Hili nalo linahitaji mkono wa Serikali?

MwanaHaki

R I P
Oct 17, 2006
2,401
704
Ndugu Zangu,

Hebu kaeni kwanza mfikirie, iwapo hili nalo linahitaji mkono wa Serikali.

Nazungumzia suala la makazi yasiyo rasmi, yaani, squatter areas. Ndani ya Dar yametapakaa kila kona, hata huko uzunguni - Masaki, Mikocheni, Mbezi Beach - yapo pia.

Je, sisi wenyewe hatuwezi kukaa na kuunda mkakati wa kuyaondoa na kuweka mbadala wake, bila kuhitaji mkono wa Serikali? Nia tunayo (?), uwezo tunao (!) na sababu pia tunazo (!!!) teleeee!

Sasa tunangoja nini? Au uwekezaji ni kwa WAZUNGU tu?

Mimi nina mpango kamambe, lakini nahitaji WATANZANIA wenzangu tukae tushirikiane, tufanye mambo YA KWELI!

Mwenye nia anitafute kwa PM, aandike ujumbe wenye maneno UWEKEZAJI MAKAZI, aache namba yake ya simu, nitampigia!

UWEZO TUNAO! Maisha bora hayaji kwa kukaa kijiweni!

-> Mwana wa Haki
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom