Hili la Uingereza kupeleka waomba ukimbizi Rwanda ni muendelezo wa ukoloni

bnhai

JF-Expert Member
Jul 12, 2009
2,778
2,299
Nchi ya Rwanda imekubali kupokea waombaji wa ukimbizi waliongia nchini Uingereza kwa njia zisizo halali.

Watu hao wakifika Uingereza watakuwa wanapelekwa Rwanda wakati maombi yao yakifanyiwa kazi.

Rwanda watapokea fedha kwa ajili ya kazi hiyo.

Matarajio ni kwamba nchi hii itapokea wakimbizi toka nchi za Kiafrika, Afghanistan na Syria na sio wale wa Ukraine.

Pamoja na viashiria na tuhuma za ubaguzi kutoka nchi za magharibi, bado nchi zetu zinaendelea kukumbatia mikataba inayoendekeza ubaguzi.

Pamoja na kwamba chimbuko la wakimbizi ni tawala zetu, lakini ni muhimu masuala yanayofanana na haya yaendelee kubaki kwenye nchi husika.
 
sisi wakimbizi tulionao wana tutosha... tuna warundi, wanyarwanda, wakongo, wasomali... na raia mmoja mmoja walio omba hifadhi nchini kwetu...

uganda walichukua waafaghanistan... rwanda ikabeba walibya, kenya ikanyakua wasomali na waethiopia... tuendelee kuwahifadhi bila ubaguzi...
 
Duuuh, kwanini wa nchi hizo? Huu ni ubaguzi wa rangi na upimbi kukubali vitendo kama hivyo
Waafrika na waarabu pia wabaguzi wa Rangi tena hovyo

Ukraine wakimbizi wako mamilioni hakuna nchi hata moja ya kiafrika au kiarabu imeomba kuwa waende nchi zao watawahudumia kama nchi sio UNHCR

Waarabu na waafrika kikiwaka kila mmoja anawaza Ulaya na Marekani

Naunga mkono uamuzi wa uingereza na Rwanda

Waafrika na waarabu wapelekwe Rwanda maombi yao yakishughulikiwa
 
Waafrika na waarabu pia wabaguzi wa Rangi tena hovyo

Ukraine wakimbizi wako mamilioni hakuna nchi hata moja ya kiafrika au kiarabu iliuoombs kuwa waende nchi zao watawahudumia kama nchi sio UNHCR

Waarabu na waafrika kikiwaka kila mmoja anawaza Ulaya na Marekani

Naunga mkono uamuzi wa uingereza na Rwanda

Waafrika na waarabu wapelekwe Rwanda maombi yao yakishughulikiwa
Wao si ndiyo huleta hayo majanga..Kuna wakimbizi wa Ukraine zenji
 
Ila waingereza wabaguzi sana Hata hao waukraine wameanza kubaguliwa huko,kuingia UK mpaka uwe na mwenyeji ndio unapokelewa hatar sana na wengine wameanza kuwarubuni online wakitaka kusaidiwa na wanaume wakule na wao watoe msaada (ngono) hatar sana nasikia UK Tinder imelalamikiwa sana kwa unyanyasaji wakingono kwa WaUkraine.
 
Wale walikuwa watalii zimetoka tu wamekwama kuondoka

Lakini nchi kama nchi iwe Tanzania bara au Zanzibar hatujapeleka maombi kama nchi za Ulaya. Zinafanya kuwa tuleteeni wakimbizi wengine huku tutawatunza kwa gharama zetu sio za UNHCR
 
Acha waukraine wapigwe miti tena wapigwe Sana tu,wao si wanaona yule Comedian wao ni mzalendo,wacha waenjoy the show.
 
Nchi ya Rwanda imekubali kupokea waombaji wa ukimbizi waliongia nchini Uingereza kwa njia zisizo halali.

Watu hao wakifika Uingereza watakuwa wanapelekwa Rwanda wakati maombi yao yakifanyiwa kazi.

Rwanda watapokea fedha kwa ajili ya kazi hiyo.

Matarajio ni kwamba nchi hii itapokea wakimbizi toka nchi za Kiafrika, Afghanistan na Syria na sio wale wa Ukraine.

Pamoja na viashiria na tuhuma za ubaguzi kutoka nchi za magharibi, bado nchi zetu zinaendelea kukumbatia mikataba inayoendekeza ubaguzi.

Pamoja na kwamba chimbuko la wakimbizi ni tawala zetu, lakini ni muhimu masuala yanayofanana na haya yaendelee kubaki kwenye nchi husika.
UN walitaka kuwapeleka waisrael wakaishi Uganda, sijui kama tungebaki salama
 
Wale walikuwa watalii zimetoka tu wamekwama kuondoka

Lakini nchi kama nchi iwe Tanzania bara au Zanzibar hatujapeleka maombi kama nchi za Ulaya. Zinafanya kuwa tuleteeni wakimbizi wengine huku tutawatunza kwa gharama zetu sio za UNHCR
Wale wakimbizi,acha kuzungusha maneno,kwao Kuna vita
 
sasa huko Rwanda watakwenda kukaa hotelini au halafu vipi maombi yao ya ukimbizi yakikataliwa watabaki Rwanda au

Huyu Kagame tamaa yake ya kupata Drone na vimissile vya kuwavimbishia kifua majirani zake atajikuta anatuletea akina Osama jirani na East Africa
 
achene kutanga tanga na kuomba 'ukimbizi' kwenye manchi ya watu, tulieni majumbani kwenu ili kuepuka hizi kero za kepelekwa 'Rwand'
 
Ni kweli aiseee...
mimi niko buza na ninamiliki simu mbili halafu unipeleke Rwanda..

1649977079893.jpeg
 
Nchi ya Rwanda imekubali kupokea waombaji wa ukimbizi waliongia nchini Uingereza kwa njia zisizo halali.

Watu hao wakifika Uingereza watakuwa wanapelekwa Rwanda wakati maombi yao yakifanyiwa kazi.

Rwanda watapokea fedha kwa ajili ya kazi hiyo.

Matarajio ni kwamba nchi hii itapokea wakimbizi toka nchi za Kiafrika, Afghanistan na Syria na sio wale wa Ukraine.

Pamoja na viashiria na tuhuma za ubaguzi kutoka nchi za magharibi, bado nchi zetu zinaendelea kukumbatia mikataba inayoendekeza ubaguzi.

Pamoja na kwamba chimbuko la wakimbizi ni tawala zetu, lakini ni muhimu masuala yanayofanana na haya yaendelee kubaki kwenye nchi husika.
Kwann wasiwapeleke Saudi Arabia?
 
Hili Swala ukiliangalia kwa umakini, kagame ameona mbali sana, na amefanya mahesabu mpaka yakatimia.

Mimi naona kaangalia kuwa atapata faida nyingi kwa hili jambo;

1. Faida ya wakimbizi kwa nchi yeyote ni kuwa, wengi huwa vijana, hapo kuna nguvu kazi.
kumbuka nchi kama Marekani imepiga hatua kubwa baada ya kukaribisha watu wa nje.

2. Fedha atakazo pewa na Muingereza zita saidia nchi.

3. Huruma na Sifa kutoka mataifa mengine duniani kuwa Rwanda ni salama na nchi ya huruma.

Kwa hivyo hapo hajapoteza kitu, ila faida tu. Changamoto ni jinsi ya kuwa changanya hao watu kwenye maisha ya kirwanda.
 
Nchi ya Rwanda imekubali kupokea waombaji wa ukimbizi waliongia nchini Uingereza kwa njia zisizo halali.

Watu hao wakifika Uingereza watakuwa wanapelekwa Rwanda wakati maombi yao yakifanyiwa kazi.

Rwanda watapokea fedha kwa ajili ya kazi hiyo.

Matarajio ni kwamba nchi hii itapokea wakimbizi toka nchi za Kiafrika, Afghanistan na Syria na sio wale wa Ukraine.

Pamoja na viashiria na tuhuma za ubaguzi kutoka nchi za magharibi, bado nchi zetu zinaendelea kukumbatia mikataba inayoendekeza ubaguzi.

Pamoja na kwamba chimbuko la wakimbizi ni tawala zetu, lakini ni muhimu masuala yanayofanana na haya yaendelee kubaki kwenye nchi husika.
Afghanistan, Sudan, Syria na Pakistani wanakimbilia UK badala ya Saudia?
 
Back
Top Bottom