Hili la mh nyambari nyangwine kusoma arts halafu anaandika vitabu vya sayansi inakuja kweli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hili la mh nyambari nyangwine kusoma arts halafu anaandika vitabu vya sayansi inakuja kweli?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by CHASHA FARMING, Jun 14, 2011.

 1. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #1
  Jun 14, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  huyu mheshimiwa wa tarime ni mmoja kati ya watu wanao ua elimu hapa tanzania, haiwezakani asomee kiswahili halafu atunge hadi vitabu vya sayansi. Jamaa kwake hamna asicho weza na anaweza kuwa anaongoza kwa uchakachuaji hapa tanzania.
  Imebaki atoe dikishonary ya page tano tu.
   
 2. K

  Kiguu na njia Member

  #2
  Jun 14, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  watunzi wa vitabu walitumia jina la Nyambari Nyangwine for businez!!
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Jun 14, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Tanzania hata profesa wa Ngonjera na Michezo ya kuigiza akipenda tu na kujichagulia mwenyewe ni ruksa hata kuingia Muhimbili kutibu watu bila shida yoyote. Na hivyo ndio maana tiba za goti huhamishiwa kichwani.

  Mwacheni Nyangwine ajikusanyie fedha zilizozagaa bila wachukuaji kwenye soko la vitabu. Wala sitomshangaa akianza hata kuandika vitabu vya engineering huyo; ndio maana huko Mara wanaona heri tu kumdunda kijulikane kimoja kwa tabia ya kudandia dandia.

  Maadam yuko bungeni, huenda akaanza hata kundika vitabu vya sheria kwa kuwa tu hapo mjengoni kuna kutungwa sheria za nchi. Piga jaramba zaidi Nyangwine, wakamatishe hasa wasiojua tofauti kati ya taaluma moja na nyingine na jinsi inavyokua na uzito kwenye utunzi wa vitabu.
   
 4. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #4
  Jun 14, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Nazani kwake imebakia vitabu vya Dini tu Korohani pamoja na Bible
   
 5. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #5
  Jun 14, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,814
  Trophy Points: 280
  Nimemsikia huyu mheshimiwa akiongea jana bungeni hadi nikashika kichwa. Alikuwa anaongea hewa sasa sijui huko kuandika vitabu inakuwaje!! Yapo mengi ya kujiuliza
   
 6. msnajo

  msnajo JF-Expert Member

  #6
  Jun 14, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 2,458
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 180
  Jamaa hajawi kuandika kitabu chochote zaidi ya kucopy na kupaste kazi za watu wengine waliofanya tafiti zao. Kitaalamu "ana-plagiarize", which is very bad. Kuna watu nimewai kuwakuta wakidai huyo Mbunge ameiba kazi zao. Mfano ni lecturer mmoja alieko TU, ANAFUNDISHA MASOMO ya lugia. Binafsi rimfagili sana coz hata vitabu anavyocopy na kujifanya kaandika vinawafanya wanfz wengi wakariri mitihani badala kusoma na kuongeza ufahamu wao.. Lets ignore him and advice our student to study hard by exposing themselves into rearched materials rather than craming and memorizing of notes from Nyambari, "the plagiarizer"
   
 7. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #7
  Jun 14, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,919
  Likes Received: 451
  Trophy Points: 180
  wivu wa ke/
   
 8. k

  komredi ngosha JF-Expert Member

  #8
  Jun 15, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 381
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  ndo mchezo wake, ana copy na ku paste. Hata mimi nimewahi kusikia mwalimu wake wa sekondari alimlalamikia kwa kuchukua notes zake na kutungia kitabu bila idhini kisha akauza kwa jina lake. Yani jamaa ndo magamba pure, anajua kuchakachua kwa asilimia mia moja.!
   
 9. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #9
  Jun 15, 2011
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Anaitwa mwalimu Masatu, alikuwa mwalimu wa english language~1 mkwawa high school kabla haijageuzwa kuwa chuo kikuu.
   
 10. LEONELL

  LEONELL JF-Expert Member

  #10
  Apr 4, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 394
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  daa aisee laivuu...... haiwezekani mtu ukawa kila kitu ni wewe tuu......
   
 11. SHIEKA

  SHIEKA JF-Expert Member

  #11
  Apr 4, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 8,121
  Likes Received: 936
  Trophy Points: 280
  Ningekuelewa kama ungechukua kitabu cha sayansi alichoandika na kuonyesha mapungufu ndani ya kitabu hicho!
   
 12. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #12
  Apr 4, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280

  nani NYANGWINE???????
  nitarudi kumwaga ugali na mboga juu ya huyu bwana
   
 13. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #13
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,966
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Japo simfahamu,nahisi ni mbabaishaji.
   
 14. e

  emkey JF-Expert Member

  #14
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 728
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Inaandikwa QUR'AN na cyo korohani. uliza kabla hujaandika mkuu.
   
 15. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #15
  Apr 4, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mimi nina mawazo tofauti kidogo. Si nia yangu kumtetea kama atakuwa ameandika vitabu vya sayansi vyenye mapungufu, maana kwa bahati mbaya mimi sijaviona hata kimoja. Ila je, waandishi wa vitabu vya historia wao hawajakopi pahala? Kuna aliyekuwepo wakati huo? Au ni wangapi wamefanya utafiti hasa ktk haya mazingira yetu?

  Jamani, waandishi wengi mashuhuri hasa wa vitabu vya sayansi hutumia references kutoka kwenye vitabu na machapisho mbalimbali. Ikumbumbukwe kuwa, mbali na utafiti unaoweza kufanyika maabara, vitabu vingi vya sayansi huandikwa kwa kutumia vitabu vingine; na mara nyingi huweka orodha ya vitabu na machapisho mbalimbali ambavyo wametumia kama reference.

  Nitoe mfano, kuna kitabu maarufu kinachotumika ktk kufundishia somo la fiziolojia(physiology) ktk vyuo vikuu mbalimbali(kama sio vyote!) duniani kimeandikwa na jamaa anayeitwa Guyton na wenzake. Kitabu kizima ametumia references ya vitabu vingine, na kila mwisho wa chapter anaorodhesha hizo references.

  Ikumbukwe kwamba kuna masomo ya sayansi ktk level fulani huwezi kufanya utafiti wa kivitendo(laboratory) ili kuweza kuandika kitabu. Kwa mfano ktk level ya shuleni (let's say secondary/primary) hatutegemei kuona mwalimu anafanya disection ya binadamu ili mwanafunzi aweze kuwa kuelewa anatomy ya mwili wa binadamu. Ni lazima atatumia vitabu ambavyo hata hivyo kwa level yake vimerahisishwa na waandishi(akina nyangwine) ili aelewe basics za humani anatomy.

  Lakini pia turudi nyuma tujiulize, hao waandishi wa vitabu vya sayansi hapa kwetu wapo wapi? Kwa wale tuliosoma miaka ya 2000 na kurudi nyuma, tutakuwa tunamkumbuka Sabaya na vitabu vyake vya Biology Form I-IV. hata yeye alikuwa akitumia references,japokuwa alikuwa hasemi(pengine ni kutokana na mentality hii kwamba ataonekana amekopi)

  Kwangu mimi, sioni tofauti ikiwa Neville Meena leo hii ataingia maktaba akakusanya vitabu mbalimbali akavitumia kutengeneza kitabu kimoja kizuri cha sayansi na kinachoeleweka kwa kufundishia. Ili mradi tu yaliyomo yawe ya kweli na yenye kusimamia ukweli wa kisayansi, mimi nitampongeza.

  Hebu tujaribu kufunguka kidogo kiupeo, hivi waandishi wa vitabu ya sayansi vinavyotoka nje tuna uhakika gania na waandishi wake? Mimi naona tusimhukumu mtu kwa taaluma yake bali tuhukumu kazi yake, je ina ubora. Maana kwa mtazamo wangu, hata hao wanasayansi wetu, wengi wameshakimbia profesional zao na kuingia na siasa. Sasa anapojitokeza mtu na kutusaidia ktk hili mimi naona ni jambo jema. Mimi naona tumlaumu huyu jamaa ikiwa kazi yake sio ya kiwango kinachotakiwa, lakini tusibeze kwa taaluma yake hata anapokuwa amefanya kitu cha maana.
   
 16. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #16
  Apr 4, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mkuu hawa ndio waandishi wetu!
  Hawa ndio tunaowategemea kutuandikia vitabu vya sayansi.
   
 17. Omonto wa-hene

  Omonto wa-hene Senior Member

  #17
  Apr 4, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 179
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Yeah, huyu Mrimi kidoogo ameelekea kutoa utetezi kwa Nyangwine kwa kutumia 'fallacy of sympathy'. Umejitahidi sana ndugu! Lakini ukweli ni kwamba ujasiliamali wa Nyangwine umetengeneza kizazi (generation) inayohusudu sana summary kwa kila kitu. Hata makala katika magazeti vijana hawa wanataka summary tu! Kwa lugha nyingine wanafunzi wanapenda kujua majawabu tu katika masomo yao. Hawataki kujishughulisha kusoma kindakindaki kupata maarifa. Ujasiliamali wa Nyangwine umechangia pakubwa kuua 'studying culture' miongoni mwa wanafunzi wa Sekondari. Na hawa ndio wako Vyuo Vikuu sasa. Profesa au Mhadhiri anayezingatia kupata kazi za kisomi (Intellectual well written works) lazima atakumbana na ubatizo wa majina aina aina kutoka kwa wanafunzi wa kozi anayofundisha. Lakini yule anayefundisha kwa kutumia 'slides' za Power Point Presentation na kuwapa nakala wanafunzi wake ataitwa 'Mzungu'! Watanzania wa kizazi cha Nyangwine ndiyo wanahadaika na tungo kama 'maisha bora kwa kila Mtanzania' bila kuhangaika kujiuliza maisha haya yanakujaje ilihali tunajua si rahisi yakashushwa kama Mana! Hata kama anaweza kujitetea kuwa yeye anachokifanya ni kujitafutia riziki, bado riziki yake haina tofauti na riziki halali aipapatayo muuza mihadarati. Huo ndio ukweli!
   
 18. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #18
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,025
  Likes Received: 3,051
  Trophy Points: 280
  Tunahitaji kuwa wadadisi sana kabla ya kurukia mambo ambayo kidogo hatuyaelewi,huyu bwana amefanikiwa kuanzisha bookshop na kuwatafuta watu wanaoweza kucompose/kucompile kazi mbalimbali na kutengeneza vitabu

  Hapa ni kuventure kibiashara,kwa vile msera ashajulikana na jina lake kwenye vitabu linauza basi waandishi wanachonga na msera wanakubaliana kwa terms na kati ya terms hzo ni Nyambari kuweka jina lake pale,la duka lake na kwa sababu unatoka kwa kuuza kupitia jina lake unatakiwa pia kutoa kiasi cha pesa ya mauzo kwa mwenye kampuni ambaye ni Nyangwine

  Ndo hivyo tu,kwahyo msiendelee kufikiria kila kitabu chenye jina lake kaandika yeye.Hapana,yeye ni agent wa wengine nao wanauza kupitia yeye

  Kwahiyo mlikuwa mnaamini mtu anaweza kuandika katika masomo yote hivyo?na je hivyo vitabu mkiviangalia ndani ni kweli hamna majina mengine zaidi ya NN?
  Hapo Vipi??
   
 19. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #19
  Apr 4, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mkuu inawezekana sikuelewa maudhui ya mleta mada, au wewe hujelewa nilichokiandika. Nimekuwa wazi mapema kwamba sio nia yangu kumtetea huyu jamaa ikiwa kweli anatoa kazi ambazo ni sub-standard. Kama uandishi wake haukidhi mahitaji ya mitaala ya sasa, hilo hakuna mtu atakayemtetea.

  Ila mimi nilivyomwelewa mleta mada ni kwamba, NN hana haki ya kuandika vitabu vya sayansi kwa kuwa yeye ana taaluma ya mambo ya arts. Na ndio maana nikatoa mifano ya waandishi waliobobea na kuheshimika kazi zao ambao wote wametumia references ktk ku-compose na kuchapisha vitabu vyao. Ambao kwa hakika aina ya maudhui yao yanahitaji wataalamu wengine kufanya utafiti, kisha mwandishi akatumia machapisho yao kutoa kitabu ambacho hutumika katika elimu zetu za kila siku. Hili linajulikana dunia nzima, kwamba waandishi wengi mashuhuri mara kadhaa(nyingi) hutumia references kuandika kazi zao.

  Nasisitiza kuwa mimi nitakuwa wa mwisho kutetea mwandishi ambaye anatoa kazi zilizo sub-standard, ila napenda kama wewe ndugu yangu ungetoa mfano wa kitabu cha sayansi ambacho kinatumika kama kitabu cha kiada(sio ziada). Issue ya kutoa vitabu vya summary haipo hapa kwetu tu, ipo sehemu nyingi tu duniani. Mifano ni mingi. Kuna waandishi wengi tu mashuhuri wanatoa pocket books na tunavitumia sana tu kama quick references mashuleni, vyuoni na hata makazini kwetu. Sioni iweje ajabu NN kutoa vitabu vya aina hiyo.

  Nadhani tunapokuwa tunajadili kazi za hawa waandishi wetu, ni vema tukajaribu hata kutumia uzoefu wa waansishi wengine mashuhuri. Lakini pia mbona tunasahau kuwa kila edition mpya ya kitabu inapotoka ina kuwa imepunguzwa ukubwa ukilinganisha na ya mwanzo, nini tafsiri yake?

  Mfano wa lecturer kufundishia power point notes, hauna maana ya kubana uwezo wa mwanafunzi kutafiti vitu. Sina hakika kama ungekuwa mwalimu ungeweza vipi kufundisha kila kitu darasani(spoon feeding) ili umfanye mwanafuzi awe na uelewa mpana wa mambo ili usiitwe mzungu! Hebu tuwe realistic jamani.

  Kama NN ametoa vitabu ambavyo nichini ya kiwango, basi hata kama angekuwa mwanasayansi bado angetoa vitu vya namna hiyo hiyo. Hiyo ni hulka ya mtu haka angezaliwa wapi. Pengine hatujui lengo lake, labda ni ujasiriamali tu ili atengeneze hela kwa ajili ya kampeni ya 2015, sina hakika kama Mwera atagombea tena, kwa sababau kama ikitokea wakasimama wawili na Waitara lazima atatoka jasho. Na ushahidi upo, kama sikosei mwaka juzi/jana aligawa vitabu ktk shule kadhaa pale jimboni. Ila kiukweli bado mi naona ipo kila sababu ya kumpa moyo na ushauri ili aboreshe kazi zake badala ya kumbeza kwa kazi ambayo kwa miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia wasomi wetu wengi wakiipa kisogo.
   
 20. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #20
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 325
  Trophy Points: 180
  Jamani,NYANGWINE anafanya kazi ya ku publish kitabu,
  vitabu vilivyo vya sayansi ambavyo nimeona jina lake kama mwandsh,basi ni cover la nje tu,ila ukifungua ndan utakuta majina ya watunz wengne walio taka kujifcha chni ya jina la Nyangwine ili wauze zaidi!
  Sina hakika,sheria zinasemaje kuhusu hili!
   
Loading...