Hili la wizi wa mafuta TPA linaumiza vichwa

senzighe

JF-Expert Member
Jan 1, 2012
1,979
1,512
Kwanza kabisa nimpongeze DC wa Kigamboni kwa swala zima la kuwabaini wezi wa mafuta kwenye mabomba ya mafuta ya mamlaka ya Bandari tanzania (TPA) kule Kigamboni cha kushangaza kabisa eti TPA nao wanadiriki kupongeza juhudi za mkuu wa Wilaya katika kuwabaini wezi wa mafuta. Hii ni aibu kubwa kwa sababu ulinzi na usalama wa miundo mbinu ya TPA inapaswa kuwa ya TPA wenyewe na sio kungojea kupongeza juhudi za DC wa Kigamboni.

Hii inatoa taswira kwamba baadhi ya wafanyakazi wa TPA wanahusika na wizi huu unaokera kwa sababu tunawaona hata uzembe wao kwenye maeneo mengine. Haiwezekani mafuta yaibiwe kiasi hicho na wao wasiwe na habari kwa kipindi ambacho hakijulikani. Wengine ukiwatembelea katika maofisi yao utakuta hawapo makini na kazi zao mpaka tunajiuliza sasa hawa wapo kwa ajili ya kazi au wana mengine.

Unaweza ukaongea jambo la maana na bosi leo lakini kesho ukienda hajui hata jana mlizungumza nini.Wanajali tu yale ambayo yana maslahi binafsi kwao. Watu kama hawa hawawezi kuwa na uwezo wa kuiangalia miundombinu yao sawasawa. Serikali chunguzeni uhusika wa wafanyakazi wa TPA kwenye wizi na uharibifu huu.
 
Back
Top Bottom