hili liwe fundisho kwetu kina dada/mama/bibi hata kwa baadhi ya kina kaka/baba. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

hili liwe fundisho kwetu kina dada/mama/bibi hata kwa baadhi ya kina kaka/baba.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by cheusimangala, Oct 18, 2010.

 1. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  NIMEJICHUBUA,JE KUNA DAWA YA KURUDISHA NGOZI YA ZAMANI?

  (hebu ona madhara ya kumkosoa Mungu,turidhike na alivyopenda tuwe jamani)!!
  mimi nina miaka 31, na mwaka 2000 baada ya kutoka tanzania na ngozi yangu asili (origino) ambayo ilikuwa ni nyeusi na ya kun'gaa, marafiki zangu hapa texas, walinishawishi niongeze uweupe kidogo ili nami ning'ae. basi nikapata vidonge vya kungarisha mwili, yaani kuwa mweupe zaidi. Na kusema kweli, nilibadilika ngozi, nikawa mweupe sana, na siyo rahisi mtu kujua kama kweli nimetumia madawa, isipokuwa walionifahamu tangu utotoni ndio wanaoshangaa uweupe huu nimeutoa wapi. sasa nilipataga mimba, ambayo ilikuja kutoka, ila sikujua tatizo ni nini. Hapa majuzi tena, nikashika mimba ya pili bahati mbaya mtoto kafa (yaani mimba imeharibika) nilienda kwa dakitari kutaka kujua tatito liko wapi, hapo ndo nikaambiwa kwamba kuna chemicals kwenye mwili wangu ambazo ndio chanzo cha watoto wangu kufa.
  nimeambiwa kwamba hayo madini ni mengi mno, na nisipoangalia nitakufa na cancer ambayo inaweza kuanza muda wowote. suluhisho linaweza kupatikana nikisafisha damu, na uwezo huo sina, au kama naweza kurudisha ngozi yangu ya zamani kwa sababu sasa hivi ngozi yangu haina kinga tena. Sisikitikii weupe, kwa maana nikitu ambacho nilikitamani, kwa hiyo mzigo lazima niubebe, ombi langu ni ushauri wa kuweza kutoa hizi kemikali mwilini mwangu.kama ni kufa basi tena. cha ajabu ni kwamba mchumba wangu ametishia kuniacha kwani siwezi kuzaa tena. yaani sasa hivi analala nje full, naumia lakini sina jinsi
  naombeni ushauri wenu, niko njia panda

  mdau, texas usa

  P.s:mimi nawakilisha tu sio mie cheusi niliyetumia mkorogo.:nono:
  jumatatu njema.
  love you all
   
 2. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  pole sana dada hapa hata sijui nitoe ushauri gani mie.
  ila nakusikitikia sana,haya mambo ya kuiga hayafai hata kidogo
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,429
  Likes Received: 5,688
  Trophy Points: 280
  kaaa na mchumba wako umwombe ushauri pole yako bado una rehema za mungu kukunusuru
   
 4. Baba Mtu

  Baba Mtu JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2010
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 881
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45

  Ukisikia vitendo mwana majuto mjukuu ndiyo hayo. Pole shosti, jaribu kuona madaktari zaidi huenda ukapata matibabu kwani utaalamu unazidiana. Hata hivyo kilikupata kipi hata ukataka kuibadirisha ngozi yako ya asiri. Mungu hakuwa mjinga alipokuumba na ngozi nyeusi.
   
 5. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Tiens tea can help
   
 6. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  nadhani daktari aliyemwambia haya diye angeweza kumsaidia kuliko kutafuta ushauri mtandaoni.hata hivyo nimefurahi alivyoandika sbb amekua mfano kwa wanaopenda kujikoboa.
   
 7. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #7
  Oct 18, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  mchumba anaanza kulala mbele anatafuta vitu natural labda.
   
 8. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #8
  Oct 18, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Majuto ni mjukuu. Pole sana dada. Hakika hili liwe somo kwa wengine. Japo sijui kama hao wengine wataelewa somo - maana ndoto za kuutafuta uweupe wengi zimewaingia mpaka wanashindwa hata kusikia ushauri. Na ukiwashauri unaonekana mnoko, mwenye wivu, nk.
   
 9. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #9
  Oct 18, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  du baba mtu vipi hapo nilipopigia mstari.shosti tena!
  well said baba mtu wengine wanakwenda mbali wakitafuta uzuri.matokeo yake ndio haya.
   
 10. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #10
  Oct 18, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0


  kuna mdada nilimsikia akisema bora afe kwa kansa kuliko kurudia weusi.can you imagine.!
   
 11. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #11
  Oct 18, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ndio ipi hiyo?
   
 12. M

  MZEE SERENGETI JF-Expert Member

  #12
  Oct 18, 2010
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 214
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Uliyataka mwenyewe,mbona mwanzoni huku tushirikisha,
   
 13. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #13
  Oct 18, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  maji yamemfika shingoni.
   
 14. chloe.obrain

  chloe.obrain JF-Expert Member

  #14
  Oct 18, 2010
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 391
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh!!! Pole yake
   
 15. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #15
  Oct 18, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Mshahara wa dhambi ni Mauti.... alikuwa anamkosoa Mungu!!
   
 16. firstcollina

  firstcollina JF-Expert Member

  #16
  Oct 18, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ni nawachukia sana watu waliojichubua. Hakika NINAAWACHUKUA VIBAYA MNO.

  Ila wewe ni binadamu gani? Husikitikii weupe, wakati hicho ndicho kitu ambacho kinasababisha kufa kwa watoto wasio na hatia. Ungekuwa karibu yangu ningekunasa vibao. Mpuuzi mkubwa wewe, Alaah!!

  Baada ya hapo sasa nakushauri.
  Cha kufanya ni kuomba wadhamini, au kutafuta wafadhili ama msaada ili ukasafishe damu. Kama alivyo kushauri Doctor that is a very IMPORTANT issue. Na unatakiwa kuanza mara moja kabla madhara hayaja komaa zaidi. Kama ulisha bahatika kwenda mpaka TEXAS lazima utakuwa na watu na marafiki wengi sana. I mean mtandao mpana sana, hata mimi nitakuchangi. Take decision immediately.

  Asanteni sana
   
 17. bacha

  bacha JF-Expert Member

  #17
  Oct 18, 2010
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 4,336
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  bora wewe cheusimangala wangu, umeendelea kuwa cheusi hivyo hivyo!Mungu akulinde uendelee na unatural wako!!!!!!
   
 18. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #18
  Oct 18, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Cheusi mpe ushauri afanyeje arudi kuwa kama wewe
   
 19. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #19
  Oct 18, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Subiri kifo cha kansa ya ngozi!
   
 20. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #20
  Oct 18, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hapo ndipo Waafrika tunapoonekana wapuuzi. Ngozi original ambayo ina kinga zote hadi Wazungu wanaitamani kimoyo moyo sisi tunahangaika kuifutilia mbali. Ni matatizo ya akili za wengi wetu,...tunahitaji msaada wa nguvu kujikomboa.

  Pia kuna tatizo la nywele. Nadhani ni muda tu tutaanza kusikia mengi. Kuna mwalimu wangu alitumia dawa nywele zote zikaisha kabisa. Tuwe makini sana na haya madawa.

  Huyu dada anatakiwaa kuendelea na jitihada za kutafuta madaktari wanaoweza kumsaidia. Sijui hali ya huko Texas, ila angekuwa Bongo ningemshauri achukue hatua ya kubembeleza vyombo vya habari (kama TV) na NGO wampatie nafasi kwa lengo la kuokoa wengine wenye mtazamo kama huo. Kwa kufanya hivyo ama jamii inaweza kusaidia kuyabana makampuni ya madawa yatoe tiba au kupata msamaria mwema akamwonea huruma na kumpa tiba. Hii kitu ikifika kwa mtu kama Oprah nadhani itakuwa big TV news na Talk show yake inaweza kuwa ya nguvu.

  Ni maoni na ushauri wangu,

  Retired Major Gen. DC
   
Loading...