Hili la Manispaa ya Ilala kumiliki magari ya kubebea nyama na kusambaza mabuchani ni kuibana sekta binafsi

Hali ya magari Mengi ya kubeba nyama yalikuwa hali mbaya na hayuko kwenye viwango ngoja halmashauri wawaonyeshe mfano
Pia bucha watu haziko kwenye standard mshauri wafanyabiadhara watembelee bucha za hapo mombada Kenya makuu nadhani haizidi hata elfu 20 kwenda waone bucha za wenzetu zilivyo hizo za kwetu za kukatia nyama kwenye gogo chafu lisilooga miaka mmmmmmmm
 
Kama Serikali itataka kufanya shughuli zote hadi za kubeba nyama kutoka machinjio mpya ya Vingunguti na kusambaza mabuchani basi sekta binafsi inaweza kudhoofu sana....
Vyanzo vingi vya mapato vya halmashauri vimechukuliwa na serikali kuu. Hivyo inalazimu kubuni vyanzo vingine
 
Ubunifu mzuri, Mimi sioni shida Kama huduma zinaongezeka na biashara ni ushindani Ili huduma ziwe Bora, na magari ya taka nayo wanunue Ila wapite Kila siku siyo mtu akae na uchafu mwezi.
 
Kwani halmashauri safari hii na wenyewe watatakiwa wapeleke gawio, maana sasa serikali badala ya kutunga sera, kukusanya kodi na kutoa hudumu inajikuta inafanya hadi biashara ndogo ndogo za mama ntilie. Juzi juzi watu walikuwa wanauliza kwa nini kampuni za serikali kama TPDC na STAMICO kwa miaka mingi zimeshindwa kuvumbua na kuendesha uchimbaji wa madini, gesi na mafuta hadi mabeberu ndo waje wafanye na kutuachia mashimo na ile asilimia 4...
 
Back
Top Bottom