Hili la 'Rais' kulihutubia Bunge tukiamini ni tukio 'Kubwa' halafu kuna Wabunge wanaanzisha Nyimbo na Pambio Kusifu nalo pia ni la Kikatiba?

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Leo nimekesha Kufanya Utafiti (Kuchunguza) ni nchi gani nyingine duniani ambayo Rais akiwa 'analihutubia' Bunge Waheshimiwa Wabunge katikati ya Hotuba yake 'humkatisha' kwa Kuanza kuruka 'Sarakasi' Vitini mwao, kuimba Nyimbo na Pambio za Kusifu na Kupongeza.

Je, hili la Wabunge 'Kuingilia' Hotuba ya Rais kwa (kuimba na Kusifu) kwa Bunge tukiamini kuwa ni tukio Kubwa na Adhimu katika Siasa za Tanzania (na hata Mataifa mengine) ni la 'Kikatiba' au labda Watanzania 'tumejibunia' tu Wenyewe ama kwa Ushamba au Upuuzi wetu uliozoeleka kwa miaka mingi?

Maajabu mengi yapo tu Tanzania Kwetu.
 
Ni fedheha na aibu!

Nimeangalia State of the Union kwa wenzetu huko ni issue serious sana! Mnapiga makofi mkiguswa sana mnasimama kwa makofi.
Nashukuru kwa Kunielewa Ndugu na Generalist nikiwa naeleweka na Watu 'Intelligent' kama Wewe hapa Jamiiforums huwa ninafurahi mno.

Hili tukio na huu Ushamba na Upuuzi unaofanywa na baadhi ya Wabunge wetu unaendelea tu 'Kutuchoresha' na hata 'Kutudharaulisha' Watanzania wote katika Mataifa ya Watu Wanaojitambua na Waliobarikiwa Maarifa ( Upeo ) mkubwa.
 
Kwani hao wazungu kila kitu lazima waanzishe wao ...acha utumwa wa fikra
Je, unajua maana na dhania nzima ya Mheshimiwa Rais 'Kulihutubia' Bunge na hilo Tukio 'Kuratibiwa' kuwa ni Muhimu ( Nyeti ) na la Kitaifa zaidi?

Je, umeshajiuliza ni kwanini Mheshimiwa Rais huwa hazungumzi na Bunge ( Mhimili ) mwingine mara kwa mara?

Je, umeshajiuliza ni kwanini Mheshimiwa Rais akipanga 'Kulihutubia' Bunge taratibu nyingi za 'Kiitifaki' hapo ( pale ) Bungeni nazo pia hubadilika?

Hauna Akili na acha Kunipotezea muda.
 
Kwani lile ni Bungee! Au ni kikao tu cha baadhi ya wajumbe wa ccm, na kinachofanyikia kwenye majengo ya bunge na kilichowapa hadhi akina Halima Mdee na wenzake ya kuwa wageni waalikwa?
 
Kiukweli ni jambo la aibu kwa press kubwa kama ile inayofatiliwa na watu wengi,nadhani ni aina ya wabunge tulionao,la tatu B apay attention anaelewa nini sasa
 
Hujui tu huyu Mara yake ya mwisho kabla ya hili, wabunge wenzake wa CCM walihitimisha kikao Cha rasimu ya katiba kwa kuimba na kucheza taarab....kwangu siyo ajabu ndiyo kuishi na kuona mengi
 
Leo nimekesha Kufanya Utafiti (Kuchunguza) ni nchi gani nyingine duniani ambayo Rais akiwa 'analihutubia' Bunge Waheshimiwa Wabunge katikati ya Hotuba yake 'humkatisha' kwa Kuanza kuruka 'Sarakasi' Vitini mwao, kuimba Nyimbo na Pambio za Kusifu na Kupongeza.

Je, hili la Wabunge 'Kuingilia' Hotuba ya Rais kwa (kuimba na Kusifu) kwa Bunge tukiamini kuwa ni tukio Kubwa na Adhimu katika Siasa za Tanzania (na hata Mataifa mengine) ni la 'Kikatiba' au labda Watanzania 'tumejibunia' tu Wenyewe ama kwa Ushamba au Upuuzi wetu uliozoeleka kwa miaka mingi?

Maajabu mengi yapo tu Tanzania Kwetu.
Au ndo kudemka huko?
 
Je, unajua maana na dhania nzima ya Mheshimiwa Rais 'Kulihutubia' Bunge na hilo Tukio 'Kuratibiwa' kuwa ni Muhimu ( Nyeti ) na la Kitaifa zaidi?

Je, umeshajiuliza ni kwanini Mheshimiwa Rais huwa hazungumzi na Bunge ( Mhimili ) mwingine mara kwa mara?

Je, umeshajiuliza ni kwanini Mheshimiwa Rais akipanga 'Kulihutubia' Bunge taratibu nyingi za 'Kiitifaki' hapo ( pale ) Bungeni nazo pia hubadilika?

Hauna Akili na acha Kunipotezea muda.
unaweza kuwa na akili sana wewe hadi kutoa mada nzuri na fikirishi,ila usipende kuonyesha wingi wa akili zako kwa kutukana watu unaodhani hawajakidhi matakwa yako ya mada yako....hii tabia yako ya matusi inakua kwa kasi
 
Leo nimekesha Kufanya Utafiti (Kuchunguza) ni nchi gani nyingine duniani ambayo Rais akiwa 'analihutubia' Bunge Waheshimiwa Wabunge katikati ya Hotuba yake 'humkatisha' kwa Kuanza kuruka 'Sarakasi' Vitini mwao, kuimba Nyimbo na Pambio za Kusifu na Kupongeza.

Je, hili la Wabunge 'Kuingilia' Hotuba ya Rais kwa (kuimba na Kusifu) kwa Bunge tukiamini kuwa ni tukio Kubwa na Adhimu katika Siasa za Tanzania (na hata Mataifa mengine) ni la 'Kikatiba' au labda Watanzania 'tumejibunia' tu Wenyewe ama kwa Ushamba au Upuuzi wetu uliozoeleka kwa miaka mingi?

Maajabu mengi yapo tu Tanzania Kwetu.
Mimi naona ni bora usingea dika huu uzi kuliko kujulikana kupitia uzi kama huu.
 
Back
Top Bottom