Elections 2010 Hili nalo litalipuka hivi karibun....maana linafukuta jikoni

komagi

Member
Nov 1, 2010
62
2
Kutokana na chanzo kilichonitonya habari hizi kuwa ni cha idara nyeti ya serikali naomba kutoa hoja kama ifuatavyo:

Katika kukurukakara za kujiandaa na uchaguzi huu wa mwaka 2010.. kuna habari kuwa kuanzia mwaka 2005 waziri mmoja wa awamu iliyopita ambaye ana mkono wake TICS alianza kulipwa TSHS 100 mil kila siku awe amefanya kazi ama la lakini hizo pesa aliagizwa na mkuu wake akusanye kwa ajili ya uchaguzi huu wa mwaka 2010. Hivyo zile pesa zikawa zinalipwa kwa huyu waziri kupitia benki kuu na kuwa deposited kwenye benki kuu ya uingereza.

Kosa walilolifanya ni kuwa kule uingereza zilikuwa zinakuwa deposited kama pesa kutoka tanzania si kwa mtu binafsi hivyo ilipofika mwaka huu walipoenda kutaka kudraw hizi pesa wakaambiwa kuwa hizi pesa ni za tanzania si za mtu binafsi hivyo wakaagiza gavana fedha mzee B. Ndulu akazisaini kuidhinisha kutoka kwa pesa hizo.

Kwakuwa ilikuwa ni mtego gavana akakataa kwenda akidai kuwa shughuli za uchaguzi zimeshika kasi hivyo hadi uchaguzi upite. Inadaiwa kuwa serkali ya uingereza ikauliza inakuwa watz wanaomba pesa ya uchaguzi wakati wana mabilion ya pesa zao hapa kwenye benki yetu?

Kisa kilichopelekea kumuita gavana akazisaini lakin hakutia mguu. inasadikika kuwa wakubwa wa kaya bado wanagonganisha vichwa ili kujua watasolve vipi hii kadhia.

Naomba kutoa hoja mwenye kuijua vizuri hii issue atuhabarishe
 
Millioni 100 kwa siku tangia mwaka 2005 hadi 2010! Hapana, haiwezi kuaminika; hapo hujanipata bado.
 
Millioni 100 kwa siku tangia mwaka 2005 hadi 2010! Hapana, haiwezi kuaminika; hapo hujanipata bado.

Kama riwaya fulani hivi za Karumekenge....Ila kwa Tz siwezi kushangaa, kwani Richmond wakuwa wanalipwa kiasi gani (hivi siyo $153,000.00 kwa siku??).

Tanzania ina wenyewe bwana...!
 
Haya Haya Njaa Haziishi Tanzania na Watanzania Hatujui Lini Matombo Yao na Tamaa Zao Zitaisha? Haiwezekani Makamba na Wote Wasimamizi wa Uchaguzi 2010 Walifanya Kumsaidia Kikwete Kuchaguliwa. Huyo Mkurugenzi wa Usalama wa Utaifa na Jeshi la Tanzania, Kama Watanzania Tungekamata Bank Statements Zao Tungeona Makubwa. Hao Wabunge na Ushindi wa CCM Sio Bure na Tutafuatilia Hizi Payments? Hawajali Nchi CCM Hiyo Tunajua.
 
Komagi habari ambayo haina source,haina attribution,haina logic na it doesn't make sense, ilistahili kuitwa tetesi sio news alert.
 
Du kaka asante mimi naiamini hiyo habari maana kuna rafiki yangu alinigusia muda hiyo habari lakini sikuikazia. Aisee ni kweli na imeleta mfarakano wa njia zilizokuwa zimetumika kuziweka hizo pesa kuwa hazikuwa sahihi na wangependa kama zingepitia kwenye makampuni. hivyo wakubwa walijigawa hapo.
 
Mimi yangu ni macho na masikio. Haya haya CHADEMA mzigo huooo kama ni kweli.
 
Millioni 100 kwa siku tangia mwaka 2005 hadi 2010! Hapana, haiwezi kuaminika; hapo hujanipata bado.

Ikiwa unaikataa hii, kwa nini unakubali kuwa tanesco ilikuwa ikiilipa richmond usd$153,000=TZS zaidi ya 200ml kwa siku???????
 
H

Komagi habari ambayo haina source,haina attribution,haina logic na it doesn't make sense, ilistahili kuitwa tetesi sio news alert.

hata richmond mlidai ni tetesi, then it came to reality. kwa ccm hakuna ja ajabu hapo> Jiulize serikali walikuwa wanawalipa sh ngapi kwa siku richmond, iptl, agreco, songas, netgroup solution? it could be over 600ml daily, sembuse hizi 100ml? ambazo walipanda kuzitumia wakati wa kampeni!
 
Millioni 100 kwa siku tangia mwaka 2005 hadi 2010! Hapana, haiwezi kuaminika; hapo hujanipata bado.

hata mimi najiuliza ivo. Ila kuna mh.mkono alikuwa analipwa ela kama iyo kusimamia kesi kwa upande wa serikali au mtoa mada anamaanisha ela ile? Maana na huo ni ufisadi ulitukuka kumlipa advocate ela kama ile.
 
wadau tuwe makini maana hata chenge alisema bil 1.2 ni vijisenti kwahiyo hata hizo ni kweli,

mimi naamini hata wakati ule wa epa kuna watu walibisha na wengine hadi leo wanaona ni uwongo wakati ni kweli.

Tufanye mabadiliko ya kweli na tuwe na chama kimoja cha upinzani ili kuhakikisha tunapata uongozi mzuri wa kuwaletea watanzania elimu bora, afya bora, kilimo bora na maisha bora kwa ujumla. Ila haya yote yanatakiwa kwa vitendo na si kwa maneno kama CCM inavyofanya.

Tukiunge mkono chadema hasa ukiwa kijana maana wazee wengi ndo kama hivyo wametufikisha hapa tulipo ukiacha wachache wanaopigana kufa na kupona hadi leo.

peoples power
 
wana JF kwa kuwa ishu hii inilinigusa na kunihuzunisha sana imenibidi niwe kachero kwa muda ili kupata kinachoendelea kwenye hili sakata. kwa habari nilizozipata ni kuwa benki ya uingereza imeblock kwa sasa hiyo akaunti na kwamba pesa haziingii wala kutolewa hadi hapo muafaka utakapopatikana.....sasa hapo nabaki kufanyia utafiti suala moja je kama zimesitishwa kuingizwa humo? je haya malipo yalikuwa sahihi? je bado yanaendelea? na je zinawekwa wapi sasa?
 
nilikuwa najiuliza huyu jamaa alichangia hela nyingi kwenye uchaguzi wa 2005 imekuwaje akakaa kimya mwaka huu kumbe alikuwa anpiga dili.
kweli jasri haachi asili.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom