Hili la ugawaji wa dawa za minyoo Shule za Msingi limekaaje?

mwangalizi

JF-Expert Member
Apr 24, 2012
834
500
Kuna mazoezi yanapita katika shule za msingi ya kuwapa wanafunzi dawa za minyoo na sijui dawa gani nyingine, hii ya pili kwa maelezo ya wanafunzi ni chungu. Utoaji wa dawa hizi huambatana na chakula, imebidi leo waende na kuni pamoja na vyombo vya chakula.

Hizi dawa hazina mkono wa mabeberu kweli?

Je, zinatengenezwa na MSD?

Kwanini watoto wanatapika na kusinzia baada ya kutumia?

Hizi nadhani ni hatari kuliko barakoa.
 

Lukonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
246
500
Ni kweli kuwa Wizara ya Afya na Elimu huwa kuna wakati wanashirikiana katika kutoa dawa za kichocho na minyoo.

Dawa hizi zinapotolewa huitaji mhusika awe amepata chakula. Nadhani, ili kuhakiki hilo ndio maana wanatakiwa kupata chakula shuleni. La sivyo watoto wengi huishiwa nguvu na wengine huweza kupoteza fahamu kwa muda/wachache.

Walimu wakuu wote hupewa taarifa rasmi na taratibu za kufanya ili kufanikisha zoezi husika. Kama kuna wasiwasi wowote basi wasiliana na mwalimu mkuu wa shule anayosoma mwanao, ili kujua kama ni kitu tofauti na ni kwaajili ya nini?. Kwa shule nyingine wamefikia kutoa notisi kwa wazazi ili kukubali/consent au kukataa zoezi husika kabla ya kufanyika.

Kitaalamu ni jambo jema na kwa kuwa zinatolewa chini ya usimamizi wa wizara ya afya basi usalama na ubora utakuwa umezingatiwa.
 

imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
26,684
2,000
Ni mpango mzuri kama Watoto wanapimwa kwanza kabla ya kunyweshwa hizo dawa kwani sio Watoto wote wanakuwa wameathiriwa na minyoo
 

Mr Q

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
10,231
2,000
Ni mpango mzuri kama Watoto wanapimwa kwanza kabla ya kunyweshwa hizo dawa kwani sio Watoto wote wanakuwa wameathiriwa na minyoo
Unaweza kunitajia jina la hizo dawa? Miaka ya nyuma niliwahi kusikia kesi chache za vifo kwa watoto kwqsababu ya hizo dawa. Isije kuwa ni mpamgo wa muda mrefu wa kuua nguvu za watoto wetu hapo baadae aukuwasababishia matatizo ya kiafnya kwa siku zijazo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom