Slim Mchuma
Member
- Aug 19, 2016
- 83
- 51
Biashara iliyokuwa ikifanywa na Wawekezaji ya kununua vifaranga na Mayai kutoka nchi za nje imepigwa marufuku, baada ya Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha, kusema kuwa Serikali haitaruhusu Mwekezaji yeyote kupewa kibali cha kuingiza vifaranga au mayai ya kuku kutoka nchi za nje. Ameyasema hayo Bungeni Mjini Dodoma, wakati wa maswali na majibu amesema kuwa katika kusimamia hilo kuanzia mwaka 2013 hadi 2017 vifaranga 67,500 vilivyoingizwa nchini kinyume na sheria viliteketezwa.