Hili Linajadilika?

Albedo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
5,559
1,452
Padre Kimaro kuachiwa huru

Padri Kimaro aachiwa huru
Na Bernard James

PADRI Sixtus Kimaro (40), aliyekuwa amefungwa jela miaka 35 mwaka 2005 baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mvulana mwenye umri wa miaka 17, ameachiwa huru jana baada ya Mahakama Kuu kutupilia mbali hatia zote mbili na kifungo.

Akitoa uamuzi huo jana Jaji wa Mahakama Kuu, Robert Makaramba alisema amemwachia huru Padri Kimaro kwa kuwa upande wa Mashitaka haukutoa ushahidi wa uhakika kwa mashtaka anayodaiwa kuyatenda kwa kijana aliyekamatwa akiwa naye katika eneo la Changanyikeni, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Pia Jaji Makaramba alifuta amri ya awali iliyotolewa ya Mahakama iliyomtaka Padri huyo alipe faini ya Sh milioni mbili.

Jaji Makaramba alitupilia mbali hatia aliyokutwa nayo ya ulawiti akisema hakukuwa na ushahidi wa moja kwa moja unaoonyesha kwamba wawili hao walikuwa wakitenda jambo lililodaiwa kutendeka.

Baada ya kutolewa uamuzi huo Padri Kimaro alinyanyua mikono yake juu na macho ikiwa ni ishara ya kumshukuru mungu kwa hatua iliyofikiwa na mahakama.

Padre Kimaro alionekana kububujikwa machozi wakati Jaji akiwa amefikia katikati kusoma hukumu hali iliyomfanya atumie kitambaa kujifuta.

Awali akiwasilisha ushahidi wa mteja wake, Wakili wa Padri Kimaro alisema upande wa mashitaka ulishindwa kuwasilisha ushahidi wa kuridhisha kumuunganisha na makosa aliyodaiwa kukutwa nayo.

Padri huyo alihukumiwa kifungo hicho katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kupatikana na hatia katika mashitaka yote matatu yaliyokuwa yakimkabili ya kulawiti, shambulio la aibu na kumdhalilisha mvulana huyo.

Alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela katika kosa la kwanza la kulawiti na miaka mitano katika kosa la pili la shambulio la aibu na kumtaka mshitakiwa huyo kumlipa Sh2 milioni mvulana aliyelawitiwa. Adhabu hizo zilikwenda sambamba.

Source: mwananchi
 
Invisible nimeiweka hii huku kwenye politics, kama sio mahala pake waweza kuiweka sehemu husika
 
MAHAKAMA IMEAMUA.....TUNASUBIRI KUSIKIA MAHAKAMA ZA VICHOCHORONI ZINASEMAJE....!
 
Inasemekana hapakuwepo na ushahidi wa kutosha!...Mshitaka alitakiwa kuwa na ushahidi mbali na mashtaka yake...
There were no witnesses or hard evidence other than the hearsay!

Mhhhhh!, sasa jaribu kufikiria huo ushahidi ulotakiwa maanake maneno matupu ktk swala hili la mchezo wa kujificha imeelezwa kuwa ni hearsay,..Yalitakiwa maji ya uzima - heee hee hee!!
Kisha hivi kweli Tanzania kuna kitengo maalum cha Polisi cha kukusanya ushahidi wanaoweza simama mahakamani kama wataalam wa Crime scene Investigation?..

Babu Seya vipi naye kulikuwepo na ushahidi gani zaidi za?
 
Mahakamani huwa tunafuata sheria iliyopo maana tukitaka haki hamna anayeweza kuionyesha kwa kuwa wote ni wanadamu na haki inatolewa na Mungu pekee.Ndo maana hata wana usalama wakikukamata wanakutafutia kitu cha kukutia hatiani ili ushitakiwe.
Sheria tulizo nazo nyingi hazikidhi haja za leo,naamini wanasheria wanajua hilo,kwa hiyo huyu kasisi kupeta mtaani ni sheria tuliyo nayo haikuweza kumshikiria kwa kifungo chake chake hicho cha miaka makumi matatu na hamsa.
 
Mlidhani miujiza ipo kanisani tu??
Haya angalieni miujiza ya mahakamani,
Ila kuna rafiki yangu mmoja pale washington aliniambia kuwa kule marekani watu ambao wamefungwa ni wenye haki yaani innocent na majahili (mafisadi) wapo nje.
Do You know why?
 
Kwa mfumo wa kusamehe saba mala sabini sijui Askofu Kiraini atamsamehe na kumpokea kanisani? YUaani kumpa Kigango! Au ndo amepoteza Ajira? Mnaolijua hili mtuambie!!
 
http://habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/27294-padri-sixtus-kimaro-asakwa-na-mahakama

Nimesikia kwa juujuu kuwa Padri Sixtus Kimario aliyehukumiwa kwa makosa ya kulawiti miaka ya 2006 na kutoka kwa kushinda rufaa mwaka 2008 amefariki dunia huko Msumbiji.

Jambo la kushangaza ni kuwa alikuwa anatafutwa na mahakama baada ya Serikali kukata rufaa na hata Kanisa lilipotakiwa kutoa taarifa zake kuhusu alipo lilitamka kuwa halimtambui na hakuwa mwajiri/mtumishi wake,

Sijui hili limekaaje na mwenye habari kamili atujuze...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom