Hili la Wamachinga Rais amenena

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,886
938
HILI LA WAMACHINGA RAIS AMENENA

Ni bahati njema kwamba idadi kubwa ya watu wetu katika taifa ni vijana, ambao ni nguvukazi muhimu katika juhudi za kujiletea maendeleo. Kuwa na vijana wengi ni moja ya vigezo muhimu sana kwa uzalishaji mali wa taifa lolote, ndiyo maana baadhi ya mataifa duniani hata yale yaliyoendelea sasa yanahaha kutaka kutafuta mbinu zote za kuwashawishi watu wao waanze kuzaliana tena baada ya kujikuta asilimia kubwa ya wananchi ni wazee.

Uwiano huu wa wingi wa vijana miongoni mwa watu wa Tanzania, ni mtaji muhimu katika kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo ya taifa letu sasa na kwa wakati ujao.

Hapa tulipo vijana wanafanya biashara mitaani bila mpangilio maalumu, wanaziba baishara za wafanyabiashara wakubwa na wengine wanakuwa kwenye mazingira hatarishi kwa maana ya kupanga bidhaa barabarani.

Hii siyo namna nzuri ya kuendesha biashara kwa vijana hawa ambao ni nguvu kazi muhimu kwa taifa, uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan kuwataka wakuu wa mikoa na wilaya kuwapanga vizuri kwenye maeneo stahiki umekuja wakati muafaka sana kwa sababu;

1. Hali ilivyo sasa ikiendelea itafika mahali miji itashindwa kuhimili ongezeko la vijana wanaoingia mijini kila siku kutafuta maisha.

2. Kuwapanga kwenye maeneo maalumu ya biashara yatawawezesha wamamchinga kuwa na maeneo ya biasahra yanayoeleweka (kwa msemo wao kuwa na anwani) na hivyo kuwafanya waaminike hata kwa taasisi za kifedha wanapohitaji mikopo.

3. Kutaipanua miji na kuifanya kuwa na maeneo maalumu ya kibiashara, ambapo inatakuwa rahisi kwa wateja kwenda maeneo hayo kwa ajali ya kujipatia mahitaji yao.

4. Maeneo haya yakipangwa vyema yataiwezesha miji kuwa na ‘Kariakoo’ zao ndogo ndogo na hivyo kuchechemua zaidi biashara za wamamchanga na uchumi wa maeneo hayo.

Wito kwa wamachinga wote ni kutoa ushirikiano kwa mamlaka za miji ili shughuli ya kujipanga upya iwe yenye manufaa kwa pande zote.

Vijana Nguvu Kazi
Taifa Ni Vijana
Machinga Twende Kisasa Zaidi
 
Back
Top Bottom