake wapi hata atumiwe katika heshima ya Mwenyezi?
 
Nadhani alitaka ulinganishi kama vile "ukistaajabu ya Mussa utashangaa ya Firauni" hawa wanaeleweka mikasa yao
 
Mungu si MTU...athumani ni kiwakilishi tu cha ordinary people(tom,sick and hurry!!!)
 
Nadhani anatamani kujua huyu binadamu Athumani aliyewekwa kwenye ulinganishi huu ana wasifu gani?! Mfano Ukisema Farao watu wanapata reflection, sasa huyu Athumani inakuwJe. Nadhani aliyepost kamaanisha hivyo

Haswaaaaa
 
Wanajanvi,

Hebu leo nijuzeni.

Neno Mungu si Athumani, ni msemo wa tangu na tangu.

Naomba kujua, huyu Athumani ni nani, asili yake wapi hata atumiwe katika heshima ya Mwenyezi?
Baada ya enzi ya manabii na mitume kufikia hatma yao!! Bw. Athuman radhi za Moula zimfikie..kwa kuwa ndiye aliyekuwa mrithi wao " hivyo Athumani alikuwa mtu mwema,mkarimu,Mstahamilivu na Mwajibikaji na mwenye sifa za utu " Hadi kufikia utukufu huo ndipo ikapigwa methali hiyo!!
 
Mungu si Luhungu...

Pia ni msamiati tu, kama vile kusema Abdallah kichwa wazi...
 
Baada ya enzi ya manabii na mitume kufikia hatma yao!! Bw. Athuman radhi za Moula zimfikie..kwa kuwa ndiye aliyekuwa mrithi wao " hivyo Athumani alikuwa mtu mwema,mkarimu,Mstahamilivu na Mwajibikaji na mwenye sifa za utu " Hadi kufikia utukufu huo ndipo ikapigwa methali hiyo!!
Bwana Athumani alikuwa anaishi wapi na ilikuwaje akawa mrithi wa manabii?
 
Back
Top Bottom