Hili laWaziri Lugola ni kashfa mpya kwa Serikali

malisoka

JF-Expert Member
Jul 8, 2012
1,860
2,637
Kama waziri wa ngazi za juu wa nchi waziri wa mambo ya ndani Mzee Lugola anatamka kwamba wakati Tundu Lissu anashambuliwa katika nyumba za viongozi wa juu wa seriakli akiwemo Naibu speaker kulikuwa hakuna kabisa ulinzi wa CCTV camera. Hii ina maana gani?

Alipotekwa MO juhudi mkubwa lilifanywa kwa kupitia CCTV camera kuwajua waliomteka.


Na Ikiwa serikali imetoa tamko kupitia mkuu wa Mkoa wa DSM na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kwamba bar , Geust house na Ofisi zote zifungwa CCTV Camera,

Na Ikiwa Hata kwenye maduka ya lejaleja yanayouza mafuta ya kula na taa kwa chupa ya soda yamefungwa CCTV Camera kwa ulinzi.


Je Waziri LUgola anataka kutuaminisha kwamba wamewapuuza wabunge na viongozi wa serikali wanaokaa Katika majengo ya Area D dodoma?

Jengo alilopigwa lisasi Lissu linaweza kwa usembe kutokuwa na CCTV Camera.

Lakini Majengo hayo hayo wanapokaa wabunge na viongozi wa serikali yanajulikana kama Sengia hapo hapo mkabala na lilipotokea shambulizi kuna CCTV Camera za kutosha wabunge au hao viongozi wa serikali wamejiwekea wenyewe.

Je ni Muhimu au si Muhimu Kuwa na CCTV Camera kwa viongozi wetu wa juu kama Naibu Speaker na Makatibu wakuu?

Na kama kweli hakukuwa na CCTV Camera nani wa kulaumiwa na nani anatakiwa kuwajibishwa kwa tukio la Lissu kwamba walifanya makusudi kutokuweka CCTV Camera.

Nawashauri serikali wasicheze na maisha ya viongozi wetu tunawahitaji sana, wao na mali zao.

Mh Lugola kwa kauli yako ni sawa na kusema kwamba wakati wa shambulio la Lissu HAKUKUWA NA ULINZI WA KUTOSHA!
 
MTU akishakuwa ccm uwezo wake kufikiri, kutathmini nakutenda vinarudi kuwa sifuri.

MTU akishakuwa ccm haiwezi kuongoza kwa weledi ni mipasho, uwongo uzandiki na uzushi

Wanatia aibu hawa watu, wanatufedhehesha na kutufanya wanyonge popote kwasababu nikama watanzania hutujitambuwi
 
Kangi Lugola awe muangalifu na karne hii ya "tekelinalokujia" (Technology),; tekelinalokujia litamuumbua kabla jogoo halijawika! Kakobe alikana kuwajua viongozi wa Chadema mara paaap! picha hizo akiwa jukwaani akihutubia mkutano wa kampeni na nyuma yake kwa karibu kabisa akiwa amekaa Edward Lowassa ambaye alikuwa mgombea Urais wa UKAWA!
 
Hawa akina Kangi hawana lolote ni watu wanaotumika kujaribu kupooza moto usienee zaidi.

Kwanza angekaa tu kimya, kuna siku hayo anayoropoka yatakuja kumpa shida asijue. He is a very shallow thinker with myopic mind.
 
Lissu akitua nchini watasema Lissu alipanga mwenyewe kujipiga risasi. Chezea awamu hii kila mtu msemaji wa matukio mradi umfurahishe mfalme.
 
Jamaa amekua kama Gari la mkaa leo anakuja na hoja nzuri kesho unamsikia na hoja ya ajabu ajabu haeleweki anataka kusimamia nini haswa...
 
Tumbo ulindwa kwa gharama yeyeto. Tl na dereva wake wakimaliza matibabu wanarudi wakurudi utasikia danadana kigugumizi cha kuwahoji tena visingizio kibao
 
Dereva hakuwa mlengwa sasa zingempataje risasi? Wasiojulikana wale sio wataalamu au wajuzi wa kutumia silaha thus wamelengalenga na awakuwa na plan B, kupona kwa Tl ni miujiza na mpango wa Mungu ili watubu,ila shingo zao ngumu
 
Je walinzi nani aliwaondoa,.?
Walinzi nani arawaondoa wakati unaambiwa ni Kampuni binafsi na si polisi.Sasa kama ni kampuni binafsi inategemea na mkataba ulioingiwa na wahusika wa eneo linalo takiwa kulindwa. Inaweza ikawa ulinzi ni wa usiku tu katika eneo ilo au masaa 24 tatizo lililopo kwenye sakata ili waongeaji ni upande mmoja tu sasa upande mwingine ukizungumza inaonekana waongo. Nivizuri Lisu na Dereva warudi wahojiwe wanayo fahamu. Mambo ya Camera na Ulinzi wa eneo husika itakua Lisu anafahamu vizuri na Upande wa pili wafafanue.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom