Hili la mbunge baraza la wawakilishi kuwadharau samaki wa ziwa Victoria lisipite pasipo mjadala. Linatoa picha mbaya

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
14,737
2,000
Kuna video moja fupi inazunguka mitandaoni anaonekana mbunge wa baraza la wawakilishi akiwaongelea kwa dharau samaki wa Ziwa Victoria. Anasema wao kwa maana ya watu wa visiwani hawana utamaduni wa kula samaki wa aina hiyo, kwamba isitokee mbegu zao zikawekwa kwenye bahari iliyo karibu na visiwa vya Unguja na Pemba!.

Hii ni kebehi mbovu sana, ina maana watu wa visiwani wanaoishi kule mikoa ya Ziwa Victoria hawali samaki wanaovuliwa kutoka kwenye maji yale!!?. Huku kujiona wa maana kunakojionyesha katika maneno ya yule mheshimiwa kunaleta taswira ya dharau kwa jamii pana ya Tanzania.

Waunguja na wapemba tumeishi nao tangu utoto mwetu, tukasoma nao vyuo vikuu na kufanya nao kazi. Na ninao uhakika vyakula vingi vinavyolisha visiwa hivyo na vile vya Comoro vinatoka huku Bara. Ni mazao yanayolimwa na wakulima wa mikoa ya Bara. Kama familia moja ya Kiembesamaki au Mwanakwerekwe inaweza kula wali unaotokana na mchele wa Mbeya lipi la hatari kwa afya ya familia hiyo iwapo itakula samaki wa maji baridi?.

Mbunge huyo wa baraza la wawakilishi kwa lugha ya kweli isiyo ya kuremba ni kwamba ameropoka, tena bila ya kujua madhara ya kauli yake. Alipaswa kutumia aina ya maneno yasiyoleta ukakasi kwa wavuvi wa Ziwa Victoria na wakazi mamilioni wanaoishi maeneo ya kanda ile. Wabunge kutoka Zanzibar wanaoingia ndani ya bunge la Jamhuri wanakula kila aina ya vyakula ambavyo baadhi vinalimwa na wakulima wa kanda ya Ziwa.

Wapo wazanzibari wengi tu waliokuzwa na Sato pamoja na Sangara kule kanda ya Ziwa, wanaujua utamu wa samaki hao. Hivyo mbunge yule atahadharishwe tu na waungwana kwamba kauli yake ndani ya kikao cha baraza la wawakilishi, inaweza kuwa imekera watu.
 
Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,260
2,000
Haitoi picha mbaya watu wamekula hela eti kuanzisha uvui wa sangara,sato na kambale ,watu mmezungukwa na bahari halafu unataka mabilioni upewe ili uanzishe ufugaji wa kambale,
Hivi mleta mada akili zenu ndio zilivyo ? sa nazidi kufaamu kwanini pale bungeni mnapiga makofi kwa kutumia meza kuyapongeza mazingahombwe kama haya.

Aafu mnataka tuendeleze muungano kwa akili hizi za kufuga kambale,na Zanzibar kiujumla hawali kambale wala sangala wala sato ,kiujumla kwa maana ukileta kipasenteji pengine wanaokula ni 0.0000001%.
Aafu Mmasai wa Zanzibar umwambie ale kambale.bora muungano ufe.
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
49,062

Kila sehemu ijitenge
 
robinson crusoe

JF-Expert Member
Oct 22, 2020
478
1,000

Hiyo unaiona kuna hoja ya kujadili kweli? Hujui tunatofautiana? Unachokula kwenu unataka nasi tule kwa sababu ya muungano? We vipi? Lete mambo ya maana hapa!
 
Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
14,737
2,000
Haitoi picha mbaya watu wamekula hela eti kuanzisha uvui wa sangara,sato na kambale ,watu mmezungukwa na bahari halafu unataka mabilioni upewe ili uanzishe ufugaji wa kambale,
Hivi mleta mada akili zenu ndio zilivyo ? sa nazidi kufaamu kwanini pale bungeni mnapiga makofi kwa kutumia meza kuyapongeza mazingahombwe kama haya.

Aafu mnataka tuendeleze muungano kwa akili hizi za kufuga kambale,na Zanzibar kiujumla hawali kambale wala sangala wala sato ,kiujumla kwa maana ukileta kipasenteji pengine wanaokula ni 0.0000001%.
Aafu Mmasai wa Zanzibar umwambie ale kambale.bora muungano ufe.
Duh hatari sana.
 
safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
8,485
2,000
Kama hamli tunachokula tumieni lugha ya staha, sio kuonyesha kwamba sisi tunaokula ni kama vile tunakula vitu vya ajabu.
Hiki ndo kinachowaharibu waunguja wengi(sio wpte)

Yani kukataa tamaduni za wengine with appreciation hawawezi,lazima kuna kauli wataziweka ambazo zinaonesha kudharau vya wenzao kana kwamba sio bora.

Yani wanaonesha kwamba wanakataa tamaduni za wenzao kwa sababu sio bora kama za kwao.

Tania hii ipo kwa wazenji wengi,ni tabia ya ajabu ambayo nimeiona sana ipo kule zanzibar.
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
42,543
2,000
Kuna video moja fupi inazunguka mitandaoni anaonekana mbunge wa baraza la wawakilishi akiwaongelea kwa dharau samaki wa Ziwa Victoria. Anasema wao kwa maana ya watu wa visiwani hawana utamaduni wa kula samaki wa aina hiyo, kwamba isitokee mbegu zao zikawekwa kwenye bahari iliyo karibu na visiwa vya Unguja na Pemba!.

Hii ni kebehi mbovu sana, ina maana watu wa visiwani wanaoishi kule mikoa ya Ziwa Victoria hawali samaki wanaovuliwa kutoka kwenye maji yale!!?. Huku kujiona wa maana kunakojionyesha katika maneno ya yule mheshimiwa kunaleta taswira ya dharau kwa jamii pana ya Tanzania.

Waunguja na wapemba tumeishi nao tangu utoto mwetu, tukasoma nao vyuo vikuu na kufanya nao kazi. Na ninao uhakika vyakula vingi vinavyolisha visiwa hivyo na vile vya Comoro vinatoka huku Bara. Ni mazao yanayolimwa na wakulima wa mikoa ya Bara. Kama familia moja ya Kiembesamaki au Mwanakwerekwe inaweza kula wali unaotokana na mchele wa Mbeya lipi la hatari kwa afya ya familia hiyo iwapo itakula samaki wa maji baridi?.

Mbunge huyo wa baraza la wawakilishi kwa lugha ya kweli isiyo ya kuremba ni kwamba ameropoka, tena bila ya kujua madhara ya kauli yake. Alipaswa kutumia aina ya maneno yasiyoleta ukakasi kwa wavuvi wa Ziwa Victoria na wakazi mamilioni wanaoishi maeneo ya kanda ile. Wabunge kutoka Zanzibar wanaoingia ndani ya bunge la Jamhuri wanakula kila aina ya vyakula ambavyo baadhi vinalimwa na wakulima wa kanda ya Ziwa.

Wapo wazanzibari wengi tu waliokuzwa na Sato pamoja na Sangara kule kanda ya Ziwa, wanaujua utamu wa samaki hao. Hivyo mbunge yule atahadharishwe tu na waungwana kwamba kauli yake ndani ya kikao cha baraza la wawakilishi, inaweza kuwa imekera watu.

Hayo maneno yake yamekukera kuliko njia waliyotumia ya mauaji kuingia madarakani? Kama wazenji wengi waliuwawa na kuachwa na vilema vya maisha, na uliona sawa, ni kipi kinakuimiza sasa kuhusu kejeli ya samaki?
 
Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,260
2,000
tafazalini misjitoe akili na kujifanya vipofu.hoja Mwakilishi anaejielewa ametoa au amepinga alieomba mabilioni kutaka kuanzisha eti ufugaji wa kambale ,jambo hilo halifanani na Zanzibar kama alitaka kupiga hela angetafuta mladi mwengine na sio huu ambao zahil shahil ni mbinu za kuchota hela halafu aludi aseme kamabale wote wamikufa kwa sababu arzi ya Zanzibar ina chunvichunvi, CCM mawazo yao siku zote ni namna gani watalaghai bungeni na kupata hela za bure.
Bajeti ya Zanzibar haihitaji kambale.
 
Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
14,737
2,000
Hayo maneno yake yamekukera kuliko njia waliyotumia ya mauaji kuingia madarakani? Kama wazenji wengi waliuwawa na kuachwa na vilema vya maisha, na uliona sawa, ni kipi kinakuimiza sasa kuhusu kejeli ya samaki?
Njia waliyotumia kuingia madarakani inawahusu wao kama wao. Wakiwa sehemu ya Muungano nimewakumbusha tu kuhusu mbunge wao kupima kauli haswa zenye kugusa maisha ya kila siku ya wengi.
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
42,543
2,000
Njia waliyotumia kuingia madarakani inawahusu wao kama wao. Wakiwa sehemu ya Muungano nimewakumbusha tu kuhusu mbunge wao kupima kauli haswa zenye kugusa maisha ya kila siku ya wengi.

Kama aliingia madarakani kwa mauaji kufanyika, huo muungano na hao samaki wana maana kuliko uhai wa watu? Kwahiyo ww unaona samaki wana maana sana mpaka umelaani hiyo kauli, huku ulikalia kimya mauaji!?
 
Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
14,737
2,000
Hiki ndo kinachowaharibu waunguja wengi(sio wpte)

Yani kukataa tamaduni za wengine with appreciation hawawezi,lazima kuna kauli wataziweka ambazo zinaonesha kudharau vya wenzao kana kwamba sio bora.

Yani wanaonesha kwamba wanakataa tamaduni za wenzao kwa sababu sio bora kama za kwao.

Tania hii ipo kwa wazenji wengi,ni tabia ya ajabu ambayo nimeiona sana ipo kule zanzibar.
Yah huwa wanadharau za moja kwa moja, wanashindwa kujishusha. Ni sawa na yule mzee mmoja wa kipemba anaonekana kumchimba mkwara IGP Sirro wakati yeye ni serikali.

Yupo yule mbunge mwingine aliyemkejeli Gwajima akisema kama anafufua basi aende akafufue watu muhimu. Halafu ni swali anauliza bungeni!!, hajui kuwa kwa swali lile amewakera waumini wa Gwajima ambao baadhi yao wapo pale pale Dodoma anapoishi.
 
Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
14,737
2,000
Kama aliingia madarakani kwa mauaji kufanyika, huo muungano na hao samaki wana maana kuliko uhai wa watu? Kwahiyo ww unaona samaki wana maana sana mpaka umelaani hiyo kauli, huku ulikalia kimya mauaji!?
Mkuu unaposema kaingia madarakani kwa mauaji ni kauli ya jumla. Vipi kuhusu zile vurugu wanazozifanya wananchi kwa wanajeshi na mapolisi?.

Ni kukumbushana tu kwamba kauli moja inaweza kuleta chuki ya kitaifa.
 
safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
8,485
2,000
Kama aliingia madarakani kwa mauaji kufanyika, huo muungano na hao samaki wana maana kuliko uhai wa watu? Kwahiyo ww unaona samaki wana maana sana mpaka umelaani hiyo kauli, huku ulikalia kimya mauaji!?
Kosa moja halihalalishi kufanyika kwa kosa jingine.

Watu walishapiga kelele humu kuhusu hayo mauwaji tafuta nyizi zipo.

Pia watu hao hao acha wapige kelele juu ya kauli za kibaguzi zinazotolewa na hao watu.

Haina maana kuwa wafanye watakavyo tu ati kwa kuwa walifanyiwa jambo fulani,ubinadamu uko pale pale.

Ukifika wakati wa kupinga uonevu wanaofanyiwa tutapinga uonevu huo,ikifika wakati wa kuwasahihisha tutawasahihisha.

Haina maana kuwa ukifanyiwa jambo dulani kwa wakati fulani endi ndo upo huru kufanya kila jambo la kebehi kwa wenzio.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom