Hili ndio kosa la Rais Magufuli, kujijenga kama Taasisi ndani ya Taasisi!

lanez

Member
Apr 18, 2019
78
163
Kwa tafsiri inayofahamika, taasisi ni chombo kinachofanya kazi kwa kushirikisha watu wengi, ili mambo yaende. Kutokana na kufanya kazi kitaasisi basi hupelekea ufanisi zaidi. kwenye somo la Principle management tunafundishwa umuhimu wa kufanya kazi kitaasisi ili kuongeza ufanisi.

Vyama vya siasa kama CCM ni taasisi , hivyo huitaji kuendeshwa kitaasisi na kutokumtegemea mtu ili taasisi isimame. Wote tunafahamu CCM ni taasisi kubwa, na yenye kila aina ya rasilimali watu na vitu toka kuanzishwa kwake. Lakini kwa miaka mitano ya utawala wa Mh Magufuli kama mwenyekiti wa CCM, CCM imekuwa hijiendeshi kitaasisi tena, bali hutegemea mtu mmoja tu, ambaye ni mwenyekiti wake Magufuli. Hili ni moja la kosa kubwa, alilolifanya Mh. Magufuli, kuigeuza taasisi kubwa kama CCM kumtegemea mtu mmoja.

Huu ni ushahidi, wa Mh Magufuli kuigeuza CCM kumtegemea mtu mmoja.
Toka aingie kwenye uongozi wake, mara nying Mh Magufuli amekuwa akijitaja "yeye" Na sio "Sisi " mfano

nitakuteua
Unaweza ukapita huku, lakini kule nikakukata
Nimemkata mtoto wa Dada yangu, nimemteua Gwajima.
Nimeamua kutengeneza vitambulisho mimi mwenyew
Sifanyi hiki nafanya hiki, sipangiwi n.k

Kwa wanaofatilia hotuba za Mh Magufuli, hizo kauili ni kawaida kuzisikia, kitu ambacho kimeleta madhara makubwa, ndani ya CCM. Unaweza ukajiuliza ni matatizo gani hayo, lakini kwa kawaida binadamu usipo wa "acknowledge " kwenye jambo ambalo mmefanya pamoja, huwa wanakuwa "disappointed "sana. Inawezekana wasiseme lakini moyoni wanaumia, hivyo kuendesha mgomo kisiri siri ili waone kama unaweza fika peke yako.

Madhara ya Mh Magufuli, kujijenga kama Taasisi ndani ya Taasisi, yalikuwa na madhara ya muda mrefu, pengine ilikuwa ngumu kuyakugundua kipindi kile, lakini kipindi hiki cha uchaguzi yameonekana wazi, yameonekanaje, basi fuatilia hapa chini.

kipindi hiki cha uchaguzi, ambacho Mh. Magufuli, amekili kuna maeneo hatofika pamoja na kupumzika sana kwa kampeni zake, tulitegemea basi katibu uenezi na katibu mkuu, kuendesha mikutano mikubwa mikoani chini ya mwamvuli wa wagombea ubunge. Kipindi cha Kikiwete ilikuwa kawaida kumuona nape na kinana wakifanya mkutano mkubwa mikoani bila hata uwepo wa Mh kikwete, hii ilitokana na CCM kuendeshwa kitaasisi.

Wagombea ubunge wengi wa CCM, mikutano yao imekuwa ya kinyonge mno huko mikoani na ndio maana hata hatuoni picha za wagombea ubunge CCM wakiwa wamejaza watu wengi. Hili pia limesababishwa na kumtegemea Mh Magufuli pekee.

mikutano ya mgombea Makam Rais na Waziri mkuu, bado haina hadhi ile ya CCM ya kipindi cha nyuma. Zaman ilikuwa inatosha kabisa mkutano wa mgombea urais, kinana, Nape na January makamba kutikisa mkoa mzima, lakini leo kinyonge mpaka Mh Magufuli awepo.

Mwisho, watu wamshauri Mh Magufuli airudishe CCM kujiendesha kitaasisi, aachane na maneno "CCM ya Magufuli" mara "serikali ya Magufuli " kwani akishinda Leo, ataisababishia ugumu CCM mwaka 2025. Hata Marehem Benjamin mkapa, aliwai kuonesha kuchukizwa, na kujimilikisha CCM na serikali kama anavyofanya Mh.

"Maendeleo hayana vyama "
 
Mkuu Pitia bandiko la Ole Mushi kuhusu Inzile,Gweregwere na Mafikizolo.



Iko hivi; baada ya uhuru wa Zimbabwe kupatikana kulitokea vita vya kugombea madaraka miongoni mwa wapigania uhuru ndani ya ZANU-PF. Kundi la kwanza ni waliopigania uhuru wakiwa ndani ya Zimbabwe msituni wakijiita "Mafikizolo" kwa lugha ya Shona, kabila kubwa nchini humo kumaanisha "wazawa", "wenyeji" au "alwatan" yaani wanaokijua ZANU-PF kuliko mtu mwingine. Kwa CCM hawa ndio "vingunge" wa chama. Hapa ndipo alikuwepo Gabriel Mugabe. Walijiona bora kuliko wengine.

Kundi la pili liliitwa "Inzile" kwa maana ya "wakuja" ambao walizikimbia familia zao na kwenda uhamishoni kama tuliowahifadhi pale Kongwa. Hawa nao walijiona ni mashujaa waliostahili kupewa viti vya mbele japo wenzao Mafikizolo waliwaona kama waoga wasiostahili kupendelewa. Vita hii ya Mafikizolo na Inzile imekitesa mno ZANU-PF kwa miaka mingi hasa nyakati za uchaguzi. Emerson Mnangagwa ni Mafikizolo. Jeshi linapendelea kundi hili.

