Hili la Manispaa ya Ilala kumiliki magari ya kubebea nyama na kusambaza mabuchani ni kuibana sekta binafsi

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,754
139,560
Kama Serikali itataka kufanya shughuli zote hadi za kubeba nyama kutoka machinjio mpya ya Vingunguti na kusambaza mabuchani basi sekta binafsi inaweza kudhoofu sana.

Nilimsikia Naibu Waziri wa mifugo mh Gekui akiipongeza Manispaa ya Ilala kwa ubunifu huo wa kusafirisha nyama.

Ni vema Serikali ikajikita kwenye kuchochea ukuaji wa sekta binafsi na ishiriki kwenye miradi mikubwa tu siyo hii ya kumiliki viholiholi vya kubebea nyama machinjioni.

Maendeleo hayana vyama!
 
Hata sijui huwa wanawaza nini huku wanakwambia wanakuza sekta binafsi , lakini kwa matendo unaona kabisa kuwa wanaiua!!na ndio maana kila siku ajira zinazidi kuwa ngumu kutokana na mambo kama haya!!na shida ni kuwa watakwambia eti sekta binafsi hawajazuiwa nao kufanya , ila kanuni zitakazowekwa lazima sekta binafsi tu atajitoa!!huko tulishatoka miaka mingi baada ya kushindikana lakini hawataki kuliona hilo!!na kwakuwa hakuna msemaji.

Mfano juzi nilikuta mzozo kati ya watu wa bodi ya nyama na wenye mabucha, wanapigwa faini kwa kosa la kutumia magogo kukatia nyama, badala yake wanatakiwa kutumia mashine au magogo ya plastic, wakawauliza hebu tupelekeni wanapoyauza hayo magogo tukanunue, kwani wengine mashine zipo ila umeme ni tatizo kwani unakatika mala kwa mala, jibu wanalopewa sio jukumu letu kujua hayo magogo ya plastic utayapata wapi bali sheria ndio inaelekeza hivyo!!
 
Waliokua wanafanya hiyo kazi kabla ya manispaa kuanza walikua wanalitosheleza soko?

Na je walikua wanakidhi vigezo na masharti ya hiyo kazi? Je, wapo wafanya biashara hiyo walioathirika na kulalamika kupoteza kazi?
 
Hata sijui huwa wanawaza nini huku wanakwambia wanakuza sekta binafsi , lakini kwa matendo unaona kabisa kuwa wanaiua!!na ndio maana kila siku ajira zinazidi kuwa ngumu kutokana na mambo kama haya!!na shida ni kuwa watakwambia eti sekta binafsi hawajazuiwa nao kufanya..
Hahahhaahhaaahahahhaaha baada ya miaka mnne iliobaki kisheria hebutue wazalendo kuniongezea 5 yes
 
Waliokua wanafanya hiyo kazi kabla ya manispaa kuanza walikua wanalitosheleza soko?
Na je walikua wanakidhi vigezo na masharti ya hiyo kazi? Je wapo wafanya biashara hiyo walioathirika na kulalamika kupoteza kazi?
Khaaa! Kwa hiyo wewe huoni kuwa Kuna watu hapo wamepoteza ajira! Shida kweli
 
Khaaa! Kwa hiyo wewe huoni kuwa Kuna watu hapo wamepoteza ajira! Shida kweli
Sijaona mkuu, kwani hayo magari ya manispaa yanatosheleza ilala nzima?
Au wale waliokua wanasambaza nyama walikua wanatosheleza uhitaji wa soko?

Tunaweza kuwa hapa tunatoa hukumu kwa mambo tusiyoyajua ukweli wake, tena usikute pamoja na hayo makundi mawili kuwepo kuna watu bado hawapati hiyo huduma
 
Pale serikali inapotaka kufanya biashara

Ova
Serikali itafanya kazi ya kuhudumia wananchi wake popote
Kama hawapati huduma stahiki au kama huduma wanazopata haziwatoshelezi

Sidhani kama watoa huduma walikuepo wa kutosha tena wanalipwa kodi kwa manispaa, hiyo manispaa ingeingia front kutoa hiyo huduma
 
Kama Serikali itataka kufanya shughuli zote hadi za kubeba nyama kutoka machinjio mpya ya Vingunguti na kusambaza mabuchani basi sekta binafsi inaweza kudhoofu sana.....
Nakuuliza kila siku hizi mada unazoanzisha unakua umetumwa kutuchora?

Kampuni za kwenye construction industry zimekufa nyingi hizi za wazawa, unajua tatizo ni nini? Anzisha na mada hiyo pia upeleke majibu walikokutuma maana ni mada zifananazo.
 
Hata sijui huwa wanawaza nini huku wanakwambia wanakuza sekta binafsi , lakini kwa matendo unaona kabisa kuwa wanaiua!!na ndio maana kila siku ajira zinazidi kuwa ngumu kutokana na mambo kama haya!!na shida ni kuwa watakwambia eti sekta binafsi hawajazuiwa nao kufanya , ila kanuni zitakazowekwa lazima sekta binafsi tu atajitoa!!huko tulishatoka miaka mingi baada ya kushindikana lakini hawataki kuliona hilo!!na kwakuwa hakuna msemaji...
Hatimae mapambio yanatoa mrejesho aka backfire
 
Serikali itafanya kazi ya kuhudumia wananchi wake popote
Kama hawapati huduma stahiki au kama huduma wanazopata haziwatoshelezi

Sidhani kama watoa huduma walikuepo wa kutosha tena wanalipwa kodi kwa manispaa, hiyo manispaa ingeingia front kutoa hiyo huduma
Ktm vp wata supply nayo

Ova
 
Waliokua wanafanya hiyo kazi kabla ya manispaa kuanza walikua wanalitosheleza soko?

Na je walikua wanakidhi vigezo na masharti ya hiyo kazi? Je, wapo wafanya biashara hiyo walioathirika na kulalamika kupoteza kazi?
Wewe kazi yako kubwa iliyokuleta duniani ni kukata vitunguu na kiuno Tu no Bora utulie Tu maana maisha yenyewe huyajui
 
Hata sijui huwa wanawaza nini huku wanakwambia wanakuza sekta binafsi , lakini kwa matendo unaona kabisa kuwa wanaiua!!na ndio maana kila siku ajira zinazidi kuwa ngumu kutokana na mambo kama haya
Ila nchi hii bana.

Wakitoka bodi ya nyama anakuja AFISA AFYA,

Akitoka Afisa Afya anakuja TMDA.

Hapo hujatembelewa na wakala wa vipimo, TRA et al.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom