Hili la umeme limekaaje: kweli tumethubut, tumeweza na twasonga mbele

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,971
1,649
Huwa nabaki kulegea viungo vyote kasoro vile vinavyohusiana na utoaji wa uchafu mwilini. Yaani Tanzania ni ya ajabu sana. Mvua ikinyesha kidogo tu, umeme unakatika, jua likikomaa nayo taabu, umeme unakosekana.

Sasa hapa mtu unajiuliza iweje kila uchao tunadai hakuna umeme coz ukame umetamalaki, na pindi mvu inaponyesha tunakosa tena huo umeme? Mwenzenu huwa nachanganyikiwa kabisa. Au ndo tuseme mitambo yetu ya kuzalisha umeme sio friendly na mvua wala jua? Kama ni hivyo basi ni heri tungeishi katika nchi ambayo ni semi arid huenda hii shida inaweza kupungua.

Napata taabu sana kuishi TZ kama mtanzania!
 
Daa kweli umeme umekatika tena Mimi nilizania mheshimiwa ngeleji Leo angeakikisha umeme aukatiki na amefanya madudu Kama kawaida yake. Huyu waziri sasa ajiuzuru aingie mwingine atakaye tuakikishia siku Kama ya Leo umeme haukatiki. Ukikatika dakika kama kumi tuu uhakikishwe umerudi
 
Back
Top Bottom