Hili ndio Kaburi la Elimu kwa Watoto wa Maskini

Hansen Nasli

JF-Expert Member
Mar 18, 2012
883
337
KABURI LA ELIMU KWA WATOTO MASKINI

KUPANDISHA viwango vya ufaulu bila uboreshaji wa elimu ni kuwazika watoto wa kimaskini ili waagane na elimu ili kesho waje kuwa wapambe na watumwa wa watoto wa viongozi wa sasa na wale wa matajiri.

Kabla hamjasimamia mipango yenu, hebu nanyi waleteni watoto wenu wasome na watoto wetu shule za umma (shule za kata).

Acha niwape kisa cha binti wa kijakazi aliyekuwa akiwania umalkia katika Taifa la Azania.

Katika Taifa la Azania alitokea mfalme ambaye maisha yake yote hadi anafika uzee hakubahatika kupata mtoto. Mfalme alitaka akiondoka duniani awe amempata mrithi wake ili aiche nchi salama.

Mfalme aliona awamu inayokuja iongozwe na mwanamke aweze kuwa malkia wa Azania. Mfalme alimwagiza msaidizi wake asimamie mchujo kisha mchujo nao ulimalizika kwa kuwapata mabinti wawili mmoja binti wa kiongozi na mfanyabiashara maarufu na wa pili akawa wa kijakazi, kwa hiyo lazima apatikane mmoja aweze kuwa malkia.

Mfalme akapanga siku ya zoezi la kumpata Malkia wa Azania na siku ilipowadia, mfalme aliwapatia zoezi dogo la kusaga mahindi apate unga wa ugali. Mfalme aliwaletea kiroba cha mahindi kila mmoja, akawatuma wakasage mahindi hayo wamletee unga kabla jua halijazama.

Binti wa kiongozi na mfanyabiashara maarufu alikwenda kwa wazazi wake na kuomba fedha za kusaga mahindi hayo kwa mashine na kufanikiwa kusaga na kuwahi kurudi kwa mfalme.

Mtoto wa kijakazi naye alimfuata mama yake kuomba ampatie fedha za kusaga mahindi hayo, mama yake alimpatia jiwe. Binti wa kijakazi alisaga mahindi hayo kwa taabu na nguvu kubwa kwa kutumia jiwe akapata unga na kuupeleka kwa mfalme.

Baada ya kufika kwa mfalme, aliwapokea na kuwapa chekecheo la kuchekecha unga huo kila mmoja akaanza kuchekecha. Binti wa kiongozi na mfanyabiashara maarufu alipata unga mwingi na chenga chache, yule wa kijakazi alipata chenga nyingi na unga mchache.

Ukweli ni kuwa binti wa kwanza alipata unga mwingi sababu alisaga kwa mashine na binti kijakazi alipata unga mchache kwa kuwa alitumia jiwe. Matokeo ya jumla mfalme alimtangaza binti wa kiongozi na mfanyabiashara kuwa Malkia wa Azania na binti wa kijakazi kwa juhudi kubwa aliambulia patupu.

Kisa hiki cha binti wa kijakazi nakifananisha na elimu ya Tanzania na matokeo haya ya kidato cha nne yanayoonesha watoto wetu wamefeli kwa takriban asilimia 70. Tujiulize tunawapeleka wapi hawa? .

Ushindani wowote ule unahitaji maandalizi ili uweze kushinda na ukiona baba au kocha wako anakupeleka kwenye mashindano makubwa yasiyoendana na maandalizi mazuri, ujue amepanga kukudhalilisha kama siyo kukudhalilisha ni kukuua kabisa.

Tujiulize kushindwa kwa binti kijakazi ni uzembe wake? Ujinga wa mama yake? au umaskini wao? Ila kwangu mimi kushindwa kwa binti wa kijakazi ni ujinga wa mfalme kutofikiria njia gani atumie ili zoezi litendeke kwa usawa.
Tuachane na hayo ya binti wa kijakazi na umalkia wa Azania, turudi hapa kwetu tuitazame elimu yetu ilipo na inapoelekea.

Serikali ya Awamu ya Tano imekuja na Waziri mpya Prof. Joyce Ndalichako.
Kama kawaida yetu, Watanzania tunawapima watendaji kwa majina na siyo mafanikio ya utendaji wao. Alipoingia tu akaanza kugombania suala la "Division" na "GPA" badala ya kuja na mpango mkakati wa kupandisha kiwango cha elimu kiweze kupanda juu na akashinda vita hiyo ya kurudisha "division" na kutupilia mbali "GPA" kwa kutumia mamlaka aliyonayo badala ya uhalisia.

Elimu ya nchi yetu imeshuka sana tena kwa kiwango cha juu, kuipandisha inahitaji muda.

Elimu bora inakuwepo pindi mambo yafuatayo yanapotekelezwa;

Mosi, Kuandaliwa Sera nzuri ya elimu inayotekelezeka.

Pili, Uandaaji mzuri wa walimu

Tatu, Kuwepo kwa zana za kujifunzia na ufundishaji kama vile vitabu vya kiada na ziada.

Nne, Mandhari nzuri ya kusomea na ufundishaji.

Hoja yangu ni juu ya upandishaji viwango vya ufaulu. Tumesikia Waziri wa Elimu Prof. Ndalichako ameturudisha katika mfumo wa madaraja, tafsiri nyepesi ni kuwa amepandisha viwango vya ufaulu.

Mtanishangaa sana kupinga kuwapima watoto wetu katika viwango vya juu, sababu ninazo na nitasimamia hata niwekewe kisu.
Viwango vya upimaji hupandishwa endapo elimu itazidi kuboreka. Dunia nzima inajua kuwa elimu yetu ipo chini. Wakati ni sasa tumwambie Mama Ndalichako aboreshe kwanza elimu iwe bora ndiyo apandishe viwango vya ufaulu.

Kuwapima watoto wa shule za S.t Kayumba na hao wenu wanaosoma shule za academia ni dhuluma ya wazi na matabaka haya mnayoyatengeneza majibu yake mtakuja kuyaona huko mbeleni.

Kisa cha binti wa kijakazi hakina tofauti na uamuzi wa Prof. Ndalichako wa kupandisha viwango vya ufaulu wa mitihani bila ya kuwa na maandalizi yeyote aliyoyafanya kuwasaidia watoto wa kimaskini.

Ndalichako wewe ni mtafiti mzuri tu, alichokifanya Prof. Mchome aliona kuwa elimu imeshuka kwa sababu ina upungufu mkubwa. Hivyo basi, ili watoto wa maskini wa Tanzania wasionewe na mfumo, aliamua kushusha viwango vya ufaulu ila siyo kwa kutangaza wazi ili watoto wa maskini hao wasionewe na mfumo.

Wazazi wa watoto maskini mnaosemesha watoto wenu shule za umma na ambao mlifurahia kuisikia kauli ya Ndalichako kurudisha madaraja, mfahamu wazi mlifurahia tanzia za elimu za watoto wenu na kuhalalisha kusonga mbele kwa watoto wao wanopata elimu bora ili kesho waje kuwa viongozi na kuwashinda watoto wenu kwenye soko la ajira.
Kuwapima sawa watoto wa shule za umma na wa shule binafsi ni kutaka kuwaita watoto wetu majina mabaya kuwa hawana akili, vilaza, wazembe, hawapendi elimu, hawana future na kashfa kibao, huku mnajua walimu wao hamuwalipi vizuri, wanawadai madeni yasiyolipika, walimu wao hawaandaliwi vizuri.

Wakati huohuo hamjawaletea zana za kujifunzia, mazingira yao kujifunzia hayaridhishi pia mmewatupia na jinamizi la lugha ya kufundishishia (Kiingereza) tusitegemee watafanya vizuri hawa.

Rai yangu kwa waziri husika boresha elimu kwanza kabla ya kupandisha viwango vya ufaulu. Namshauri pia afikirie upya upimaji wa wanafunzi ili kuleta usawa kutokana na elimu inayotolewa ili tupunguze mwanya uliopo sasa.

Inabidi mtafute suluhu juu ya lugha ya kufundishia na mfumo wa sasa ufumuliwe ili tujikite zaidi kwenye kutoa maarifa na siyo kuwakaririsha.

Hawa watoto robo tatu waliopata daraja la nne na sifuri tuwaweke katika uangalizi maalum, watafutiwe namna ya wao pia kuvuka hiki kizingiti. Ni wazi uwezo wao ni mzuri ila mazingira hayakuwaruhusu wapenye kwenye chujio lenu.

Pia mmemtaja shujaa wa shuleni zenu tunawaomba nasi mtutajie shujaa wa shule zetu za umma hata huyo wa kwenu akiitwa Ikulu na wa kwetu pia aitwe Ikulu kapambana kwa juhudi zake kuliko huyo wa kwenu aliyesoma kama mfalme.

Mwisho wabunge mfikirie kuweka sheria kwa viongozi wa serikali, wabunge na watumishi wa umma kusomesha watoto katika shule za umma labda ndiyo wataboresha elimu yetu, bila hivyo kilio hiki hakitaisha.

Taifa lenye madaraja tofauti ya elimu ni bomu linalongoja kulipuka.

Ndimi

Kwenye taarifa ya habari asubuhi wameonyesha mgogoro wa wanakijiji na serikari huko Rungwe mkoani mbeya. Kisa cha ugomvi wanamgombania mwalimu mkuu kwa jina bwana Msigwa; wanakijiji wanataka mwalimu mkuu abaki wakati serikari inataka kumuamisha.

Huyo mwalimu mkuu kaikuta shule ina wanafunzi saba na madarasa mawili, kwa ubunifu wake akiwashirikisha wanakijiji kaifanya shule iwe na moja ya madhari bora ndani ya Tanzania kwa yale mazingira niliyoyaona na watoto wote wanalala bweni ili wasome bila ya kuingiliwa au kupewa majukumu wakiwa nyumbani yatakayo watoa nje ya masomo na matokeo ya ufaulu yameanza kuwa mazuri.

Sasa basi imemchukua karibu miaka saba kufanikisha hayo malengo, badala ya wataalamu wa wizara kwenda kujifunza mbinu zake watungie sera it is as if he has done nothing special wala awajali jitihada za wanakijiji na imani waliyojijengea kwa yule mwalimu mkuu. Jamaa wamesema watachoma moto shule bwana Msigwa akiondolewa na awataki kusikia kabisa utani wame invest vya kutosha ndani ya hiyo shule kwa sababu ya kumuamini mwalimu mkuu leo tena mnataka mumtoe aende wapi; hii ndio Tanzania watu wapo wizarani na titles za wataalamu watoto zao wanaenda private huku chini awajuhi nini kinaendelea na wala awana shinda ya kujifunza ubunifu wa mtu kama Msigwa na changamoto za elimu ya Tanzania.
 
Mkuu umeandika ukweli mtupu na umeelezea vizuri. Nakubaliana na wewe kwa asimilia 99.

Wapinga chochote watakuja soon bila hoja.
 
vipaji vingi vimeishia kusikojulikana bila kufikia malengo,hiyo bado ni hazina tusiisau kabisa inaweza kutumika.
 
Hii mada nzuri sana,watunga sera waisome,tupate elimu bora,upate ujuzi na maarifa endelevu na yenye kufikia malengo.
 
Wanafunzi wanaopata daraja la kwanza na pili hupewa kipaumbele zaidi kusonga mbele,huku vipaji vingine vikipotelea mbali bila kufikiriwa kuibuliwa tena vitumike.
 
Watakaopinga hoja kama hizi lzma wana migogoro kichwani mwao. Hongera mtoa mada. Natamani Ndalichako angeiona binafsi. Aione Mawazo mbadala.
 
Wataniita mchochezi na huo ndio ukweli inatupaswa tupaze sauti maana watoto wetu watatuadhibu baadae kwa kushiriki kuwaangamiza
 
KABURI LA ELIMU KWA WATOTO MASKINI

KUPANDISHA viwango vya ufaulu bila uboreshaji wa elimu ni kuwazika watoto wa kimaskini ili waagane na elimu ili kesho waje kuwa wapambe na watumwa wa watoto wa viongozi wa sasa na wale wa matajiri.