Vita hiyo imehamia CCM kwa sasa. Ni vita kubwa Kati ya "Mafikizolo" yaani waliolelewa na kukulia CCM dhidi ya wale wasioijua CCM na tendegu zake. Tunakumbuka JPM ndani ya chama kabla ya kugombea aliambiwa hakijui CCM maana hakuwahi hata kuwa mjumbe wa kamati ya siasa ya wilaya hivyo ni "Inzile" tofauti na kina Lowassa "Mafikizolo" na Membe wanaokijua chama nje ndani. Lakini sasa chama kimekamatwa na "Inzile" kina Bashiru, Polepole, Makonda, Cyprian nk ndio maana huwasikii kina Mangula "Fikizolo". Hii ni vita.
Anga za uchambuzi zinaeleza kwamba hiki kinachoitwa "CCM Mpya" ni harakati za "Inzile" kujiimarisha na kuwatupilia mbali "Mafikizolo" wanaoonekana kuendesha harakati zao kisayansi zaidi.

Hatari inayoikumba "Inzile" ni kwamba imekosa uungwaji mkono na "Mafikizolo" na hivyo kutafuta nguvu nje ya chama na ndipo ilipoanza biashara ya "kuunga mkono juhudi" kutoka upinzani. Tukaanza kuona wapinzani wakiingia CCM kwa gharama kubwa ya walipa kodi na kupewa vyeo kwa mkakati maalumu kama alivyofafanua DC Richard Kasesera wa Iringa Mjini.

Hawa wahamiaji kutoka upinzani kuja CCM kishona au Kizulu huitwa "Gweregwere" yaani wakimbizi wa kiuchumi. Waliokimbia makwao kusaka "green pasture". Gweregwere ni hatari mno maana kimsingi yeye hajui itikadi wala misingi ya chama maana kilichomleta ni njaa na hivyo anahitaji shibe. Hawa ndio kina Mollel, Waitara, Kafulila na wengine unaowajua. Hatari iliyopo CCM ni kwamba "Gweregwere" nao wameanza kujiimarisha ndani ya chama ili litambuliwe kama kundi halali lenye akili kuliko wenyeji: Mafikizolo na Inzile. Kwa mantiki hiyo liko tayari kufanya lolote la kufurahisha "Inzile" ili wakubalike. Ningeshangaa kama Mollel angesema tofauti na aliyoyasema maana kundi hili linatafuta udhaifu wa Inzile na hupiga hapo hapo.

Kwa mfano; Serikali na chama tumeshindwa kumjibu Lissu kiasi cha mkuu wa chama kudai "Lissu anadeka" kauli ya ajabu kabisa kwa kada ya msomi wa PhD. Kwa sababu hiyo "Gweregwere" kwa kuwa waliwahi kuishi na Lissu wanapokuja na "siri" kuhusu Lissu mara moja hukubalika lakini Mafikizolo wanacheeeka! Sitoshangaa kauli zingine kutoka kwa "gweregwere" kuhusisha CHADEMA na kushambuliwa Lissu maana kwa kusema hivyo Inzile hupumua. Sasa "gweregwere" linatafuta aliyeng'oa CCTV camera. Hili la kuondoa askari lindoni linawasumbua nadhani wakilipatia watapata neema ambayo ndiyo shabaha yao.

Vijana ndani ya CCM hawafurahishwi na ugeni wa "gweregwere" wa kupewa vyeo ilhali wao wapo. Hawasemi ila wamenuna sana maana wanajiona si lolote mbele ya "gweregwere" kwa sasa. Wanashangaa hata waliokatwa mikia wakiwekewa mikia bandia ili tu wajae pishi. Kwa mantiki hiyo tusishangae maneno ya hovyo kutoka kwa "gweregwere" maana ili wakubalike kutoa "siri" za huko walikotoka hata kama ni za kubumba "Inzile" itapona jeraha lisilopona.

Bado ninaamini zipo njia za kupangua hoja za Lissu lakini tukiamua kuabudu kwenye altare ya ukweli, masamaha na kushikana mikono kama Raila na Kenyatta kujenga Tanzania. Yaliyopita si ndwele tugange yajayo ni kauli inayoweza kumfanya bubu Tundu Lissu lakini si piga nikupige hata ya kina Musukuma. Ametushika pabaya, ngoma inazama! Vijana CCM tuendelee kuwapinga "gweregwere" tukishindwa basi tuwanunie tu watajua kuwa hatuwapendi!
 
Unaota mchana siyo, uje hapa baada ya kupiga kura yako,
Mwanzoni nilikua nashangaa kwanini baadhi ya watu humu hushangilia misiba au matatizo ya kundi flani la watu, nikaja gundua kuwa uonevu huzaa chuki na visasi kwenye mioyo ya watu. Unamcheka anayepigwa na polisi leo, kesho usitegemee akaja kulia kwenye msiba wako.
 
Nyie endeleeni kuota ndoto za mchana.Uchaguzi wa mwaka huu ni rahisi kuliko yoote .Ni wabunge gani hao wanaofanya kampeni kwa unyonge! Subiri tarehe 28.Chadema wakiwa wabunge wengi basi watakuwa 5 Nao ni Prof J, SUGU, Wenje,Heche na.Tena hata hawa ni kwa bahati sana
 
Kwa tafsiri inayofahamika, taasisi ni chombo kinachofanya kazi kwa kushirikisha watu wengi, ili mambo yaende. Kutokana na kufanya kazi kitaasisi basi hupelekea ufanisi zaidi. kwenye somo la Principle management tunafundishwa umuhimu wa kufanya kazi kitaasisi ili kuongeza ufanisi...
Kukwambia Asante tu kunatosha mkuu.
 
Back
Top Bottom