Albert Einstein
JF-Expert Member
- Aug 24, 2017
- 384
- 560
Taarifa ya Ikulu imeeleza kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Assad amemaliza kipindi chake cha miaka mitano kwenye nafasi hiyo. Lakini Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 (ambayo ndio sheria mama) haelezi hicho kinachoitwa "kipindi cha miaka mitano"
_
Katiba inaeleza kuwa CAG atakoma utumishi wake atakapotimiza umri wa miaka 60. Yani akifikisha umri wa miaka 60 anapumzika bila kujalisha ametumikia nafasi hiyo kwa muda gani. Iwe miezi miwili, miaka nane, au miaka kumi.
Ndio maana maCAG wote waliotangulia wameongoza ofisi hiyo kwa vipindi tofauti.
Mzee Mohamed Aboud aliongoza kwa miaka 27 tangu 1969 hadi 1996. Thomas Kiama akaongoza kwa miaka 9 tangu 1996 hadi 2005. Ludovick Utouh akaongoza kwa miaka 8 tangu 2006 hadi 2014. Sasa hii kauli ya kusema Assad amemaliza kipindi chake cha "miaka mitano" imetoka wapi?
Matakwa ya kikatiba ni umri wa miaka 60, unless aondolewe kwa kushindwa kutimiza majukumu yake. Na ikitokea hivyo Katiba imeweka utaratibu wa kumuondoa kwa kuunda tume.
Lakini taarifa ya Ikulu inaeleza Assad amemaliza kipindi chake cha miaka mitano. Je, hiki kipindi cha miaka mitano Ikulu wamekitoa wapi? Kwenye sheria ipi? Kama ipo sheria hiyo ipo ni batili maana inapingana na katiba.
Na kwa kawaida unapotokea mgogoro kati ya sheria na katiba, basi Katiba ndiyo inayoshika hatamu (When a state law conflicts with a Constitution, then constitution prevails because constitution rules supreme above all state laws).
_
Prof. Assad amezaliwa tarehe 06 October mwaka 1961. Kwa sasa ana umri wa miaka 58. Atafikisha umri wa miaka 60 October 06 mwaka 2021. Hivyo kwa mujibu wa KATIBA alipaswa kustaafu nafasi yake ya CAG akifikisha umri huo, na si kwa hiki kinachoitwa "miaka mitano". I stand to be corrected!
Zaidi soma:

Naomba nitumie mfano wa Rais.
1. Article 33(1) inasema There SHALL BE a president of United Republic. 'Shall be' ikikaa peke yake maana yake ni lazima Rais wa Jamhuri awepo.
2. Article 40(1) inasema President SHALL BE ELIGIBLE for re-election. Ukiona eligible imekaa mbele ya 'shall be', maana yake inampa haki Rais aliyepo madarakani kuchaguliwa kwa mara pili lakini siyo lazima achaguliwe kwa mara pili.
Sasa tukija kwa CAG, Public Audit Act inasema CAG shall be eligible for renewal, kitendo cha kuweka 'eligible' mbele ya 'shall be', maana yake CAG ana haki ukiteuliwa mara ya pili lakini siyo lazima achaguliwe.
AsanteniView attachment 1253281View attachment 1253282View attachment 1253283
Zaidi soma:
Suala la Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Vipengele kadhaa vya Kisheria
Nafahamu kwamba watu wengi wameanzisha threads wakijaribu kuelezea suala la CAG Kisheria! Hata hivyo, wengi wao kama sio wote walichofanya ni kurundika vifungu vya kisheria bila kutoa ufafanuzi! Mbaya zaidi, hawatoi ufafanuzi wa matumizi ya neno SHALL kwa mujibu wa sheria zetu! Nimelazimika...
www.jamiiforums.com