Hili la simu za Polisi ni aibu kwa Tanzania!

mzozaji

JF-Expert Member
Jul 28, 2010
255
13
Kwa kweli huwa nashindwa kabisa kuwaelewa viongozi wetu hasa waziri wa mambo ya ndani na Sayansi na Teknolojia kwa kukosekana kwa simu hasa za Polisi zilizo rahisi kukumbuka na maarufu duniani kama 999 , 991 na 112. Hivi kweli hawa wanategemea watu kukariri simu za akina Mwema na Kova na wengine? Je wageni ambao wanaingia nchini wakipata dharura itakuwaje? Je ukienda mkoani itakuwaje? (maana inabidi utafute simu ya Polisi wa huko).

Tatizo jingine kubwa ni kuwa simu hizo za binafsi ni laini moja, hivyo haziwezi kuwasiliana na watu wengi kwa wakati mmoja, tena tunaambiwa tuandike message, je message ikiingia baada ya saa moja na wewe huko kwenye dharura itakuwaje?

Ni rahisi sana kwa makampuni ya simu kuwaunganisha Polisi na namba hizi na kuwa na laini nyingi kwenye namba moja, lakini badala yake kila siku tunawaona kwenye magazeti wakitoa T-shirt za usalama barabarani kwa polisi na kupiga picha kupata umaarufu badala ya kutatua matatizo ya msingi kama haya na kuokoa maisha ya wanainchi wanaohitaji msaada wa haraka wakati dharura.

Wakati umefika kwa wahusika kuamka na kufanya kazi yao ili kuwasaidia wananchi wa kawaida kwani simu hizi zitawasaidia sana kupata msaada wa haraka popote bila ya kuanza kutafuta simu binafsi, kuandika message na kukariri.
 
kuna jamaa mmoja ni askari aliniambia hizo namba hawazitumii kwani kuna watu walikuwa wanapiga halagu hawaongea au wanahold line .... ndo maana ukiwaita kikosi cha fire wanachukua muda kutokana na hali hiyo maana sie wanadamu akili zetu zinatutosha wenyewe
 
Hta hivyo namba kama 112 inazidiwa maana ni hiyo moja tu na ikiwa inapigwa na watu wengi kwa pamoja inakuwa shida kupata line. Inatakiwa zitoke namba nyingi mfano 111, 112, 113, 114 115 nk
 
mi nafkiri imefika mahala police nao wangekuwa na call center inayokusanya taarifa na kuwa na system itakayo desplay namba ya anaepiga naamini sasaivi karibia kila mtumiaji wa simu amesajili hawatapokea simu za kijinga kama ilivo sasa
 
mi nafkiri imefika mahala police nao wangekuwa na call center inayokusanya taarifa na kuwa na system itakayo desplay namba ya anaepiga naamini sasaivi karibia kila mtumiaji wa simu amesajili hawatapokea simu za kijinga kama ilivo sasa atakaepiga kweli atakuwa ana report ya tukio kweli
 
jamani haya mawazo ya wanaJF yazingatiwe sana maana yanajenga hii nchi sana.....Aliyetoa wazo la kuwa Poisi wawe na call centre kweli ameshauri vizuri sana......Naunga mkono hoja yake kwa asilimia mia moja bila kuomba mwongozo wowote.....
 
Hta hivyo namba kama 112 inazidiwa maana ni hiyo moja tu na ikiwa inapigwa na watu wengi kwa pamoja inakuwa shida kupata line. Inatakiwa zitoke namba nyingi mfano 111, 112, 113, 114 115 nk
wanaposema piga 112 haina maana kuwa hiyo namba inapokea simu moja tu kwa wakati. Hiyo line ina uwezo wa kupokea calls nyingi kwa wakati mmoja lakini Tz inakuwa shida kwa sababu ya uzembe. Sehemu nying duniani namba ya imejensii ni 112 lakini inauwezo wa kupokea calls nyingi kwa wakati mmoja.
 
Umeniwahi
mi nafkiri imefika mahala police nao wangekuwa na call center inayokusanya taarifa na kuwa na system itakayo desplay namba ya anaepiga naamini sasaivi karibia kila mtumiaji wa simu amesajili hawatapokea simu za kijinga kama ilivo sasa atakaepiga kweli atakuwa ana report ya tukio kweli
 
kwani walitusajili ili iweje?all in allwanausalama wa taifa
wanatakiwa wawe kisasa zaidi naishangaa serikali badala ya kununua
vifaa vya kisasa kama hivyo inakazi ya kuzurura
kila pahali na kuongeza msururu wa mav8 shame upon you?

kuna jamaa mmoja ni askari aliniambia hizo namba hawazitumii kwani kuna watu walikuwa wanapiga halagu hawaongea au wanahold line .... ndo maana ukiwaita kikosi cha fire wanachukua muda kutokana na hali hiyo maana sie wanadamu akili zetu zinatutosha wenyewe
 
kuna jamaa mmoja ni askari aliniambia hizo namba hawazitumii kwani kuna watu walikuwa wanapiga halagu hawaongea au wanahold line .... ndo maana ukiwaita kikosi cha fire wanachukua muda kutokana na hali hiyo maana sie wanadamu akili zetu zinatutosha wenyewe

Mkuu watu watachezea hizo namba kama tuu hakuna udhibiti na watu hawapati adhabu kama wakikamatwa ili iwe mfano. Serikali haiwezi kukaa kuogopa watu kuvunja sheria kwa makusudi wakati ina vyombo vya dola kwa kazi hiyo. Sasa hivi tumesajili simu ili kuleta udhibiti wa mambo kama haya. Labda Polisi inakosa wasomi wa kufikiri.
 
WanaJF kwa kweli sijaona umuhimu wala msaada wa hizi namba 111,112 nimejaribu kuzipiga kwa simu tano tofauti hazipatikani!
 
Back
Top Bottom