" Hili nalo jambo: 3/4 ya Wafanyakazi wa Serikali hawawajibiki"

We Know Next

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
814
380
Wanajamii, Baadhi ya magazeti ya leo tarehe 21/6/2011, yameripoti kuwa Waziri Mkuu, jana amesema kuwa 3/4 ya wafanyakazi wa Serikali hawawajibiki ipasavyo na ndiyo chanzo kikubwa cha ufanisi mdogo serikalini.

1. Ikiwa kama hizo statistics ni kweli, basi kuondoa umasikini wa watanzania ni ndoto za alinacha;
2. Hii inamaana kuwa, hakuna viongozi wa kuweza kuwawajibisha watu huko serikalini ndio maana watu wapowapo tu;
3. Waziri Mkuu anachukua hatua gani baada ya kuona hali hiyo?

My take:

1. Inawezekana wafanyakazi serikalini wamekuwa wengi sana, basi ni vyema wapunguzwe;
2. Napendekeza Ajira Serikalini ziwe za Contract kati ya miaka 3-5. Na mtu aweze kureview contract yake based in performance. Kwa utaratibu wa sasa, watu wanajisahau kwa vile wanajua hakuna kufukuzwa kazi hata kama ukiiba. Watu wengi wanasema Serikalini kuna security, hilo ndilo jambo linawafanya wengi kuwa wazembe na kutowajibika;
3. Serikali iingie mkataba na Private firms kusimamia zoezi zima la perfomance za wafanyakazi Serikalini, nina uhakika hapo ngoma itanoga.

Natoa hoja!
 
(job descriptions x performance) = output = (Salary/benefits)
Je yeye Mr. Pinda si naye yupo kwenye 3/4 au yupo kwenye remaining 1/4!??? ....na JK je yupo 'fraction' ipi!?
 
Wanajamii, Baadhi ya magazeti ya leo tarehe 21/6/2011, yameripoti kuwa Waziri Mkuu, jana amesema kuwa 3/4 ya wafanyakazi wa Serikali hawawajibiki ipasavyo na ndiyo chanzo kikubwa cha ufanisi mdogo serikalini.

1. Ikiwa kama hizo statistics ni kweli, basi kuondoa umasikini wa watanzania ni ndoto za alinacha;
2. Hii inamaana kuwa, hakuna viongozi wa kuweza kuwawajibisha watu huko serikalini ndio maana watu wapowapo tu;
3. Waziri Mkuu anachukua hatua gani baada ya kuona hali hiyo?

My take:

1. Inawezekana wafanyakazi serikalini wamekuwa wengi sana, basi ni vyema wapunguzwe;
2. Napendekeza Ajira Serikalini ziwe za Contract kati ya miaka 3-5. Na mtu aweze kureview contract yake based in performance. Kwa utaratibu wa sasa, watu wanajisahau kwa vile wanajua hakuna kufukuzwa kazi hata kama ukiiba. Watu wengi wanasema Serikalini kuna security, hilo ndilo jambo linawafanya wengi kuwa wazembe na kutowajibika;
3. Serikali iingie mkataba na Private firms kusimamia zoezi zima la perfomance za wafanyakazi Serikalini, nina uhakika hapo ngoma itanoga.
Natoa hoja!

Hakuna hata kujadili swala kama hilo kama 3/4 ya wafanyakazi wa serikali wanaochukua karibu trillioni 7.4 kati ya bajeti nzima ya trillioni 11.6 huku wakituachia trillioni nne tu kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wote millioni 42 basi neno moja tuu serikali hii imeshindwa kazi na inapaswa kunq'olewa full stop,na huyu aliyetangaza upupu huu ambaye anaongoza serikali za Kitanzania anastahili kufunguliwa mashitaka na kufungwa kwa kushindwa kusimamia serikali na kuingizia hasara nchi
 
yaani huyu jamaa sasa nae ameamua kujiunga na JK kuchafua hali ya hewa kabisa, ingewezekana JF tumpige bann mizengo pinda asijadilwe hapa tena.
 
Wafanyakazi wengi wa Serikali wanapoteza muda kupiga siasa humu jf na kuangalia michuzi blog kisha pipoz pawa kwa wingi at the same time wanainanga Serikali ilhali wao ni part and parcel kwa kufeli mipango ya Serikali.
 
Back
Top Bottom