Hili la wanajeshi kutumia ilani ya chama imekaaje?

Juzi wakati Mheshimiwa Waziri wa ndani akihutubia maafisa wa juu wa vyombo vya ulinzi aliwauliza ni wangapi wana ilani ya chama na wanyooshe juu.

Wakabaki kutazamana tu kila mtu anamuangalia mwenzake.

Hivi jamani Afisa wa polisi, magereza, uhamiaji au zimamoto anatakiwa k
Juzi wakati Mheshimiwa Waziri wa ndani akihutubia maafisa wa juu wa vyombo vya ulinzi aliwauliza ni wangapi wana ilani ya chama na wanyooshe juu.

Wakabaki kutazamana tu kila mtu anamuangalia mwenzake.

Hivi jamani Afisa wa polisi, magereza, uhamiaji au zimamoto anatakiwa kutembea na Ilani ya chama?

Maana kwa mujibu wa katiba wao wanatumia sheria ya kulinda serikali na wananchi bila kufuata ilani yoyote.

Je, huyu waziri anajua majukumu ya jeshi au ndio utaratibu Mpya?

Alloooo!!!!!!!
Nadhani baada chama kushinda Kinaanda muongozo wa jinsi yq kutekeleza ilani yake. Inaweza kuwa mipango ya vipindi vjfupi au virefu, pamoja na kuwakilishwa kwenye budget bungeni. Ilani haionyeshi jinsi ya kutekeleza ahadi. Hivyo watumishi hawahitaji kuwa na ilani ila mipango ya serikali iliyoanishwa kwa utekelezaji.
 
Hakuna anayebisha kuhusu utekelezwaji wa ilani, kwa sababu ccm ndiyo 'walioshinda' tenda ya kutufanyia kazi kwa miaka mitano. Kitu ambacho wewe unatakiwa kuelewa ni kwamba, utekelezwaji huo ni sehemu ya maisha ambayo tayari yanaendelea kwa utaratibu mama ambao ni KATIBA. Kwa akili yako mhandisi akishinda tenda ya kujenga madaraja, watu wake site watatumia/watakuwa wanarejea kwenye andiko la mradi kila wanapotaka kuchanganya zege au watatumia maelekezo ya taaluma ya uinjinia?. Fikiria hiyo mifano mepesi alafu, jijibu kama unachokishupalia kinawapa matumaini au kuwasikitisha unaowatetea!
Ilani imesema serikali itajenga barabara kadhaa hapo waandisi watafuata ni barabara zipi hizo za kujenga....tumia akili kidogo tu kujua haya mambo.Aliyekuambia ilani inaeleza ratio za kuchanganya zege ni nani?...tumia ubongo wako kidogo kutafakari hayo...
 
Ni kweli sie wafanyakazi wa serikali (hata wa sekta binafsi) tunatekeleza ilani ya chama kilichoshinda uchaguzi. Ilani ya chama inakuwa incorporated katika sera, mipango na mikakati ya wizara, idara, mashirika na wakala wa serikali lakini sio Ilani ya chama directly. Mfano: ilani ikisema "tutafufua majosho 132 ya kuogeshea mifugo nchi nzima kati ya 2015-2020" basi wizara ya mifugo inapopanga bajeti yake inajiwekea lengo kila mwaka ifufue majosho mangapi ili ikifika mwaka 2020 idadi hiyo ya majosho iwe imefufuliwa. Kwa maantiki hii hakuna haja ya kulazimisha watumishi kutembea na ilani ya chama cha kisiasa. Huo ni ujuha na ulevi wa madaraka. Ni umbumbumbu wa kutojua mpaka wa serikali na chama katika utekelezaji wa majukumu yao.
Hakuna aliyelazimishwa kutembea na ilani.....waliulizwa mpango kazi ambao unatokana na ilani ya CCM...tusipotoshe jambo
 
Ukweli unaujua ila umeamua utetee tumbo lako na si vizazi vyako pole sana. Ndo nyie mnazaa watoto afu unatoa kafara. Wewe unadhani unayoyatetea hapa hayatawathiri watoto wako.
Asubuhi njema.
Serikali inatekeleza ilani ya CCM
 
Shida kubwa iliyofanywa kikatiba ni polisi,magereza,uhamiaji na zimamoto kuwaita majeshi hilo nikosa kubwa hata kama zilikuwa ni sababu za kisiasa. Zile ni idara dunian huwezi kuta eti jeshi la zimamoto ama magereza ila ni idara ya magereza siasa imeharibu
Duniani kote majeshi ni army ambapo kwetu ni landforce ama askari wa miguu,navy ama wanamaji airforce marine na mengne ambayo yanajukumu ya kulinda nchi ila hizo idara za usalama wa raia haziwezi kuwa jeshi
Nini maana ya police force ? .hili neno linatumika nchi nyingi duniani
 
Hakuna aliyelazimishwa kutembea na ilani.....waliulizwa mpango kazi ambao unatokana na ilani ya CCM...tusipotoshe jambo
waziri wa sekta yako anakuuliza uionyanyue juu kitabu cha ilani kama umekuja nacho kikaoni then since then unamuona anatembea nacho muda wote maana yake nini?
 
waziri wa sekta yako anakuuliza uionyanyue juu kitabu cha ilani kama umekuja nacho kikaoni then since then unamuona anatembea nacho muda wote maana yake nini?
Jamani waliulizwa mpango kazi ...work plan ya kila mmoja kitengo au idara yake na si Ilani.....mbona wabongo tunapenda sana kubadili maneno
 
Juzi wakati Mheshimiwa Waziri wa ndani akihutubia maafisa wa juu wa vyombo vya ulinzi aliwauliza ni wangapi wana ilani ya chama na wanyooshe juu.

Wakabaki kutazamana tu kila mtu anamuangalia mwenzake.

Hivi jamani Afisa wa polisi, magereza, uhamiaji au zimamoto anatakiwa kutembea na Ilani ya chama?

Maana kwa mujibu wa katiba wao wanatumia sheria ya kulinda serikali na wananchi bila kufuata ilani yoyote.

Je, huyu waziri anajua majukumu ya jeshi au ndio utaratibu Mpya?

Alloooo!!!!!!!

Hii nchi inaongozwa na vihiyo...kila anayeteuliwa ni afadhali ya aliyetoka....!!
Hivi kuna mtu anaweza kunipa Elimu na Taaluma aliyosomea huyu Mbunge wa Mwibara Bwana Kangi Lugola...lakini pia napenda kujua kama huyu jamaa ni Mkurya, Mzanaki au Msukuma kwa kabila....maana yajayo yanafurahisha!
 
Hahahahahahahah eti " wangapi wana ilani ya chama" hahahahahahahh

Hii nchi hii jamani khaa!!
 
Wanatekeleza Ilani ya CCM kisheria wala hakuna jipya hapo kila kitu kimeanishwa ndani ya Ilani ya CCM namna gani Serikali itafanya kazi za utekelezaji baada ya uchaguzi....kama ambavyo CHADEMA nayo kama ingeshinda Serikali ingetekeleza Ilani ya CHADEMA yakiwemo na hayo Majeshi ya Ulinzi na Usalama.

UTAPATA TAABU SANAAAAAA
aaah broh. ..jeshi likaongozwa na ilani ya chama kweli?
auwez ukawa upo serious!!!!
em kajielimishe asee

usicho kijua ilani inatekelezwa na wanasiasa/raia = safu yote ya juu wizarani

sio kila mtu anajua majeshi yanajiendesha vip vitu vingine vipo beyond your knowledge
 
Ilani ya chama ndiyo imeeleza namna gani masuala ya ulinzi yatafanyika, humo ndimo kuna nyumba za askari, uboreshaji wa miundombinu ya vyombo vyetu vya ulinzi,vitendeakazi vya majeshi nk. Pia kumbuka serikali ni ya ccm na ndio inayopamga ,matumizi ya bajeti ambayo inapitishwa na bunge. Je kama wakuu wa vyombo vya ulinzi hawana ilani inayopangiwa bajeti, watatekelezaji majukumu yao?
Si tayari yanakuwepo kwenye mpango wa taifa wa miaka 5 au hujui ilani huwa inafungamanishwa na mpango wa taifa wa mwaka mmoja mmoja na miaka 5

Kazi kwelikweli
 
Hujaambiwa kutembea nayo bwana mbona mnapenda sana kubadili maneno.....ila kazi zao zipo ambazo wanatakiwa kufuata ilani ya CCM kwasababu kuna mambo yaliyoainishwa mle ili kuyatekeleza.Liko wazi tu kuhusu ulinzi na usalama wa nchi pamoja na GO walizonazo.
ebu weka uchama pembeni myb unaeza ukawa na point
 
Wanatekeleza Ilani ya CCM kisheria wala hakuna jipya hapo kila kitu kimeanishwa ndani ya Ilani ya CCM namna gani Serikali itafanya kazi za utekelezaji baada ya uchaguzi....kama ambavyo CHADEMA nayo kama ingeshinda Serikali ingetekeleza Ilani ya CHADEMA yakiwemo na hayo Majeshi ya Ulinzi na Usalama.

UTAPATA TAABU SANAAAAAA
soma tena ulichokiandika alfu tafakari upya upana wa vyombo vyetu vya ulinzi mkuu alfu viongozwe na ilan ya chama
 
Sijui sheria zinasemaje, lakini uongozi haupaswi kuwa juu ya legally right or legally wrong. Kuna perceptions and image pia. Ni kweli serikali ya CCM inatekeleza ilani ya CCM kama ambavyo serikali ya chochote.

Lakini kwenye serikali yoyote duniani, kuna political appointees na career bureaucrats. Political appointees, concern yao kubwa ni kusimamia hiyo ilani ya chama tawala, kuhakikisha inatekelezwa, bureaucrats kazi yao ni kusimamia sheria, taratibu na uendeshaji wa kila siku wa serikali;

Kama political appointee anaona ilani haiendi mbele, anapaswa kubadilisha sheria, sera au taratibu, sio kumpa bureaucrat ilani. Ilani ni malengo tu, kisheria haina nguvu yoyote.

Leo hii ilani inaweza sema "Tuhakikisha tunaondoa kodi kwenye vifaa vya ujenzi", waziri hawezi kumpa ilani commissioner wa TRA na kumwambia tekeleza! Kama ni swala la kisheria, Waziri anapaswa kwenda kubadilisha sheria bungeni au kutengeneza mwongozo mpya; na aseme kabisa, hili ni kutekeleza ilani. Then commissioner wa TRA atafuata.

Sio busara, kuwapa bureaucrats ilani ya chama tawala. Kazi yao sio kutekeleza ilani, wao wapo kusimamia sheria na taratibu. Ndio maana utakuta wapo wizarani au kwenye taasisi miaka 40; chini ya mawaziri kati ya 5-10
 
Back
Top Bottom