Hili liwe funzo: Tudai Katiba bora zaidi (maboresho)

Joshua justine

JF-Expert Member
Sep 1, 2021
474
1,000
Habari zenu wadau wa jukwaa hili adhimu sana,

Sasa nadhani imefika wakati wananchi tuamke na kukataa huu uzombi unaotutesa; Taifa letu limekuwa halieleweki, mpaka sasa hakuna anaejua kesho tukiamka kiongozi aliyeko madarakani atakuja na jambo gani jingine, je atafuta lipi jingine lililoachwa na mtangulizi wake ama je ataanzisha lake lipi jipya?

Ni nchi isiyokuwa na dira, ni kama safari ya wendawazimu wasiojua wanaelelea wapi,. Kwa mwendo huu tunaweza kuzunguka hapo hap tulipo, tukatumia nguvu na resource nyingi lakini mwisho tukawa displacement ni sifuri.

Naona tunakoelekea majuto yatakuwa makubwa zaidi kama hatutawabana viongozi wetu kisheria, maana mtu yeyote anaposhika madaraka kama haelewani na mtangulizi wake tutatarajia vurugu tupu, hii ni nchi jamani tuamkeni, huu sio uwanja wa watu kufanyia kazi chuki zao madarakani, hili ni taifa lenye watu wenye vizazi, wanaohitaji kuona maendeleo, hii nchi sio mali ya familia za viongozi, wakaonyeshane chuki zao huko kwenye familia zao, sio kwenye serikali ya wananchi.

Mi nadhani nidhamu ya woga ifike mwisho, hakuna anaeweza kupiga risasi taifa zima ama kuwafunga watu wote, wananchi tuache uzwazwa muda umekwisha, tujifunze kwa lililotokea kwamba tunahitaji katiba iboreshwe kwa haraka sana vinginevyo mtu yeyote anaweza kurudisha taifa lilikotokea, kama njia iliyobaki ni maandamano watu wahamasishane nchi nzima jambo hilo limeongelewa sana bila vitendo, hilo jambo la katiba mpya, somo la yanayojiri litoshe kuwapa mwanga hata wale waliokuwa hawaelewi.
 

Slowly

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
6,200
2,000
Watanzania mazombi sana, wazee wa kumwachia Mungu, sasa hivi ni mwendo wa ki-hamza tu, wakiingilia angle yako ya ULAJI unakufa na mmoja chap! Sa hv kila mmoja apambanie roho yake
 

Joshua justine

JF-Expert Member
Sep 1, 2021
474
1,000
Watanzania mazombi sana, wazee wa kumwachia Mungu, sasa hivi ni mwendo wa ki-hamza tu, wakiingilia angle yako ya ULAJI unakufa na mmoja chap! Sa hv kila mmoja apambanie roho yake
Mkuu ndio tunakoelekea huko, kama tukishindwa kuandamana pamoja ipo siku kila mmoja ataandamana peke yake, kigaidi zaidi, uvumilivu uliopitiliza ni upumbavu, ipo siku.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom