Hili linaweza kuwa jibu tosha kwa wale wanawake wanaopenda kupeleka matatizo ya kimahusiano mitandaoni

Course Coordinator

JF-Expert Member
Jul 27, 2019
1,678
3,052
Dear Uncle
Naomba msaada wako nifanye nini? Mimi ni mke wa mtu, na mume wangu tunapendana sana. Juzi niliondoka kwenda kazini nikamuacha mume wangu ana angalia TV. Sikufika mbali gari ghafla likazima, nikalazimika kutembea kwa miguu kurudi nyumbani ili niikamwambie mume wangu anisaidie. Nilipofika nyumbani sikuamini macho yangu baada kumkuta mume wangu na binti wa
jirani yetu. Nilimkabiri mume wangu na kwa bahati nzuri kakubali makosa kuwa uhusiano wao una mwaka sasa, lakini cha ajabu amesema atalazimika kumuacha huyo binti pole pole ili asimchanganye kisaikolojia kwa kuwa bado mdogo.

Je hii ni sawa? Nifanye nini? Naomba
ushauri Mzee wangu Maliefwale

JIBU
Binti yangu Juliana
Nimesoma kwa makini ujumbe wako, kitu ambacho nimekiona mara moja ni hili tatizo la gari kuzimika ghafla. Kwanini uendeshe gari na baada ya muda mfupi lizime? Hapa kuna matatizo kadha wa kadha ambayo yanaweza kuwa chanzo. Inawezekana plag mbovu au uchafu umeingia kwenye mrija unaopeleka mafuta kwenye injin. Au pengine ni tatizo la umeme, au fuel pump, ulicheki kama petroli ipo? Ikiwezekana waone mafundi warekebishe hivyo nilivyovitaja.

Nategemea ushauri huo utakusaidia mwanangu.

Solve matatizo ya kimahusiano wewe na mwenzi wako nyumbani usipeleke kwa akina Idd Makengo watakupotezea ndoa.
 
1. Alitakiwa ampigie simu mumewe aende msaidia palepale barabarani.

2. Kama mume hakupokea simu alitakiwa ampigie jirani amwambie mumewe apokee simu ya mkewe.

3. Tafuta houseboy leta ndani, asiwe na mahusiano na houseboy ila amzoee sanaa hii itamfanya mume awe karibu na mkewe muda mwingi na atamsahau binti jirani.

Kasie Paltinums Matata.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom