Hili Neno kutoka kwenye Biblia Takatifu lilinijia muda nikiwa usingizini.

GJHariohay

JF-Expert Member
Oct 24, 2013
1,041
1,160
Mithali:28.16
Mkuu aliyepungukiwa na akili huwaonea watu sana; ....

Mwana JF anaeweza kutafsiri Biblia vema atusaidie.

Nimepost kwenye jukwaa hili la Siasa nikiwa na maana kubwa sana, moods msiondoe huu uzi hapa.
 
Hilo ni neno lenye pumzi ya Mungu. Ikiwa baba au msimamizi katika taasisi yeyote anatumia nguvu kutatua changamoto mbali mbali maana yake hana namna nyingine ya kutatua. Ila baba au kiongozi mwenye akili na hekima hutatua changamoto zilizopo bila kutumia nguvu.
 
Siku zote mfalme asiye pendwa na watu wake hutawala kwa mabavu ili apate kujilipiza kisasi kwa wao wamchukiao, nae mikono yake hujaa damu, na moyoni mwake hutamani kuisulubisha nchi ili watu wamwinamie na kumsujudia kwa kuogopa uovu wake, wanafiki na mahayawani humzunguka na kusifu njia zake za uovu, amini nawaambia Mungu wa majeshi husikia kilio na maumivu yao watesekao na kumlilia, nae huachilia mvinyo wa ghadhabu yake kulipa kisasi cha watu na damu imwagikayo bila hatia.
 
Ikiwa ni kweli neno hilo umelipata usingizini ndotoni ni maono. T
Tazama imeandikwa Mungu hataweza kufanya lolote kwa mtu au nchi kabla hajawafunulia watu wake.
Kuyaona hayo ni kufunuliwa means wewe ni mtu wake. Unapewa taarifa ili useme kama hivi. Huo si mwisho endelea kuomba Mungu atakuonesha sura ya mambo yote yaliyo mbele ktk taifa lako.
Usibeze ndoto zako. Njia pekee na ya siri ambayo Mungu husema na wanadamu ni njia ya ndoto. Ubarikiwe mno ndg, Mungu ana makusudi nawe haijalishi ukoje amini wewe ni wake na anataka kukutumia utende mapenzi yake.
Simamia kweli nayo itakuweka huru.
 
GJHariohay ,
Mkuu unaweza ikawa uko sahihi ila angalia sana mambo ya usingizini, ndoto, maono na fikira huwa havianikwi.

Maana, hawa hawakawii kuku Godblesslema...

Naamini, umenielewa na wasomaji wote watanielewa.
 
Hahahaha
Hiyo ni kuzimu!
Fanya toba ni maono ya nyumbani kwako
Laana inatamalaki kwenu!
 
Ikiwa ni kweli neno hilo umelipata usingizini ndotoni ni maono. T
Tazama imeandikwa Mungu hataweza kufanya lolote kwa mtu au nchi kabla hajawafunulia watu wake.
Kuyaona hayo ni kufunuliwa means wewe ni mtu wake. Unapewa taarifa ili useme kama hivi. Huo si mwisho endelea kuomba Mungu atakuonesha sura ya mambo yote yaliyo mbele ktk taifa lako.
Usibeze ndoto zako. Njia pekee na ya siri ambayo Mungu husema na wanadamu ni njia ya ndoto. Ubarikiwe mno ndg, Mungu ana makusudi nawe haijalishi ukoje amini wewe ni wake na anataka kukutumia utende mapenzi yake.
Simamia kweli nayo itakuweka huru.
Amen Amen Amen.
 
Back
Top Bottom