Hili la makampuni ya simu kulazimishwa kujiunga na soko la mitaji limekaaje?

hapo ndipo ninapochoka mimi, ina maana serikali haina mamlaka ya ku-access financial info za kampuni flani kiukamilifu mpaka hiyo kampuni iende dse? sasa kwa nini hayo makampuni waliyaruhusu yaanze kazi wakati hawana uhakika wa namna ya kujua hizo info!!!!???
 
hapo ndipo ninapochoka mimi, ina maana serikali haina mamlaka ya ku-access financial info za kampuni flani kiukamilifu mpaka hiyo kampuni iende dse? sasa kwa nini hayo makampuni waliyaruhusu yaanze kazi wakati hawana uhakika wa namna ya kujua hizo info!!!!???
Tatizo mmechagua viongozi vilaza.
 
Kwa hiyo hamtaki..Inamaana hatak gesi na mafut hamtaki waje waambiwe siku moja wawauzie share watanzania?? Kweli wabongo kwa kutetea wakoloni wako mbele kwa maslahi yao binafsi?Kwanini kampuni zinatumia kila njia kukataa wazo hili zuri ambalo nchi nyingine wanafanya?
Samahani hivi DSE ikianguka kama ilivyotokea kule USA hayo makampuni serikali na watanzania watafidiwa au?
 
Huwezi kuzuia uhuni unaondelea kwenye hayo makampuni ya simu hapa Tanzania kama hawakuweka kila kitu wazi, na namna bora ya kuaanika kila kitu ni kujisajili soko la hisa. Vingenevyo hela zitaishia Panama.

Pia kumbuka sheria iko wazi, wanatakiwa kuwa kwenye soko la hisa tatizo huko nyuma hawa mabwana walikuwa wanafanya watakavyo kwenye shamba la bibi.
 
Mjadala mzuri sana huu umetufumbua macho akina sisi . Niwapongezeni nyote Kwa elimu mnatupatia humu. Ila nawasihi punguzeni jazba na ujuaji ili tufaidie wenzenu kwani Sisi sote ni wamoja. Mbarikiwe sana wandugu. Mungu ibariki Tanzania
 
watanzania wangapi watanunua hizo hisa kwa pesa ipi kama sio vigogo wachache ambao na wao watatuajiri sie makabwela katika biashara zao.......tuwe wapole si kila jambo likisemwa kuhusu watanzania litakugusa kwa jinsi lilivyo.......TRA ni mamlaka huru isitegemee DSE ikusanye mapato kulingana na faida inayopatikana nafikiri ndio utaratibu.....mfano kwenye madini mpaka leo nini kimeendelea
 
Mkuu asante kwa maoni mazuri.
Lakini essence ya Capital Markets ni kuraise capital na si monitoring company financial performance.
Hapo ina maana kama kuna ulazima kisheria kulist, basi vile vile kuna idara ya serikali ambayo ina udhaifu katika utendaji wake wa kufuatilia mahesabu ya kampuni binafsi.

Na kwa mtaji huo, basi kila kampuni binafsi itakwepaje utaratibu huo?

Hawajalazimishwa na capital market, ni serikali ndiyo imetunga sheria hiyo so capital market authority ni mtekelezaji. Mbona kuagiza mafuta nje mmewekewa Maharti na hamjalalamika.This is to do with controls
 
Kosa kubwa linalofanywa hapa ni kudhani kuwa kununua hisa maana yake ni kupata faida.

Kununua hisa maana yake ni kuingia kwenye biashara. Biashara yoyote ina faida au hasara. Kwahiyo, kusema kuwa kuuza hisa ni ili watu wapate faida sio kauli kamilifu.

Nchini India pia ipo sheria inayolazimisha makampuni kujisajili kwenye soko la hisa.

Kwa kweli sina uhakika kama no utaratibu mzuri au mbaya, ila kwa jinsi tulivyofanya nadhani ingefaa zaidi iwapo tungetoa muda wa kutosha kwa makampuni kujiandaa na wananchi kuelimishwa. Muda kama miezi 18-24 ungeweza kufaa kabla ya utekelezaji wa agizo kuanza.
 
Mkuu nilitaka nikujibu kirefu kidogo hoja yako lakini naona sina muda wa kutosha kukuelimisha namna biashara zinavyoendeshwa kimafanikio kidunia na jinsi ambavyo udhibiti unaopita kiasi wa serikali kwa biashara una madhara hasi siyo chanya kwa jamii. Ushauri tu, jaribu kujisomea kujifunza namna ambavyo biashara zinaendeshwa kwenye nchi ambazo biashara hata ya kigeni hailazimishwi kuuza hisa publicly na bado wananchi wa hizo nchi wamenufaika kupitia ajira na kodi zinazolipwa na hizo biashara. Bado upo mwaka 1947 kifikra Mkuu.
Mkuu ulisoma shule ya wapi ww. Hakuna uchumi wowote katika nchi yoyote ambao ambao hausimamiwi na serikali. Biashara lazima isimamiwe na serikali.
Nchi nyingi zina mpaka sheria ya re-investment policy yaan kampuni ikipata faida baada ya kodi hairuhusiwi kuondoka na hela yote bali kuna percent ambayo lazima wawekeze tena ndan ya nchi hiyo hiyo.

Zingine zina sheria inaitwa wearth distribution yaan kampuni inatakiwa ku sub contract kazi zake zingine kwa kampuni za ndan ya nchi ili kusaidia Wananchi na nchi kwa ujumla kufaidika na utajiri mkubwa wa hizo kampuni.

Serikali ya Tanzania inachofanya kwa makampun makubwa ya nje ni sahihi na ni kama vile wamechelewa sana. Faida yote hii kubwa ya makampun haya haiwezi yote kupelekwa nje. Ni unyonyaji mkubwa. Huwezi kuwa unavuna tu bila kuwekeza kidogo. Watakuwa wanatuachia umaskin mkubwa. Ni lazima kiasi fulan cha faida kibaki nchin kwa watanzania through stocks. Watanzania waweze kumiliki kiasi fulan cha hisa.
Kuna nchi nyingi tu zina mpaka limiti kuwa huruhusiwi kumiliki kampuni kwa zaid ya asilimia fulan let say 60%.

Hebu Soma tena vitabu mbali mbali na hata jaribu ku peruzi sheria za nchi mbali mbali kuhusu foreign investment policy. Utajifunza kitu. Dunia iko mbele sana. Umeachwa nyuma sana mkuu.

Hii kitu ina faida nyingi sana. Nikianza kukutajia apa ntaandika mpaka bass. Hii ndo serikali inayofanya kazi. Hii ndo serikali ya watanzania WAZALENDO. Wanawasaidia watanzania ili miaka mitatu minne ijayo waje wawe na maisha reasonable wao wanaita uchumi wa kati.

Haya mambo yanapaswa kusimamiwa na watu jasili kama akina Magufuli.

Watanzania tuamke sasa. Tuache kulala. Magufuli anatuamsha. Mpaka wakenya wameanza kuwa na wasiwasi kuwa miaka minne au mitano ijayo tunaweza kuwapita kirahisi sana.

We mtanzania amka. Fungua akili acha ujinga. Tambua fursa.
 
Kuyalazimisha makampuni ya simu kuwa listed kwenye Dar es Salaam stock excharge kuna faida kubwa sana
Zifuatazo ni faida hizo
Moja, ni ukweli usiopingika kuwa kumekuwepo na tetesi za muda mrefu sana kuwa kampuni hizi zimekuwa zikificha hesabu zake
Kwa lengo la kukwepa kulipa kodi stahiki
Hivyo wakiwa listed DSE
Itawalazimu makampuni haya kuweka wazi mahesabu yao yote, ili shareholders waweze kujua maendeleo ya kampuni hizo
Kwani nao watakuwa ni sehemu ya umiliki
Hivyo itasaidia nchi kupata mapato stahiki katika kodi
Mbili, itanufaisha umma wa Watanzania kuwa sehemu ya umiliki wa makampuni haya
Hasa ukizingatia kuwa yamekuwa yakipata faida kubwa sana
Kwa hiyo sehemu ya faida hiyo itabaki humu humu ndani
Hizo ni sababu mojawapo inayoelekea serikali kuwalazimisha wawe listed DSE
Hata makampuni ya madini nayo yanapaswa yawe listed DSE
Kupynguza mwaya wa kukwepa kulipa kodi stahiki
Jibu swali faida sawa swali linasema je kuna ulazima je sheria ilala zimeisha makampuni binafsi kujiunga kwenye soko la hisa
 
kuwalazimisha makampuni yajiunge DSE sio uamuzi sahihi kabisa..
watu wanajificha kwenye mgongo wa maslahi ya wananchi uongo mtupu...
unakuta kipande cha hisa cha chini kabisa kinauzwa labda 520 halafu sharti ununue vipande 1000..maskini gani ana uwezo huo??
haya suala la eti ..haya makampuni yana manipulate financial statements zao ili kulipa kukwepa ..nalo di hoja yenye mashiko TRA wameshindwa kubaini hilo iweje DSE waweze??
hata ivo mchezo huu tz bado hatuwezi..makampuni pale pale U.K yanafanya ujanja huo sembuse huku tz..

DSE.Bado changa sana na bado technolojia iko chini sana..

tusilazimishe mawazo haya ya kikomunist yslishafeli hayawezi kutusaidia..
serikali ipeleke mashirika yake ya umma yakajiunge na dse ili wananchi sisi tuwe wamiliki directly
 
safi sana mkuu umezungumza ukweli kuna mtu anajua akinunua hisa 7@750 basi mwisho wa mwaka anasubiri faida
 
