Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,985
- 20,263
Vita vya Kiuchumi Tanzania chini ya mradi mtambuka wa maporomoko ya Rufiji, siasa ya Mazingira duniani na muundo na mienendo ya Shirika la Elimu, Sayansi na Udhibiti wa Mazingira duniani (UNESCO), vinanipa sababu ya kuiponeza TISS katika ulimbe huu wa vita vya kiuchumi.
Bonde la Rufiji liko kwenye urithi wa dunia kwamjibu wa Shirika la Uhifadhi wa Mazingira (UNESCO), Na hivyo ulinzi wa bonde hili ni kwa sheria za kidunia sio kwa sheria za Tanzania, hapa ndipo ambapo nataka kusifu idara za ujasusi na kumsifu Rais Magufuli kwa kuishinda dunia dhidi ya misimano na sera za mashirika haya ya kidunia ambayo Mwalimu yalimshinda, Mwinyi yalimshinda, Mkapa yakamshinda, Kikwete yakamshinda
Kwa wiki kadhaa nimekuwa nikipitia nyaraka za kijasusi za mashirika na taasisi mbalimbali ulimwenguni (Realiised docs), nimejiridhisha kuwa vita nikubwa kuliko wengi wanavyofikiri, na ikiwa mradi wa umeme bonde la Rufiji utafanikiwa, basi TISS itaingia kwenye historia ya mashirika bora kabisa ulimwenguni kwa counter intelligence hii. Palipo na uthubutu lazima tupongeze,
Awali mradi huu wa Umeme wa Stiegler's Gorge Ethiopia walikubali kujenga, lakini hakuna maelezo kama waliishia wapi ama walishindwa tenda. Zikawepo taarifa za Waturuki kuwa watajenga, nazo zikaishia hewani. Kisha tukashuhudia Arabb Contractors wa Misri wakisaini mikataba ya ujenzi. Bado ujenzi rasmi haijaanza, lakini hatua tu ya kuthubutu kusaini mkataba ni hatua kubwa inayostahili kupongezwa.
Bunge la Ujerumani liliweka azimo kuitaka serikali ya nchi hiyo kuzuia ujenzi wa mradi huo wa Rufiji na badala yake serikali ya Ujerumani isaidie kujenga vinu vya gesi kwaajili ya nishati ya umeme. Kwakuangazia jambo hili watu wengi wanaweza kujiuliza, itakuwaje nchi ya Ujerumani iingilie masuala ya ndani ya Tanzania? Mifumo ya kijasusi iko hivi, kwamjibu wa Nyaraka za idara ya ujasusi ya nchini Lithium (Anual report 2016) inaonyesha kuwa Ujerumani pekee ina majasusi 11 wa ngazi za juu ndani ya UNESCO, na kwa nadharia hiyo, Ujerumani ikitaka kuzuia miradi yoyote yenye uharibifu wa mazingira inatumia msukumo wa UNESCO.
Kinachoweza kutokea ni kuwa UNESCO inaweza kuiandikia barua ya katazo nchi husika kwamba pale ni sehemu ya Urithi wa Dunia (World heritage site.) na hairuhuriwi kupajenga. Na wanaonya kuwa ukiwa mbishi na ukaendelea kujenga utakuwa black listed. Na kampuni inayopata tenda ya kujenga nayo inapewa barua na kuonywa kuwa itakuwa black listed na Bank Account zako zitakamatwa. Kwakufanya hivyo wanashinikiza kampuni zijitoe katika mradi husika.
Majasusi hawa wamefanya hivyo kuidhibiti Iran, enzi za Reza Khan kwakutumia mashirika haya ya kidunia , ambayo mengi ni mashirika ya kijasusi. Pia nchi za Panama zimewahi kukumbana na nguvu ya mashirika haya.
Kwa namna yoyote naipongeza Serikali kwa ujasiri huu wa kufunga masikio na kelele za kidunia na kuamua kuanzisha mradi huu uliokwamba tangu miaka ya 60+. Hii ni hatua kubwa sana na ninaamini itaacha legacy kubwa sana kwa rais Magufuli na kwa vyombo vya ujasusi nchini ikiwa utafanikiwa, ingawa hakuna nchi au kikundi kilichowahi kushindana na mashirika haya ya kidunia na kikashinda, zaidi ya hapo labda ziwe ni siasa za kura. Bado naamini tumethubutu pakubwa sana, na katika ndoto tutashinda...
Unaweza kujipa nafasi ya kusoma kwa undani zaidi kitabu cha Ujasusi kujua nama Ujasusi dhidi ya Ujasusi unavyofanya kazi na mifano hai toka katika viunga vya dunia ya ujasusi.
Nakuletea ulipo PROMOSHENI ya VALENTINE DAY ya Kitabu cha Ujasusi nakala TANO kila nakala ni 50,000/= tu badala ya bei halisi ya 80,000/=
.
Nunua kwa 50,000 kwa 0715865544 au 0755865544. Kisha tuma majina yako na mahali ulipo, kitabu kitaletwa popote ulipo Tanzania