Hili la Pinda kuchangia Tshs10m kwa USDM limekaa vipi hili?

Fredy Azzah
WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) jana walimkaribisha chuoni kwao Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa bango lililoandikwa "Mtoto wa Mkulima, Tunalala Nje", kilio kilichomsukumu mtendaji huyo mkuu wa serikali kuahidi kukichangia Sh10 milioni kila mwaka kwenye ujenzi wa malazi yao hadi ukomo wa uongozi wake.

Huyu kweli ni "Mtoto wa Mkulima"? Jameni, idadi ya wakulima nchini ni 80% ya wananchi wote, je watoto wa wakulima wenye uwezo wa kutoa mchango kama huu nchini ni wangapi? Nasemea "watoto wa wakulima" wanao tegemea kilimo kujikimu, siyo watoto wa mafisadi. Au ndo muendelezo wa usanii? Watoto wa mafisadi wametoa ngapi? Kumbe Bongo hatuhitaji misaada, kama mtoto wa mkulima anatoa zote hizo msaada wa nini? Vinginevyo naona kama ni muendelezo wa filamu ya KISANII TU!
please kuwa mtoto wa mkulima siyo kuwa mkulima, hata Bill Gates anaweza kuwa mtoto wa mkulima. Mbona Mengi naye ni mtoto wa mkulima
 
alisema ana m25 benki, ukitoa na gharama za kampeni atakuwa amebaki na kama m2 au 3. sasa hapo nadhani hataweza kutekeleza hiyo ahadi.
 
Oh!ndugu yangu hakuana jipya hapo mbio za urais 2015 zimeshaanza !unashangaa nini?
 
Back
Top Bottom