Lomunyaki Leteiva
Member
- Mar 7, 2014
- 47
- 6
Nianze kwa kusema nawapa Tano wabunge wa upinzani kwa utetezi wao wa wanyonge hasa sisi walimu. Ukweli tunanyanyaswa na mchango huo wa mwenge. Niwape historia fupi kuwa mimi ni mwalimu wa hapa MISUNGWI MWANZA. Mwaka jana nilikuwa mwl Mkuu lakini nilivuliwa madaraka kwa kukataa kutoa mchango wa mwenge. Ninao ushaidi nina barua ya kunivua madaraka na Sababu imeandikwa pia Kwenye log book imeandikwa. Hivyo nathubutu kusema mheshiwa Lukuvi na Wazirikuu wamelidanganya bunge kusema hawalazimishwi kutoa huo ni uongo kabisa. Watanzania wenzangu ukweli ndo huo mimi sasa na mwl wa kawaida mwenge umenitosa madaraka yangu. Mchango wenu tafadhari.