Hili la Pinda kuchangia Tshs10m kwa USDM limekaa vipi hili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hili la Pinda kuchangia Tshs10m kwa USDM limekaa vipi hili?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ntemi Kazwile, Nov 27, 2010.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  Nov 27, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Jana Waziri Mkuu ameahidi kuchanga milion 10 kila mwaka mpaka ukomo wa utumishi wake ili pesa hizi zitumike kuwasaidia wanafunzi kutatua matatizo yao ya malazi, huyu ni Waziri Mkuu na mtendaji mkuu wa serikali!

  Jamani kama hii ndiyo aina ya viongozi tulio nao basi tuna kazi ya ziada, utafanya nini na milioni 10 kwenye ujenzi? Hivi kuna ulazima wowote wa Pinda kuingia mfukoni mwake kutatua kero za wananchi? Au anatuambia kuwa analipwa hela nyingi mno kiasi hiki?

  Kama ningekuwa Pinda, nisingeahidi chochote kwa wanafunzi, ningewaahidi kulichukua na kulifanyia kazi. Ningewatafuta wawekezaji wa ndani hasa hasa mashirika ya Pension na kuwaomba wawekeze kwenye ujenzi kwa ubia na UDSM, UDSM wana ardhi ya kutosha ambayo sasa inamezewa mate na walafi kwa ajiri ya kujenga shopping mall, which as good as it is it is the not the first priority for UDSM!

  Pinda jiuzuru kama kazi uliyopewa ni kubwa kuliko uwezo wako!

  Habari kamili soma hapa:http://www.mwananchi.co.tz/habari/-/6851-pinda-apokewa-kwa-bango-udsm
   
 2. shungurui

  shungurui JF-Expert Member

  #2
  Nov 27, 2010
  Joined: Sep 1, 2008
  Messages: 1,578
  Likes Received: 1,548
  Trophy Points: 280
  Ni usanii tu.
   
 3. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #3
  Nov 27, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Pinda hajui hata wajibu wake, ndo maana huamua kulia lia tu. Kama ameona kuna tatizo pale kwa nini asi adjust sera zilizopo? yeye anaacha kazi after five years sasa itakuwaje baada ya hapo? ila msimseme sana atalia na mimi sitaki kumuona msanii akilia maaana aibu
   
 4. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #4
  Nov 27, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Je tunahitaji waziri Mkuu msanii kweli? Inabidi ifike mahala wananchi tuchachamae kudhalilishwa namna hii na viongozi wetu
   
 5. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #5
  Nov 27, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Kama unataka kuwa radical kuhusu Pinda, ana matatizo mengi (si Waziri Mkuu halali kwa sababu si mbunge wa kuchaguliwa kwa mfano) lakini sioni vipi hili la kutoa linakuwa tatizo, ukiondoa swala la anapata wapi milioni kumi za kutoa spontaneously hivyo. Tusitake kuwavunja moyo hata wenye kutaka kuanza tu kutatua matatizo.

  Hili swala Pinda ana lawama zake za serikali kiujumla, kwamba walitakiwa kulijua na kulifanyia kazi hata kabla ya aibu hii.

  Lakini kwa jinsi alivyolihandle, siwezi kumlaumu. Amekubaali tatizo lipo, hajawapa Kiswahili cha "tutalishughulikia" ambacho kingeweza kuwa ndicho kitu rahisi kabisa kufanya, ameonyesha kujitoa yeye binafsi kwa kuchangia pesa zake, na kaleta chachu ya kutaka viongozi wenzake wachangie - ingawa sijui hata wanachochangia specifically ni nini, it may be too early to specify at this point anyway- lakini angalau mtu unaona huyu hili jambo limemuuma na kalianzia kwa vitendo.

  Na kutoa hivi hakuna maana kwamba mtu hawezi kwenda kutafuta fumbuzi nyingine zinazojikita katika sera zaidi na mipango kabambe ya kiuwekezaji (na wala hakumaanishi kwamba mipango hii itafanyika pia).

  Wasomi waliojaliwa neema kuchangia vyuo walivyosomea ni kitendo cha kawaida kabisa dunia nzima. Wahitimu wa UDSM waliofanikiwa kimaisha wako wapi? Kabla ya kuinyooshea vidole serikali, sisi wenyewe wananchi tuko tofauti vipi na serikali hii tunayotaka kuilaumu ?

  Pindakama mtu binafsi msemeni kwa mengine, siyo hili. Kama mnalaumu serikali kwa kuachia hili mpaka lifika hapa, of course lawama zipo kedekede na Pinda hawezi kuzkwepa.
   
 6. e

  emma 26 Senior Member

  #6
  Nov 27, 2010
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 108
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unataka we uchangie au umeona nini mtu anasaidi we unapinga ili waeendelee kuteseka au? Kila kitu ni kupinga unataka aijie ushauri kwako? Pinda ndo mzalendo 4memuuma mpaka akaamua atoe naye kutokana na mshahara wake we unataka atoe ahadi ambazo hazina maana?
   
 7. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #7
  Nov 27, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Pinda ana haki ya kuchangia kama Pinda. sioni tatizo. na hapa kachangia specifically kwa malazi. Hajachangia kuondoa tatizo la mikopo ambalo ni jikumu la serikali.
   
 8. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #8
  Nov 27, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nyie acheni upuuzi, tafuta chanzo cha tatizo then find a solution. Ni sawa una dependants wako kwenu then unawapa pesa kila siku it doesnt help wapeleke shule wasome wajitegemee. Je ukifa leo nani atawapa pesa tena>??? kama ungewapeleka shule wangeendelea kujitegemea. Hivyo jamaa kwa great thinkers wanaona hajatatua tatizo ila kalifunika tu tatizo bado liko pale pale
   
 9. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #9
  Nov 27, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kuona tatizo ni lazima uwe na macho ya ziada, wewe hamtofautiani na pinda naye ambaye tatizo aliiona vibaya na solution yake ikawa kama hiyo aliyotoa.
   
 10. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #10
  Nov 27, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Mazee hakuna aliyesema kutoa milioni kumi kila mwaka kunamzui mtu kutafuta permanent solution. Kama serikali inashindwa kupata permanent solution, isemeni kwa kukosa permanent solution, sio kumuandama Pinda kwa sababu kaleta challenge ya watu kuchangia vyuo walivyohitimu, kitu kinachofanyika dunia nzima.
   
 11. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #11
  Nov 27, 2010
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Fredy Azzah
  WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) jana walimkaribisha chuoni kwao Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa bango lililoandikwa "Mtoto wa Mkulima, Tunalala Nje", kilio kilichomsukumu mtendaji huyo mkuu wa serikali kuahidi kukichangia Sh10 milioni kila mwaka kwenye ujenzi wa malazi yao hadi ukomo wa uongozi wake.

  Huyu kweli ni "Mtoto wa Mkulima"? Jameni, idadi ya wakulima nchini ni 80% ya wananchi wote, je watoto wa wakulima wenye uwezo wa kutoa mchango kama huu nchini ni wangapi? Nasemea "watoto wa wakulima" wanao tegemea kilimo kujikimu, siyo watoto wa mafisadi. Au ndo muendelezo wa usanii? Watoto wa mafisadi wametoa ngapi? Kumbe Bongo hatuhitaji misaada, kama mtoto wa mkulima anatoa zote hizo msaada wa nini? Vinginevyo naona kama ni muendelezo wa filamu ya KISANII TU!
   
 12. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #12
  Nov 27, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ok Mimi siko tofauti na Pinda nakubali wewe hauko tofauti na nani au uko sawa na nani ? Kesho akichangia Yatima utasemaje? Before u criticise someone walk a mile on his shoes.

  Ebu sema serikali au Pinda inatakiwa kufanya nini kuhusu tatizo la Malazi UDSM.hii ni kazi ya Uongoi wa UDSM wenyewe. Kuna mipaka.
   
 13. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #13
  Nov 27, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Mazee, ingawa swali lako la msingi lina mantiki, na mimi nimeliuliza hapo juu, ulivyosema kwamba mtoto wa mkulima hawezi kupata hizo pesa nakushangaa. Kwanza kuna wakulima wa aina tofauti, pili, hata kama Pinda ni mtoto wa wakulima masikini, yeye si mkulima masikini, yeye ni PM kwa miaka kadhaa sasa.

  Kwa hiyo kusema mtoto wa mkulima hawezi kupata 10 million kila mwaka si sawa. Na hatujui Pinda atapata wapi hizi hela, si lazima zitoke mfukoni mwake, anaweza kuanzisha mfuko or something like that.

  Hizo hela mbona ni kujinyima extravagances za safari moja tu ? Wakiamua hawa wanajenga Chuo Kipya kabisa, achilia mbali kuboresha makazi ya hiki kilichopo.
   
 14. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #14
  Nov 27, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kaka hujui kuwa pinda ndio serikali? ndio maana tunasema its wrong for him to introduce such an idea.
   
 15. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #15
  Nov 27, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Inabidi tuulizane pia, wanaomshutumu Pinda wamechangia nini?
   
 16. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #16
  Nov 27, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Nimesema hapo juu Pinda ana lawama za serikali, lakini hilo halimaanishi kwamba kupromote philanthropy kushutumiwe.

  Moja ya sababu huduma zetu za jamii zinazorota ni kwamba watu wanategemea serikali kwa kila kitu, hawachangii, hawalipi kodi, wanasubiri serikali itoe tu.

  Sasa Pinda kaonyesha kuna sehemu ya watu binafsi kuchangia pia, mbali na serikali. Nothing wrong with that.

  Na hakusema kwa kutoa milioni kumi ananunua kutoulizwa maswali kuhusu suluhisho lingine la kimsingi zaidi.
   
 17. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #17
  Nov 27, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  UDSM wana serikali yao? Kaka pinda hakutakiwa kutoa pesa zake pale alichotakiwa ni kukaa na uongozi wa udsm na kujadili ili kupata permanent solution sasa milioni kumi inatosha nini kama sio kuongeza ufisadi tu. Zitamfikia nani? ni msaada ambao uko verge
   
 18. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #18
  Nov 27, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Angekaa na watu hao wangeweza hata kujenga majengo na sio mil 10 tu.
   
 19. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #19
  Nov 27, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Tatizo watu sometime tunakuwa na unreliastic expectation . No wonder hata CHADEMA ingekuwa ikulu watu kama Johnsecond wangekuwa ni kuponda tu .
   
 20. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #20
  Nov 27, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kazi ipoooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
   
Loading...