Kuyalazimisha makampuni ya simu kuwa listed kwenye Dar es Salaam stock excharge kuna faida kubwa sana
Zifuatazo ni faida hizo
Moja, ni ukweli usiopingika kuwa kumekuwepo na tetesi za muda mrefu sana kuwa kampuni hizi zimekuwa zikificha hesabu zake
Kwa lengo la kukwepa kulipa kodi stahiki
Hivyo wakiwa listed DSE
Itawalazimu makampuni haya kuweka wazi mahesabu yao yote, ili shareholders waweze kujua maendeleo ya kampuni hizo
Kwani nao watakuwa ni sehemu ya umiliki
Hivyo itasaidia nchi kupata mapato stahiki katika kodi
Mbili, itanufaisha umma wa Watanzania kuwa sehemu ya umiliki wa makampuni haya
Hasa ukizingatia kuwa yamekuwa yakipata faida kubwa sana
Kwa hiyo sehemu ya faida hiyo itabaki humu humu ndani
Hizo ni sababu mojawapo inayoelekea serikali kuwalazimisha wawe listed DSE
Hata makampuni ya madini nayo yanapaswa yawe listed DSE
Kupynguza mwaya wa kukwepa kulipa kodi stahiki
sheria iko wazi kabisa kuwa kama kampuni inamilikiwa na watu zaidi ya 20 na kuendelea basi hiyo kampuni huwa public company.. Na kisheria DSE hujumuisha only public companies. so kama wamelazimishwa it means that sasa wako katika public company otherwise hizo story ni uzushi kama uzushi mwingine.
NB Public company haimaanishi kuwa inamilikiwa na serikali bali inamilikiwa na watu wengi na iko open kiasi kwamba hata wewe waweza pata share na kuwa shareholder wa hiyo kampuni.
 
Tigo,Vodacom na Airtel ndo kampuni pekee zilizotajwa mpaka mwisho WA December 31 2016 lakini cha kushangaza hadi TTCL yenyewe ambayo Ni kampuni ya serikali haijapeleka maoimbi DSE
 
Watanzania sisi ni watu wa ajabu sana, hii sheria ipo kwa ajili ya kutulinda na kutufaidisha sisi waTz ila ukisoma comments humu utahudhunika kwa ignorance iliyoshamiri.

Makampuni yaliyolazimishwa ni makampuni ya mawasiliano nia na dhumuni kuu ni mawili, moja kampuni ikishakuwa ya umma hawawezi tena kutengeneza mahesabu kirahisi, hakutakuwa na sababu ya kutengeneza mahesabu na kumficha hadi mmiliki wake hapo serikali itapata kodi yake sahihi bila ya kudanganywa, waTz inabidi tulilie sheria kama hii ipanuliwe hadi kwenye sekta ya madini, mafuta na gesi na sio kulia lia tu.

Pili, target wa hizi hisa sio walalahoi, watu wenye pesa zao wataenda kununua, hata middle class na wenyewe wakipata elimu nzuri watanunua hisa badala ya kuhangaishana na biashara za juani, tumepewa fursa ya kumiliki uchumi wa sekta ya mawasiliano tuache kulia lia badala yake tutumie fursa hiyo.
 
Huwezi kuzuia uhuni unaondelea kwenye hayo makampuni ya simu hapa Tanzania kama hawakuweka kila kitu wazi, na namna bora ya kuaanika kila kitu ni kujisajili soko la hisa. Vingenevyo hela zitaishia Panama.

Pia kumbuka sheria iko wazi, wanatakiwa kuwa kwenye soko la hisa tatizo huko nyuma hawa mabwana walikuwa wanafanya watakavyo kwenye shamba la bibi.
Sheria ipi iliyokuwepo huko nyuma inayowalazimisha kulist kampuni zao,tusaidie tafadhali
 
Kila mtu ana mawazo yake lakini uamuzi wa gvt ni mzur.Kilichobaki ni utekelezaji tu. Hao wanaopinga eti utakua uchumi was kicominist hawana mashiko. Mwaka 2008 UK gvt walitoa pesa kuzipa bank binafsi ili kusaidia credit crunch uliyotokea. Kitendo kile kilitionekana ni cha kicominist lakin kilifanywa ktk nchi za kibepari.
Vile vile, ktk juhudi za kuondoa gap kati ya maskini na tajiri moja kati ya measures zinazopendekezwa ni kusaidia wengine kuwa na umiliki wa compuni ili kupata faida.
Pamoja na ukweli kua kwenye biashara ya hisa kuna faida na hasara lakin gvt inajua hizo kampuni za simu hua zina faida kubwa, hivyo serikali haiwezi kukushauri ukale hasara.
Kupitia kila kinachoitwa "protectionism policy" nchi pamoja na kuwepo sheria za kimamaifa km WTO bado nchi hujiwekea sera zao ambazo wanaona ni muhim kwa kipindi fulani.
Kuna repatriation of fund kwa nchi km Indonesia kuna nchi huwezi fanya investment bila ya kuhusisha wazawa.
Ni vyema watu wakaangalia angles zote. then kuchagua ile ambayo ni nzur kwa wakati flan then unaweza kubadilisha ikiwa sera haifanyi kazi kwa muda flani.
Lakin kwa uwamuzi huo wa serikali yetu sidhani kma kuna mashaka ni uamuzi wa kizalendo.
 
Back
Top Bottom