Hili la rais Pombe: Kamata! Weka ndani!!

MWALLA

JF-Expert Member
Dec 12, 2006
16,952
10,500
Mkuu wa kaya tangazo lako la jana/juzi kuhusu sie vijana wazururaji tumelisikia ila nadhani bado hatujakusoma vizuri!!

Tukufahamishe tu ya kwamba..
Si kwamba sisi ni wavivu au hatupendi kazi la! Tangu enzi za mwalim mpaka enzi hizi zako wewe bado vijana tupo tena wengi huwezi kutumaliza kwa unaposema kamata weka ndani wakalimie huko hii haisaidi na haitakusadia wewe katika harakati zako.
Haitatui tatizo linalotukabili vijana. Kwanza hutaweza kutumaliza tumejaa vibaya mnoo.

Tunasema.. Tunataka kazi.. Tupe kazi uone kazi.

Tunataka kulima kama ulivoona kwamba kulima ndo suluhisho kwa vijana basi tupo tayari kupiga kazi.

Tutekelezee haya tu.
Tuandalie hayo mapori ili tuyageuze yawe mashamba.
Tutayalima na mazao yake ututafutie masoko.
Tupatie nyenzo za kutendea hiyo kazi ya kulima.
Tusisumbuliwe wakati wa kuuza mazao yetu.
Ututengenezee soko kuu kwa ajili ya mazao yetu tutakayovuna.

Ukifanikisha kutekeleza haya tutakuwa nyuma yako.

Tumeshaandaa list ya majina ya vijana wa nguvu kazi
Na tunaendelea kukusanya majina ya hao unaopanga kuwakamata. Badala ya kuwakamata tunakuomba utuambie ni lini zoezi linaanza ili usipate tabu ya kumaliza mafuta na kusumbua vijana wako wa POLICCM Wa kusubiria kuamrishwa piga Tuu.

Sisi tutakuja wenyeeewe na utatukuta mlangoni pako tunakusubiria.
Tupe mda na siku ipi tutie maguu ili utupangie wapi tukalianzishe gwaride la kilimo PILI.
maana kilimo kwanza imepoteza mwelekeo.

Wako katika maisha magumu.

Kijana mtanganyika

Ukifanya haya mkuu wa kaya utatuokoa vijana wako na janga hili la kujitakia kama huyu dogo aliyeamua kuolewa ili maisha yaende.
winnie ngalaba: eeeeeee mwenyezi mungu tunusuru, hivi kweli ni mtanzania huyu??
 
Duuh hii hatari .. sasa kama ni hivi wakuu wa wilaya na mikoa si wataweza hata kutuchukulia mademu zetu wakali halafu tukileta ngebe wanatuweka mahabusu? Hee hee kweli hii ndo kazi tuliyoahidiwa. Asante CCM kweli mnatukomesha
 
ImageUploadedByJamiiForums1458132914.983316.jpg
 
kijana unashinda kwenye pool table,kijiweni unakunywa viroba halafu unasema hakuna ajira wengi wao ndio walikuwa wanazungusha mikono wanataka mabadiliko
 
Mwambie pombe alete kazi a one kaz Co kubwabwaja jf
 
List ya majina ya vijana wazururaji IPO tayari. Mr pombe tupo tayari kuingia porini kupiga jembe. Tunakusubiria we tu
 
kijana unashinda kwenye pool table,kijiweni unakunywa viroba halafu unasema hakuna ajira wengi wao ndio walikuwa wanazungusha mikono wanataka mabadiliko
We Zombie Mwambie pombe vijana tupo tayari na viroba vyetu kupiga jembe
 
Hao wanaolima na kuuza mazao yao magufuli ndiyo kawatafutia soko la mazao yao au pori la kulima?mwisho hata wake zenu mtaomba mtafutiwe na muozwe
 
pombe na busara wapi na wapi?

Hahahaha.Kaka unajitaka??Mie nilipigwa mkwala wa nguvu nilipokosoa ile hotuba yake na kusema hakutumia na hekima wala busara kuongea vile.Duh nikaambiwa Mwenye busara na hekima ni Rais kwanza wengine ni baadaye.Sasa sijui ni akili zetu kuwa ona watawala ni Miungu!

Lakini Yawezekana ni Mungu maana alisema anataka kuwa Rais wa Malaika akifa,duh nikamfikiria huyu Mkatoliki Mwenzangu ambapo tunaamini kwamba Yesu Kristu ndiye Mfalme wa Mbinu na Dunia.Akaniacha hoi kama anaweza kujifananisha na Yesu basi Wabongo Tumekwisha.
 
Back
Top Bottom