mzozaji
JF-Expert Member
- Jul 28, 2010
- 255
- 13
Kwa kweli huwa nashindwa kabisa kuwaelewa viongozi wetu hasa waziri wa mambo ya ndani na Sayansi na Teknolojia kwa kukosekana kwa simu hasa za Polisi zilizo rahisi kukumbuka na maarufu duniani kama 999 , 991 na 112. Hivi kweli hawa wanategemea watu kukariri simu za akina Mwema na Kova na wengine? Je wageni ambao wanaingia nchini wakipata dharura itakuwaje? Je ukienda mkoani itakuwaje? (maana inabidi utafute simu ya Polisi wa huko).
Tatizo jingine kubwa ni kuwa simu hizo za binafsi ni laini moja, hivyo haziwezi kuwasiliana na watu wengi kwa wakati mmoja, tena tunaambiwa tuandike message, je message ikiingia baada ya saa moja na wewe huko kwenye dharura itakuwaje?
Ni rahisi sana kwa makampuni ya simu kuwaunganisha Polisi na namba hizi na kuwa na laini nyingi kwenye namba moja, lakini badala yake kila siku tunawaona kwenye magazeti wakitoa T-shirt za usalama barabarani kwa polisi na kupiga picha kupata umaarufu badala ya kutatua matatizo ya msingi kama haya na kuokoa maisha ya wanainchi wanaohitaji msaada wa haraka wakati dharura.
Wakati umefika kwa wahusika kuamka na kufanya kazi yao ili kuwasaidia wananchi wa kawaida kwani simu hizi zitawasaidia sana kupata msaada wa haraka popote bila ya kuanza kutafuta simu binafsi, kuandika message na kukariri.