Kabla hamjasimamia mipango yenu, hebu nanyi waleteni watoto wenu wasome na watoto wetu shule za umma (shule za kata).

Acha niwape kisa cha binti wa kijakazi aliyekuwa akiwania umalkia katika Taifa la Azania.

Katika Taifa la Azania alitokea mfalme ambaye maisha yake yote hadi anafika uzee hakubahatika kupata mtoto. Mfalme alitaka akiondoka duniani awe amempata mrithi wake ili aiche nchi salama.

Mfalme aliona awamu inayokuja iongozwe na mwanamke aweze kuwa malkia wa Azania. Mfalme alimwagiza msaidizi wake asimamie mchujo kisha mchujo nao ulimalizika kwa kuwapata mabinti wawili mmoja binti wa kiongozi na mfanyabiashara maarufu na wa pili akawa wa kijakazi, kwa hiyo lazima apatikane mmoja aweze kuwa malkia.

Mfalme akapanga siku ya zoezi la kumpata Malkia wa Azania na siku ilipowadia, mfalme aliwapatia zoezi dogo la kusaga mahindi apate unga wa ugali. Mfalme aliwaletea kiroba cha mahindi kila mmoja, akawatuma wakasage mahindi hayo wamletee unga kabla jua halijazama.

Binti wa kiongozi na mfanyabiashara maarufu alikwenda kwa wazazi wake na kuomba fedha za kusaga mahindi hayo kwa mashine na kufanikiwa kusaga na kuwahi kurudi kwa mfalme.

Mtoto wa kijakazi naye alimfuata mama yake kuomba ampatie fedha za kusaga mahindi hayo, mama yake alimpatia jiwe. Binti wa kijakazi alisaga mahindi hayo kwa taabu na nguvu kubwa kwa kutumia jiwe akapata unga na kuupeleka kwa mfalme.

Baada ya kufika kwa mfalme, aliwapokea na kuwapa chekecheo la kuchekecha unga huo kila mmoja akaanza kuchekecha. Binti wa kiongozi na mfanyabiashara maarufu alipata unga mwingi na chenga chache, yule wa kijakazi alipata chenga nyingi na unga mchache.

Ukweli ni kuwa binti wa kwanza alipata unga mwingi sababu alisaga kwa mashine na binti kijakazi alipata unga mchache kwa kuwa alitumia jiwe. Matokeo ya jumla mfalme alimtangaza binti wa kiongozi na mfanyabiashara kuwa Malkia wa Azania na binti wa kijakazi kwa juhudi kubwa aliambulia patupu.

Kisa hiki cha binti wa kijakazi nakifananisha na elimu ya Tanzania na matokeo haya ya kidato cha nne yanayoonesha watoto wetu wamefeli kwa takriban asilimia 70. Tujiulize tunawapeleka wapi hawa? .

Ushindani wowote ule unahitaji maandalizi ili uweze kushinda na ukiona baba au kocha wako anakupeleka kwenye mashindano makubwa yasiyoendana na maandalizi mazuri, ujue amepanga kukudhalilisha kama siyo kukudhalilisha ni kukuua kabisa.

Tujiulize kushindwa kwa binti kijakazi ni uzembe wake? Ujinga wa mama yake? au umaskini wao? Ila kwangu mimi kushindwa kwa binti wa kijakazi ni ujinga wa mfalme kutofikiria njia gani atumie ili zoezi litendeke kwa usawa.
Tuachane na hayo ya binti wa kijakazi na umalkia wa Azania, turudi hapa kwetu tuitazame elimu yetu ilipo na inapoelekea.

Serikali ya Awamu ya Tano imekuja na Waziri mpya Prof. Joyce Ndalichako.
Kama kawaida yetu, Watanzania tunawapima watendaji kwa majina na siyo mafanikio ya utendaji wao. Alipoingia tu akaanza kugombania suala la "Division" na "GPA" badala ya kuja na mpango mkakati wa kupandisha kiwango cha elimu kiweze kupanda juu na akashinda vita hiyo ya kurudisha "division" na kutupilia mbali "GPA" kwa kutumia mamlaka aliyonayo badala ya uhalisia.

Elimu ya nchi yetu imeshuka sana tena kwa kiwango cha juu, kuipandisha inahitaji muda.

Elimu bora inakuwepo pindi mambo yafuatayo yanapotekelezwa;

Mosi, Kuandaliwa Sera nzuri ya elimu inayotekelezeka.

Pili, Uandaaji mzuri wa walimu

Tatu, Kuwepo kwa zana za kujifunzia na ufundishaji kama vile vitabu vya kiada na ziada.

Nne, Mandhari nzuri ya kusomea na ufundishaji.

Hoja yangu ni juu ya upandishaji viwango vya ufaulu. Tumesikia Waziri wa Elimu Prof. Ndalichako ameturudisha katika mfumo wa madaraja, tafsiri nyepesi ni kuwa amepandisha viwango vya ufaulu.

Mtanishangaa sana kupinga kuwapima watoto wetu katika viwango vya juu, sababu ninazo na nitasimamia hata niwekewe kisu.
Viwango vya upimaji hupandishwa endapo elimu itazidi kuboreka. Dunia nzima inajua kuwa elimu yetu ipo chini. Wakati ni sasa tumwambie Mama Ndalichako aboreshe kwanza elimu iwe bora ndiyo apandishe viwango vya ufaulu.

Kuwapima watoto wa shule za S.t Kayumba na hao wenu wanaosoma shule za academia ni dhuluma ya wazi na matabaka haya mnayoyatengeneza majibu yake mtakuja kuyaona huko mbeleni.

Kisa cha binti wa kijakazi hakina tofauti na uamuzi wa Prof. Ndalichako wa kupandisha viwango vya ufaulu wa mitihani bila ya kuwa na maandalizi yeyote aliyoyafanya kuwasaidia watoto wa kimaskini.

Ndalichako wewe ni mtafiti mzuri tu, alichokifanya Prof. Mchome aliona kuwa elimu imeshuka kwa sababu ina upungufu mkubwa. Hivyo basi, ili watoto wa maskini wa Tanzania wasionewe na mfumo, aliamua kushusha viwango vya ufaulu ila siyo kwa kutangaza wazi ili watoto wa maskini hao wasionewe na mfumo.

Wazazi wa watoto maskini mnaosemesha watoto wenu shule za umma na ambao mlifurahia kuisikia kauli ya Ndalichako kurudisha madaraja, mfahamu wazi mlifurahia tanzia za elimu za watoto wenu na kuhalalisha kusonga mbele kwa watoto wao wanopata elimu bora ili kesho waje kuwa viongozi na kuwashinda watoto wenu kwenye soko la ajira.
Kuwapima sawa watoto wa shule za umma na wa shule binafsi ni kutaka kuwaita watoto wetu majina mabaya kuwa hawana akili, vilaza, wazembe, hawapendi elimu, hawana future na kashfa kibao, huku mnajua walimu wao hamuwalipi vizuri, wanawadai madeni yasiyolipika, walimu wao hawaandaliwi vizuri.

Wakati huohuo hamjawaletea zana za kujifunzia, mazingira yao kujifunzia hayaridhishi pia mmewatupia na jinamizi la lugha ya kufundishishia (Kiingereza) tusitegemee watafanya vizuri hawa.

Rai yangu kwa waziri husika boresha elimu kwanza kabla ya kupandisha viwango vya ufaulu. Namshauri pia afikirie upya upimaji wa wanafunzi ili kuleta usawa kutokana na elimu inayotolewa ili tupunguze mwanya uliopo sasa.

Inabidi mtafute suluhu juu ya lugha ya kufundishia na mfumo wa sasa ufumuliwe ili tujikite zaidi kwenye kutoa maarifa na siyo kuwakaririsha.

Hawa watoto robo tatu waliopata daraja la nne na sifuri tuwaweke katika uangalizi maalum, watafutiwe namna ya wao pia kuvuka hiki kizingiti. Ni wazi uwezo wao ni mzuri ila mazingira hayakuwaruhusu wapenye kwenye chujio lenu.

Pia mmemtaja shujaa wa shuleni zenu tunawaomba nasi mtutajie shujaa wa shule zetu za umma hata huyo wa kwenu akiitwa Ikulu na wa kwetu pia aitwe Ikulu kapambana kwa juhudi zake kuliko huyo wa kwenu aliyesoma kama mfalme.

Mwisho wabunge mfikirie kuweka sheria kwa viongozi wa serikali, wabunge na watumishi wa umma kusomesha watoto katika shule za umma labda ndiyo wataboresha elimu yetu, bila hivyo kilio hiki hakitaisha.

Taifa lenye madaraja tofauti ya elimu ni bomu linalongoja kulipuka.

Ndimi

Hansen Nasli
Ulicho sema ni kweli tupu.
 
Hii mada nzuri sana,watunga sera waisome,tupate elimu bora,upate ujuzi na maarifa endelevu na yenye kufikia malengo.
 
Wanafunzi wanaopata daraja la kwanza na pili hupewa kipaumbele zaidi kusonga mbele,huku vipaji vingine vikipotelea mbali bila kufikiriwa kuibuliwa tena vitumike.
Hivi serikali na sekta binafsi nani ana pesa? Tatizo ni kujidai kila MTU anaweza elimu ya sekondari wakati kiuhalisia siyo kweli. Wanafeli form 2 wanalazimisha waendelee matokeo ndio hayo. Viva private Schools keep on beating Government Schools.
 
Wanafunzi wanaopata daraja la kwanza na pili hupewa kipaumbele zaidi kusonga mbele,huku vipaji vingine vikipotelea mbali bila kufikiriwa kuibuliwa tena vitumike.
 
Hii mada nzuri sana,watunga sera waisome,tupate elimu bora,upate ujuzi na maarifa endelevu na yenye kufikia malengo.

Nina hisia kwamba hii mada tuliosoma mpaka paragraph ya mwisho hatuwezi kufika 20 na hii ndio mojawapo ya athari ya elimu Tanzania.
 
Ndg. Nasli umetoa mada kwa uzuri na umetoa upembuzi mzuri sana. Elimu yetu watanzania imetetereka muda mrefu sana umepita, si ya msingi, sekondari wala chuo kikuu zote zinahitaji kufanyiwa maboresho makubwa. Elimu imejikita kwenye vyeti tuu, ubunifu umeachwa mbali badala yake hata mtu ukajitutumua utapata first class chuo kikuu ila ya vitini na kukariri.
Elimu ya msingi ndio kabisaaa, mtoto anatoka darasa la saba kusoma kwa ngazi ya darasa la 3 hawezi. Sekondari nayo hoi. Yote haya anayeathirika ni mwananchi wa kipato cha chini na hawa ndio wengi.
Nafikiri serikali ilione hili na itizame ilipoteleza na ifanye masahihisho.
Elimu bora ndio itakayopeleka mbele malengo ya kuelekea uchumi wa kati tunaoutazamia. Tusipofanya hivyo, watu wengi tutaishia kuwa manamba na matarishi kwenye viwanda vya wazungu tukiongozwa na wenzetu waloenda kupata elimu bora kwingineko duniani.
Kwa mfumo huu uliopo hata wanaoenda kwenye michepuko ya ufundi hawajaandaliwa vizuri, utakuta mtu kamaliza diploma ya ufundi fulani lakini hana ubunifu wowote hata alichokisoma hajaelewa ila amefaulu.
Serikali na wadau sasa wakati umefika tufikiri namna ya kuiokoa elimu yetu. Kama kikwazo ni lugha ya kufundishia ya kiingereza ndio inatufanya tusielewe kwa uzuri tuitoe tuweke tunayoielewa zaidi maana heri kuelewa kwa lugha ya kingoni kuliko kukomaa na kizungu ambacho huelewi.
 
Elimu haitakuwa bora kwa hizi shule za kata zilizo nyingi kama utitiri. Wilaya moja kama Chalinze ilitosha kuwa na shule za Form 1-4 shule 4 na Advance shule 3 zingetosha wilaya nzima na zikawa na kila kitu mazingira bora na vifaa bora vya kufundishia, huu utitiri wa kukuta wailaya moja ina shule sijuia 40 za Secondary ni kudanganyana, hakunaelimu pale.
Cheki shule za zamani, Chukuli mfano wa iliyo kuwa Mkwawa, ilikuwa ni shule yenye majengo na madhali ya watoto kusoma, au ile shule ambapo sasa ni Chuo kikuu cha St Joseph pale Dodoma. Shule kama zile tatu zilikuwa zinatosha wilaya nzima labda kwa wilaya kubwa za mijini kama Dar na kwingineko ndo shule zingeongezwa.

Hina maana kuwa na utitiri wa shule za kata, Kila wilaya hasa za huko mikoani zingehengwa shule 4 zingetosha kabisa, na ziwe ni shule kweli
 
Umeenda deep sana hasa kwa mfano wako.
Sihitaji kupunguza wala kuongeza neno.Wenye kuelewa na kuwa tayari kushaurika nitafurahi wakianza kuchukua hatua mapema.Tuache siasa wala kutafuta kumridhisha mtu/kundi fulani.Tufanye mambo kwa mustakabali na ustawi wa jamii yetu
 
Ndg. Nasli umetoa mada kwa uzuri na umetoa upembuzi mzuri sana. Elimu yetu watanzania imetetereka muda mrefu sana umepita, si ya msingi, sekondari wala chuo kikuu zote zinahitaji kufanyiwa maboresho makubwa. Elimu imejikita kwenye vyeti tuu, ubunifu umeachwa mbali badala yake hata mtu ukajitutumua utapata first class chuo kikuu ila ya vitini na kukariri.
Elimu ya msingi ndio kabisaaa, mtoto anatoka darasa la saba kusoma kwa ngazi ya darasa la 3 hawezi. Sekondari nayo hoi. Yote haya anayeathirika ni mwananchi wa kipato cha chini na hawa ndio wengi.
Nafikiri serikali ilione hili na itizame ilipoteleza na ifanye masahihisho.
Elimu bora ndio itakayopeleka mbele malengo ya kuelekea uchumi wa kati tunaoutazamia. Tusipofanya hivyo, watu wengi tutaishia kuwa manamba na matarishi kwenye viwanda vya wazungu tukiongozwa na wenzetu waloenda kupata elimu bora kwingineko duniani.
Kwa mfumo huu uliopo hata wanaoenda kwenye michepuko ya ufundi hawajaandaliwa vizuri, utakuta mtu kamaliza diploma ya ufundi fulani lakini hana ubunifu wowote hata alichokisoma hajaelewa ila amefaulu.
Serikali na wadau sasa wakati umefika tufikiri namna ya kuiokoa elimu yetu. Kama kikwazo ni lugha ya kufundishia ya kiingereza ndio inatufanya tusielewe kwa uzuri tuitoe tuweke tunayoielewa zaidi maana heri kuelewa kwa lugha ya kingoni kuliko kukomaa na kizungu ambacho huelewi.

Kwa nini sasa lugha iwe tatizo na huko nyuma haikuwa tatizo? Ishu ni Serikali kuingiza siasa kwenye Elimu, Ujenzi wa shule za kata ni siasa tupu, shule hazina ubora ni full usanii na shule ziko pale kuzalisha wajinga,
Tulipo anza kujenga utitri wa shule na tulipo anza clashing program ndo hapo elimu ilizikwa lasimi.
 
elimu bora itamfikiaje mlingwa wakati main vessel (teacbers) imetoboka toboka?
elimu bora itamfikiaje mlingwa wakati main bridge(teachers) lipo vipande vipande?

walimu
maslahi
walimu
mazingira bora ya kazi
kiwe kipaumbele hayo mengine utaona yakitokea automatic.....
 
Back
Top Bottom