Hili neno "literal" maana yake nini?

Pastory Kimaryo

JF-Expert Member
Jan 16, 2018
967
664
Habarini za asubuhi wana lugha JF.

Hili neno "literal" na kielelezi chake "literally" maana zao halisi ni zipi na huwa zinatumika kumaanisha nini kwenye sentensi maana nimekuwa nafuatilia Google na kwingine lakin siambulii kitu labda mnieleweshe kwa kiswahili.
 
Unaweza kulitafsiri kama 'kwa maanawia.'
 
Neno literally huwa linamaanisha kuwa kitu kimefanyika bila manipulations,bila kukikuza kwa hisia za kibinadamu,bila kulazimisha kuwa kimefanyika, bila kufoji kuwa kimefanyika, bila kuongezea chumvi!

Mfano:
Seconds literally ticked away on the old grandfather clock in the next room.Hii kauli maana yake ni kwamba babu hali yake ya afya ni mbaya sana/kwelikweli na amezidiwa na atakufa na hii ni kauli ambayo ipo serious na haijatiwa chumvi.Yaani mtu akikuambia hivyo maana yake wewe andaa geneza la kumzika babu!
 
Habarini za asubuhi wana lugha JF.

Hili neno "literal" na kielelezi chake "literally" maana zao halisi ni zipi na huwa zinatumika kumaanisha nini kwenye sentensi maana nimekuwa nafuatilia Google na kwingine lakin siambulii kitu labda mnieleweshe kwa kiswahili.

Neno "literal" unaweza kusema ni sawa na neno "dhahiri" katika kiswahili, mfano; He literally swallowed a piece of stone to show his bravery, yaani Alimeza kidhahiri kipande cha jiwe kuonyesha ujasiri wake.

Mfano, He literally rose to the sky like a bird, Yaani, kidhahiri alipaa angani kama ndege., hapo nimesema kidhahiri (literally) kwakuwa sio jambo la kawaida mtu kupaa angani kama ndege au mtu kumeza jiwe.

Mfano, When it is said that someone has let his cat out of bag, this sentence needs not be taken in a literal rather in a metaphorical sense, yaani, inaposemwa kwamba mtu fulani amemtoa paka wake kutoka katika begi, sentensi hii isichukuliwe katika maana ya dhahiri (maana ya moja kwa moja) bali ichukuliwe kwa maana ya fumbo/majazi. (To let a cat out of bag maana yake metaphorically ni kutoa siri) hiyo ni proverb ya kiingereza.

Hapo sasa utaona kinyume cha neno literal ni metaphor, literal ni dhahiri, wazi au maana ya moja kwa moja (straight forward) na metaphor ni fumbo, majazi, mfano, tamathali nk.
 
Ni DHAHIRI timu ya Namungo FC imeyaaga mashindano ya CAFCC.
-
KIUHALISIA tulifahamu timu ya Simba SC itafuzu mashindano ya CAFCL.
-
Pastory Kimaryo amekuwa akihoji masuala kadhaa, KIUHALISIA wengi hawakufahamu hili.
-
Liverpool ilionekana kuisumbua Arsenal ni DHAHIRI timu hii ilimkosa Xhaka kama mtu muhimu.
 
Dah, wewe nimekuelewa sana
 
Habarini za asubuhi wana lugha JF.

Hili neno "literal" na kielelezi chake "literally" maana zao halisi ni zipi na huwa zinatumika kumaanisha nini kwenye sentensi maana nimekuwa nafuatilia Google na kwingine lakin siambulii kitu labda mnieleweshe kwa kiswahili.
Huna haja ya kujua neno hilo kwa kiswahili, lakini ili kujua kwa maana yake, twende pamoja na ndugu wa neno LITERARY ambaye ni FIGURATIVE.

Kuna maneno ambayo huzungumzwa kwa Idioms ambazo zinaweza kuwa na shida kwa kiswahili kuna sentensi kama 'Amempaka mafuta kwa mgongo wa chupa' hii ni figurative kwa kinachozungumzwa bali kinakupa picha nyingine

Lakini mtu akikuambia Literary jamaa amepakwa mafuta kwa mgongo wa chupa, maana yake unaondoa ile Idiomatic meaning ambayo iko attached na kujua kuwa ni kweli jamaa kapakwa mafuta

Hivyo kama neno Literary linakupa tabu kulielewa zaidi nenda pamojana ndugu yake Figurative
 
Uhalisi. Mfano rahisi zaidi ni kwenye uzi maarufu wa wahuni hapa JF: “Umeshawahi kula tunda kimasihara ?”

Literally (kiuhalisia), ingekuwa ni kula tunda kama embe, papai, chungwa, nanasi, n.k. Lakini kwenye uzi huo “tunda” na “kula” zimetumika kama tafsida kukwepa panga la moderators. Kiuhalisia, tunda haliliwi kimasihara.
 
Huna haja ya kujua neno hilo kwa kiswahili, lakini ili kujua kwa maana yake, twende pamoja na ndugu wa neno LITERARY ambaye ni FIGURATIVE.

Kuna maneno ambayo huzungumzwa kwa Idioms ambazo zinaweza kuwa na shida kwa kiswahili kuna sentensi kama 'Amempaka mafuta kwa mgongo wa chupa' hii ni figurative kwa kinachozungumzwa bali kinakupa picha nyingine

Lakini mtu akikuambia Literary jamaa amepakwa mafuta kwa mgongo wa chupa, maana yake unaondoa ile Idiomatic meaning ambayo iko attached na kujua kuwa ni kweli jamaa kapakwa mafuta

Hivyo kama neno Literary linakupa tabu kulielewa zaidi nenda pamojana ndugu yake Figurative
Huu ndio ufafanuzi sahihi mkuu. Hongera.
 
Ni DHAHIRI timu ya Namungo FC imeyaaga mashindano ya CAFCC.
-
KIUHALISIA tulifahamu timu ya Simba SC itafuzu mashindano ya CAFCL.
-
Pastory Kimaryo amekuwa akihoji masuala kadhaa, KIUHALISIA wengi hawakufahamu hili.
-
Liverpool ilionekana kuisumbua Arsenal ni DHAHIRI timu hii ilimkosa Xhaka kama mtu muhimu.
Kwanini wasiende Mombasa?
Au Msumbiji?

Ni dhahiri hakuna Nchi inayoweza kukubali mradi huu
 
LET ALONE...nayo ina maana gani..
Ni kama vile "achilia mbali" au "sembuse"

E.g Jamaa alishindwa kuongoza shule sembuse kuongoza nchi?
Screenshot_20210414-145615.png
Screenshot_20210414-145609.png
 
Habarini za asubuhi wana lugha JF.

Hili neno "literal" na kielelezi chake "literally" maana zao halisi ni zipi na huwa zinatumika kumaanisha nini kwenye sentensi maana nimekuwa nafuatilia Google na kwingine lakin siambulii kitu labda mnieleweshe kwa kiswahili.
Tuchukue hili neno:
Abdallah
(Abd Allah, literally The Follower of God, in Islamic teachings)
Hutumika kufafanua jambo kwa undani!
Kwa mfano mdogo ni Mwananyamala, ukimfafanulia mtu kwa Kiswahili kuwa ni Neno la Kibantu Likimaanisha Mtoto Nyamaza, sasa LIKIMAANISHA kwa kiingereza wangesema LITERALLY-CHILD STOP CRYING!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom