Hili linanichanganya: Nani mwenye fedha kanali wa jeshi au mkazi wa kawaida wa kigamboni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hili linanichanganya: Nani mwenye fedha kanali wa jeshi au mkazi wa kawaida wa kigamboni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Nanu, Mar 8, 2011.

 1. N

  Nanu JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ndugu zangu kuna hili linaniumiza akili yangu na nimeshindwa kuendelea nalo. Siku moja nilikwenda ferry ya Magogoni. Nilichoona pale ikaniachia maswali mengi. Unakuta mwanajeshi na kwanza mwenye cheyo kama kanali yuko na familia yake na gari lake binafsi wanapanda ferry bure! Gari halilipiwi, yeye mwenyewe halipi na familia yake au abiri wake kwenye gari lake pia hawalipi.
  Si hilo tu bali pia wafanyakazi wengine wa serikali ikiwa ni pamoja na mkuu wa Chuo Cha Mwl. Nyerere Magogoni, polisi, wakurugenzi wa idara mbalimbali za serikali pia hawalipi kutumia hii ferry!
  Kwa watoto wa shule nakubaliana wasilipe maana hawana kipato. Mtu wa kawaida aliyefunga mihogo kidogo kwenye baiskeli, na mwingine yeyote bila kujali kipato chake lazima alipie ferry.
  Swali langu ni hili hapa: Hawa wanaoitwa wafanyakazi na wakubwa wa serikali katika nyadhifa mbalimbali kwanini wasilipe angalau nauli ili kuchangia "operation cost" ya kivuko? Magari ambayo yanavushwa kwa siku pale Kivukoni ni zaidi ya 3000 lakini kati ya hizi zaidi ya 1600 hayalipi nauli ya kivuko! Kila idara ina bajeti yake ambayo pia ni pamoja na usafiri kwanini wasilipe na hata hivyo hii pesa inarudi serikalini na zikiisha wanaomba zingine za kutumia? Hao maofisa wa serikali si ndiyo wanakipato kikubwa kuliko wananchi wa kawaida lakini wao ndiyo wanafurahia huduma ya bure?
  Je hii si ndiyo inaweza ikawa sababu mojawapo inayowafanya watumishi wa serikali wasiwe na machungu hasa katika matumizi yasiyokuwa ya lazima za fedha za walipa kodi maana wao si sehemu ya hiyo kodi?
  Nadhani ni vizuri kila mtu angechangia huduma, na kama tatizo ni kipato basi swala la kipato liangaliwe lenyewe kama lenyewe na litafutiwe ufumbuzi. Mimi bado siafiki na sikubali mtumishi wa serikali au wa umma anayetumia huduma za kijamii bila kuchangia. Hata kwenye daladala polisi na wanajeshi pia walipe nauli na kwanza wawe mstari wa mbele kuonyesha mfano.
   
 2. doup

  doup JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2011
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  maji hufuata mkondo kuelekea baharini sio jangwani, na aliye nacho ataongezewa. na sisi kwa ufinyu wa kufikiri tumechuria hivyo hivyo.
  Heri Punda afe lakini mzigo ufike.
   
 3. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  nakubaliana nawe, kila mtu anatakiwa alipie gharama stahiki, mafao yake ajadiliane na mwajiri wake period
   
 4. Revolution

  Revolution JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2011
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 567
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 60
  Ni kweli kabisa, au hizo nauli zingewekwa katika entitlements zao ili waajiri wao wazisubmit kwa wahusika wa vivuko kila mwezi, ingawaje ni fedha za serikali na zinarudi huko huko lakini itaonyesha responsiveness....hiyo ni kama unavyojikopesha bidhaa dukani kwako na kuilipa kwa fedha zinazotokana na faida ya duka hilohilo........
   
Loading...