Hili ndio eneo pekee mkuu wa mkoa hawezi kulifikia eneo lake la kazi bila kukatisha mkoa mwingine

Jelavic

Senior Member
Dec 28, 2016
180
380
Salaam..!
Habari zenu.wana bodi...

Wananchi wengi wa Tanzania wamelazishwa na vyombo vya habari kuijua Kibiti hasa kwa sifa ya mauaji yanayoendelea. Bi nafsi nalaani sana tuko hilo hasa kumwaga damu ya mtu bila hatia ,tena ni mzazi pengine nitegemeo kwa familia yake lakini pia nikiongozi ambaye kwa namna moja Ama nyingine au kwa sababu hii au ile nitegemeo la taifa hili la WANYONYWAJI.

Ninachotaka niseme kuhusu Kibiti hiki! Kibiti ni wilaya nyonge kihistoria.
Waliosoma Kibiti hasa miaka ya hivi karibuni watanisadikishia hili.
Ndugu wanabodi kabla Kibiti haijawa wilaya ilikuwa ndani ya wilaya ya Rufiji.

Mheshimiwa sana alipoingia madarakani ilikuwa tayari rufiji na Kibiti vimegawanywa na mtangulizi wake kuwa wilaya tofauti lakini pamoja na hivyo katika KUPANGA NI KUCHAGUA NA PANGA PANGUA hakuweza kuipa Kibiti mkuu wa wilaya.

Unapoinyima Kibiti muwakilishi wako kwenye eneo lile maana yake unachelewesha maendeleo.

Ndugu wanabodi,
Mkuu wa mkoa wa Pwani hawezi kutoka sehemu ya eneo lake kwenda lingine mpaka apite mkoa wa Dar e Salaam.

Namaanisha huwezi toka Kibaha kwenda Kibiti isipokuwa lazima avuke mkoa wa Dar es Salaam.

Tafsiri yake nini,
Muwakilishi wa Rais anapokuwa mbali na jamii ndio maendeleo yanavochelewa. Nasikitika msemo usemao pwani wavivu hawasomi bila Serikali kutumia jitihada kuleta mabdiliko katika hili wakati wanajua kuwa wao ni miongoni mwa sababu.

Ndugu wanabodi naomba kuwasilisha.
 
So what as long ni Ndani ya Tanzania na kazi zao ni kumuwakilisha raisi
 
Kukosekana kwa mkuu wa wilaya ambaye kimsingi ni mwenyekiti wa ulinzi na usalama wa wilaya inaweza ikawa ndio sababu ya kuzorota kwa amani?Ila tuangalie upande wa pili, hawa wakuu wa wilaya wapo busy katika kurudisha nyuma na kuzoofisha upinzani.Kibiti ni janga na wa kulaumiwa ni serikali ya CCM.
 
Kabla ya mwaka 1972 Dar es salaam ilikuwa ni sehemu na makao makuu ya mkoa wa Pwani. Hivyo Dar ilikuwa ni kiungo cha kuunganiaha wilaya zote za mkoa wa Pwani (Bagamoyo-kisarawe-Rufiji na Mafia). Wilaya ya Kibaha iliundwa kwa kumegwa kwa Wilaya za Kisarawe na Bagamoyo na kufanywa makao makuu mapya ya mkoa wa Pwani. Baadae Mkuranga nao ikamegwa toka Kisarawe na Kibiti toka Rufiji.
Kutokana na asili hiyo ya Kijiografia kwa sasa Pwani bado tegemezi kwa Dar kama kiungo.

Kunahitajika jitihada za makusudi kujenga barabara itakayounganisha wilaya zote za mkoa wa Pwani na makao makuu ya mkoa. (Bagamoyo➡ Kibaha ➡ Kisarawe ➡ Mkuranga ➡ Rufiji ➡Kibiti)
 
Naunga Mkono hoja Kwa watu kama sisi ambao miaka Ya nyuma ktk mishemishe zetu za kutafuta maisha pwani Yote ilikuwa tulivu tu
Usiku unatembea mida wowote lkn Kwa sasa baada Ya kutokea mauaji huko pwani basi kumekuwa shidaaa

OvA
 
Nasikitika msemo usemao pwani wavivu hawasomi bila serikali kutumia jitihada kuleta mabdiliko katika hili wakati wanajua kuwa wao nimiongoni mwa sababu.
Nakubaliana nawe kwa yote uliyo yaeleza ktk Uzi wako lkn kwenye hili LA uvivu na kutokusoma....nasema hapana. Mila na desturi za watu wa Pwani ndiyo kikwazo. Shughuli zao kubwa uvuvi, hivyo waliamini hakuna shida as long as bahari haikauki. Vigodoro , baikoko, mdumange na ndoa za utotoni vimewaingia kwenye damu. Ndiyo maana hali ya mkoa wa Pwani ni sasa kabisa na ile ya Lindi na Mtwara.

Luna mikoa huko bars INA jiograpia mbaya kuliko mkoa wa Pwani lkn huwezi kukutana na upuuzi unaoendelea mkoa wa Pwani.
 
Huko kibiti inatakiwa wachungaji na viongozi wa dini wapelekwe kwa wingi ili wakaeneze neno la Mungu tetetetetetete, badala ya kupeleka polisi kwa wingi, huko wanahitaji maombi zaidi
 
Tuwekee na ramani tuone.

Na kwani shida haswa ni nini kwako?

Na unataka iweje? Yaani nini unataka kuona kinafanyika?
 
Kukosekana kwa mkuu wa wilaya ambaye kimsingi ni mwenyekiti wa ulinzi na usalama wa wilaya inaweza ikawa ndio sababu ya kuzorota kwa amani?Ila tuangalie upande wa pili, hawa wakuu wa wilaya wapo busy katika kurudisha nyuma na kuzoofisha upinzani.Kibiti ni janga na wa kulaumiwa ni serikali ya CCM.
Tena vyeo vya RC na DC vifutwe
 
Sawa mkuu nmekuelewa ngoja nikupigie debe uwe mkuu wa wilaya ya kibiti ili ulete maendeleo
 
Tuwekee na ramani tuone.

Na kwani shida haswa ni nini kwako?

Na unataka iweje? Yaani nini unataka kuona kinafanyika?
Ccm ishakuathiri ww
Ramani ya nn anachosema ni kweli kwenda rufij kutok kibah lazm upite dar
Anachotaka kiwepo barabara inayounganisha mkoa pwani moja kwa moja bila kukatisha dar na mkuu wa wilaya ya kibiti ateuliwe kwa tuliko kaa kibiti tunaelewa
 
Kabla ya mwaka 1972 Dar es salaam ilikuwa ni sehemu na makao makuu ya mkoa wa Pwani. Hivyo Dar ilikuwa ni kiungo cha kuunganiaha wilaya zote za mkoa wa Pwani (Bagamoyo-kisarawe-Rufiji na Mafia). Wilaya ya Kibaha iliundwa kwa kumegwa kwa Wilaya za Kisarawe na Bagamoyo na kufanywa makao makuu mapya ya mkoa wa Pwani. Baadae Mkuranga nao ikamegwa toka Kisarawe na Kibiti toka Rufiji.
Kutokana na asili hiyo ya Kijiografia kwa sasa Pwani bado tegemezi kwa Dar kama kiungo.

Kunahitajika jitihada za makusudi kujenga barabara itakayounganisha wilaya zote za mkoa wa Pwani na makao makuu ya mkoa. (Bagamoyo Kibaha Kisarawe Mkuranga Rufiji Kibiti)
well said wewe unaifahamu pwani.
 
Back
Top Bottom