Hili nalo ni miongoni mwa mitihani inayomkabili mwanamke….! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hili nalo ni miongoni mwa mitihani inayomkabili mwanamke….!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Feb 15, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Feb 15, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Inaelezwa kwamba kuna uhusiano kati ya wanawake waliofanikiwa kwenye ajira kwa kuwa na kipato kikubwa zaidi ya waume zao na talaka. Labda nisema tu kwamba, binafsi sikubaliani na jambo hilo. Sikubaliana na dhana hiyo kwa sababu kuna idadi kubwa tu tena ya kutosha ya wanawake waliofanikiwa kwenye ajira zao kwa kuwa na kipato kikubwa zaidi ya waume zao lakini ndoa zao zimeendelea kuwa na Amani, imara na furaha tele.

  Kama zipo ndoa ambazo zimetikiswa kwa sababu ya mke kumzidi mume kwa kipato, nafikiri sababu haitakuwa ni mume kuzidiwa kwa kipato, bali kuna jambo lingine ambalo wengi tunashindwa kuling'amua , inawezekana kwa makusudi au kwa kutojua. Kuna swala la kutojiamini ambalo ni tatizo linalowakabili wanandoa wengi. Kama ikitokea mume au mke ana tatizo la kutojiamini katika ndoa, basi ni vigumu kwa ndoa hiyo kuwa na amani.

  Hebu chukulia kwamba, mwanamke ndiye anayefanya kazi na mwanaume hana shughuli ya kumuingizia kipato. Mwanamke huyu anaporejea jioni kutoka kazini anakuta nyumba ni kama jalala. Vitu vimetupwa huku na kule, mwanaume pengine kalala kwenye makochi, huku TV inakoroma. Lakini, kando kuna chupa mbili tatu za pombe. Hebu niambie, hapo mwanamke afanye kitu gani? Ni lazima atazungumzia kukerwa na hali ile. Kwa kutojiamini kwake, mwanaume ataanza kusema, mwanamke anamnyanyasa kwa sababu ya kazi yake au cheo chake.

  Hivi hapo kuna uhusiano gani kati ya ajira au cheo na kauli au madai hayo ya mwanaume kwamba, anaonewa. Hapa kuna mtu kushindwa kukua. Mwanaume hapa anashindwa kukua na kuwajibika kwa maisha yake. Kama mwanaume hana shughuli na bado anashindwa hata kupanga vitu nyumbani na bado anaamini kwamba kunywa pombe ndiyo suluhu kwa matatizo yake ya kukosa ajira, inahusiana vipi na mke kumnyanyasa mume?

  Kama mume hana shughuli ya kumuingizia kipato au anayo lakini ina kipato kidogo ukilinganisha na kipato cha mwanamke, lakini mume huyo anajitahidi kupata shughuli itakayolipa zaidi, ni vigumu mwanamke kumzonga. Kama ikitokea mwanamke kumzonga, hapo ndipo naweza kusema, mwanamke ana matatizo. Kwa hiyo tatizo hapa ni kukua, yaani mwanamke au mwanaume anaposhindwa kukua, ndipo matatizo kama hayo ya kuoneshana ubabe na ujuaji kati yao yanapojitokeza. Kwa hiyo siyo suala la mwanamke kuwa nacho zaidi ya mwanaume.

  Lakini pia labda niseme tu kwamba, kuna suala la malezi, kwa nini kuna baadhi ya wanawake wanapopata fedha wanaamini kwamba hawana sababu ya kuwajali waume zao? Hapa kuna suala la malezi. Je mwanamke huyo aliaminishwa nini juu ya fedha? Kwa hiyo siyo kila mwanamke aliyesoma sana au ambaye ana kipato kuliko mume, anakuwa mkorofi, hapana. Kuna wakati ni kweli na kuna wakati siyo kweli. Na mara nyingi wanawake wenye tabia hizo ni wachache sana na ni wale walioathiriwa na malezi.
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  Feb 15, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  umenena vyema, sina la kuongeza................
   
