Hili la Wamachinga Rais amenena

Ojuolegbha

Member
Sep 6, 2020
22
75
Hili la Wamachinga Rais amenena

Na Israel Mngamba

Ni bahati njema kwamba idadi kubwa ya watu wetu katika taifa ni vijana, ambao ni nguvukazi muhimu katika juhudi za kujiletea maendeleo. Kuwa na vijana wengi ni moja ya vigezo muhimu sana kwa uzalishaji mali wa taifa lolote, ndiyo maana baadhi ya mataifa duniani hata yale yaliyoendelea sasa yanahaha kutaka kutafuta mbinu zote za kuwashawishi watu wao waanze kuzaliana tena baada ya kujikuta asilimia kubwa ya wananchi ni wazee.

Uwiano huu wa wingi wa vijana miongoni mwa watu wa Tanzania, ni mtaji muhimu katika kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo ya taifa letu sasa na kwa wakati ujao.

Hapa tulipo vijana wanafanya biashara mitaani bila mpangilio maalumu, wanaziba baishara za wafanyabiashara wakubwa na wengine wanakuwa kwenye mazingira hatarishi kwa maana ya kupanga bidhaa barabarani.

Hii siyo namna nzuri ya kuendesha biashara kwa vijana hawa ambao ni nguvu kazi muhimu kwa taifa, uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan kuwataka wakuu wa mikoa na wilaya kuwapanga vizuri kwenye maeneo stahiki umekuja wakati muafaka sana kwa sababu;

1. Hali ilivyo sasa ikiendelea itafika mahali miji itashindwa kuhimili ongezeko la vijana wanaoingia mijini kila siku kutafuta maisha.

2. Kuwapanga kwenye maeneo maalumu ya biashara yatawawezesha wamamchinga kuwa na maeneo ya biasahra yanayoeleweka (kwa msemo wao kuwa na anwani) na hivyo kuwafanya waaminike hata kwa taasisi za kifedha wanapohitaji mikopo.

3. Kutaipanua miji na kuifanya kuwa na maeneo maalumu ya kibiashara, ambapo inatakuwa rahisi kwa wateja kwenda maeneo hayo kwa ajali ya kujipatia mahitaji yao.

4. Maeneo haya yakipangwa vyema yataiwezesha miji kuwa na ‘Kariakoo’ zao ndogo ndogo na hivyo kuchechemua zaidi biashara za wamamchanga na uchumi wa maeneo hayo.

Wito kwa wamachinga wote ni kutoa ushirikiano kwa mamlaka za miji ili shughuli ya kujipanga upya iwe yenye manufaa kwa pande zote.

Vijana Nguvu Kazi
Taifa Ni Vijana
Machinga Twende Kisasa Zaidi
 
Nipo huru

JF-Expert Member
Jul 20, 2021
924
1,000
Nawashangaa baadhi ya watu wanaopinga mpango wa serikali kwani hali ilivyo sasa sio nzuri inatishia amani na utulivu maana kundi moja linajiona ndio muhimu kuliko mengine hii sio sawa ni lazima kuwe na mpangilio kuruhusu wengine pia kurahisisha shughuli zao za utafutaji.
 
Kimla

JF-Expert Member
Jun 8, 2008
2,288
2,000

Huwezi kupambana na ongezeko la vijana kwa kuwapnga tu..Suala muhimu kwa serikali ni kupeleka huduma muhimu hadi vijijini ili watu wapate fursa kulekule..Mafano usambazaji wa umeme vijijini na maji kwenye centres vijijini inafanya vijana waanze kukaa kule.Kujenga hospital zinazotoa huduma na kupeleka internate hadi vijijini na centres mbalimbali inafanya watu kuanzisha fursa hukuko..mfano kunamiji midogomifogo kama katoro..busersere huku Chato zinaendelea kwa kasi kwa sbb ya fursa..Hoja ya magufuri kupelekq huduma kama hospital chato..musoma..inafanya watu wakarle kule badala ya kuja wote kujazana mwanza..kwa sbb watakuwa wanapata huduma za kibingwa karibu hukohuko
 
elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
10,234
2,000
Kwa mtindo huu swala la kuwapanga litakuwa ni la kudumu, kilasiku wamachinga wanaingia Dar na kufikia barabarani! Hivyo kazi ya serikali itakuwa ni ya kuwapanga wamachinga badala ya kanuni na sheria za Jiji na Miji kuifanya kazi hiyo.
 
Shoctopus

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
3,055
2,000
Nawashangaa baadhi ya watu wanaopinga mpango wa serikali kwani hali ilivyo sasa sio nzuri inatishia amani na utulivu maana kundi moja linajiona ndio muhimu kuliko mengine hii sio sawa ni lazima kuwe na mpangilio kuruhusu wengine pia kurahisisha shughuli zao za utafutaji.
Kwa kifupi kuongeza umachinga hakuongezi uzalishaji badala yake mnaongeza wasambazaji au 'middle men' (ambao wote ni walaji sio wazalishaji) na kuumiza wazalishaji hasa.
Bila kuzalisha 'educated labor force' kwa maana ya vijana wenye elimu ya kuwawezesha kuajiriwa ktk modern production industry; kwamfano viwanda vya electronics, vya magari kama kule Rwanda, tutabaki kuhubiri elimu ya ujasiriamali kama ndiyo muarobaini wa tatizo la unemployment bila mafanikio ya kweli.
Priority zetu lazima zibadilike kuwa 1. ELIMU 2. ELIMU na 3. ELIMU. Siyo magorofa, magorofa, magorofa na maflyower.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom