Hili la wafugaji na hifadhi zetu liangaliwe kwa mapana

Paragumu

JF-Expert Member
Dec 8, 2014
326
140
Kuna habari sasa ikiripotiwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari juu ya muendelezo wa migogoro ya wafugaji na maeneo yetu yaliyohifadhiwa hasa (Mapori ya Akiba GR's na Hifadhi za Taifa NP).

Yaweza kuwa sina uelewa mzuri juu ya mgogoro huu hivyo naweza kusaidiwa juu ya ninachokiona lakini nilichobaini pande zote zinaweza kuwa zimechangia kufika hapa tulipo.

Mosi yaweza kuwa uongozi wa hifadhi zetu ulilegalega sehemu wakati fulani kwa kuchukua rushwa na kuchangia kuingiza mifugo hifadhini kama wananchi wengi tunavyodai hasa wafugaji wenyewe.

Lakini kwa upande wa pili hasa wenye mifugo nadhani wanamatatizo zaidi kadri ya muono wangu. Kwann uingize mifugo sehemu isiyoruhusiwa je ni kweli kukosa malisho na maji!?kwann ufuge idadi usiyoweza kuimudu!sawa yawezekana ndio jadi yenyewe na ndio utajiri lakini kwa hili wafugaji tumepotoka. Mbaya zaidi mmekuwa na idadi kubwa ya mifugo kwa sasa msiyoimudu suluhisho tumeona kutumia vyombo vya habari kukuza tatizo.

Hivi inakuaje mfugaji una ng'ombe zaidi ya 700 alafu mifugo hiyo haikusaidii uonekane kweli binadamu tajiri,hatuchangii mapato yoyote ya maana katika halmashauri zetu au kodi maana mifugo hiyo kila kukicha iko hifadhini alafu bado tunataka umma utetee HAPANA tena NO!!tubadilike ni kweli tunataka malisho na maji lakini sisi wenyewe kupitia hivi vyama vyetu tuwe wakweli matope sasa yamezidi kwa hawa wahifadhi wetu narudia tena ni kweli yawezekana nao wamepotoka kuna wenye matatizo lakini wafugaji ni tatizo zaidi. Tuache kufuga kwa jadi kwa ninavyojua faida tunazopata kutokana na hifadhi zetu ni kubwa zaidi kuliko za ufugaji maana zimekaa ki-individual zaidi.

Nashauri sheria za kuhifadhi zisimamiwe kikamilifu mifugo itoke haraka kwa maana hata hiyo grace period iliyotolewa hadi June 15 nafahanu itafika na mifugo haitatoka kwenye hifadhi zetu. Nanyi watumishi wa hifadhi zetu badilikeni acheni rushwa simamieni hiyo mifugo itoke. Niko tayari kurekebishwa.

Nawasilisha,ni mm babu yenu PARAGUMU.
 
Back
Top Bottom