 3. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #3
  Feb 15, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kabisa, kwani nimeuliza maswali na kuyajibu mwenyewe......................Kama umefurahi basi gonga LIKE inatosha tu..............LOL
   
 4. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #4
  Feb 15, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hata mimi sina la kuongeza hapo!
   
 5. F

  Fmewa JF-Expert Member

  #5
  Feb 15, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 294
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Asante mkuu. pamoja na kuwa sijafanya utafiti kuhusu hilo lakini idadi ya wanawake wanaonyanyasa wanaume baada ya vipato vyao kuongezeka idadi hiyo ni kubwa kuliko wale ambao huwa wanaendelea kuwaheshimu waume zao. Kwa sababu sija evidence naomba niishie hapa kwa sasa. thanks
   
 6. chriss brown

  chriss brown JF-Expert Member

  #6
  Feb 15, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 292
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wapo wanawake wanapesa sana,lakini heshima kwa mume wake au mpenz wake ipo palepale,hii inategemea na mazingira aliyolelewa,na jinsi anavyoona hasa hasa mama yake anavyo mtreat baba yake mzazi. Either anapesa zaidi au kidogo..
   
 7. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #7
  Feb 15, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Ni kweli kabisa babu yangu unayoyasema, kitendo cha kutojiamini ni tatizo kubwa kwa wanandoa waliotofautiana vipato nimeshashudia sana aina ya ndoa hizi.
   
 8. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #8
  Feb 15, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,325
  Likes Received: 2,319
  Trophy Points: 280
  Niangalie kwa upande mmoja -kisasi- namzungumzia mwanaume ambaye alikuwa anamnyanyasa mke wake, inaweza kuwa kwa maneno,kulala nje n.k.ghafla kipato kinashuka au kuisha kabisa halafu mwanamke anakuwa juu kiuwezo,Wachache ndio husahau yaliopita lakini wengi wao inakuwa balaa la kisasi...utapigwa mpaka singe!!! utakuwa mdogo kama piriton.
   
 9. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #9
  Feb 15, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Unajua wanawake wana huruma sana! sitashangaa kuona au kusikia wapo wanawake walionyanyaswa na waume zao wakati wakiwa kwenye kilele cha mafanikio na pale mambo yanapogeuka na mke kuwa na kipato na mume kugeuka kula kulala, mke huyo akaendelea kumheshimu mumewe na kumjali kama vile hakuna kilichotokea.......................Wanawake bana (Some of them) wana mioyo ya huruma sana.
   
 10. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #10
  Feb 15, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,325
  Likes Received: 2,319
  Trophy Points: 280
  Ni kweli wana huruma - wapo,ila kuna wasiosamehe na utawaona kwenye vitendo..pita kwenye hiyo nyumba kama mgeni utaduwaa..mara utamsikia "jamani nyie watoto msije kuniharibia TV yangu nilinunua kwa kujinyima". Au "Juma kamwambie baba yako akupe chenji yangu, tokea nimpe hela wiki jana hajarudisha au anafikiri nitasahau'.
  Na hii " Benny kesho nikitoka kazini ndio nitawalipia ada yenu ya shule baba yenu kama hivyo mnavyomuona"
   
 11. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #11
  Feb 15, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Wanawake wa kichaga na kipare ndio wenye tabia hizo. Loh!
   
 12. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #12
  Feb 15, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Tabia zipi, maana nimezungumzia tabia mbili tofauti....................
   
 13. Mpatanishi

  Mpatanishi JF-Expert Member

  #13
  Feb 16, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kuanzia leo nakuaita mchambuzi instead of mtambuzi.
   
 14. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #14
  Feb 16, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,108
  Likes Received: 6,583
  Trophy Points: 280
  "Lakini pia labda niseme tu kwamba, kuna suala la malezi, kwa nini kuna baadhi ya wanawake wanapopata fedha wanaamini kwamba hawana sababu ya kuwajali waume zao"?

  Wanaume wenyewe kila mahali wanalalamika kuwa nguvu za kiumeni zimekwisha,
  pesa ndo inayotusuuza roho zetu.
   
 15. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #15
  Feb 16, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,471
  Likes Received: 19,861
  Trophy Points: 280
  inabidi jamaa abadili jamii
   
Loading...