Hili la maiti kulipishwa madeni Hospitali za Serikali limekaaje?

Mloganzila ni mbaya kuliko popote duanian nilienda kufanya vipimo mwaka Jana hivi nikalipa gharama zote mwisho wakanishangaza kusomewa majibu hela nikamwambia nipen Basi ntajua mwenyewe mbele wakagoma mpaka nilipe na hapo nimesafir Kutoka katav mpaka hapo kwa matibabu tu nikaona isiwe kesi nikamwambia mhusika uzur hata wewe utaumwa na utakufa baki na majibu nikaondoka kurud katav Ila Mungu mwema sana sijawah tumia dawa yeyote Ila najihis nimepona kabisa maumivu hayapo kabisa
Ila I wish wenye kuweka hizo Sera sijui sheria wangekufa wote tu hapo tuqmze upya
Mloganzila ni kituo cha upigaji wafe na Sera zao
yaan kumpeleka mgonjwa wako pale ni bora umpeleke kwa mganga wa mitishamba anaweza pona, sisi wenyewe marehemu alikuwa hataki kabisa tumpeleke pale
 
yaan hospital za serikali mnaweza kuuza Nyumba kugomboa maiti kwasasa
Kweli kabisa, halafu bado waziri husika anasema huduma zimeboreshwa na bei ni rafiki kwa watanzania lakni mambo ni kinyume chake. Ila kwenye wataalamu bado napata mashaka makubwa sana huwenda wanafunzi wa intern wanaaminiwa kufanya majaribio kwenye miili ya waatu ambapo naona sio sawa.

Naomba mjaribu kulifuatilia hilo hapo mloganzila.
 
Ww acha hizo maana ya kulipa si kwamba mgonjwa apone mmeshindwa kumtibu mgonjwa kafa mnadai hela ya nn ww mfano umepeleka gari geleji limeshindwa kutengemaa utatoa pesa hata km fundi alitumia gharama ...Hapo tunaomba tu serikali iangalie namna ya kufanya maaana Afya ya watanzania ni muhim kwa taifa letu
Ni upumbavu wa kiwango cha juu kabisa kulinganisha BINAADAMU na GARI.

Gari likiharibika linatengenezwa kwa kubadilisha spea. Binaadamu akiumwa=kuharibika HAKUNA SPEA ya kubadilisha ili utoe iloharibika. Binaadamu tunarepair spea hizohizo alizonazo. Sasa kama hizo spea zikishindwa kutengemaa ndo basi tena.

Fundi gari akiona hii gari haiwezi pona basi anachukua spea zake ambazo alikuwa kashaziweka tayari kwa hiyo hana cha kupoteza labda muda wake tuu. Then wewe unabaki na mkweche wako wa gari.

Binaadamu akiumwa anafanyiwa vipimo, anatumia na dawa za hospitali. Akifa huwezi sema hivi vipimo tulivyomfanyia tunavirudisha. Wala dawa alizotumia huwezi kuzitoa mwilini mwake na uendelee kuzitumia kwa mgonjwa mwingine.

KULIPIA NDIO SOLUTION PEKEE.

Kwa hiyo mkuu usifananishe mwili wa binaadamu na gari. Unakosea sana. Ni vitu viwili visivyoendana kabisa.

Unforgetable
 
hapafai pale, wapo kipesa zaidi,
Umeombwa mchanganuo wa gharama umeshindwa kuuleta lakini stil unabwabwaja tuu pale hapafai, pale hapafai, pale hapafai.

Package ya gharama MNH,MLOGANZILA,MOI,JKCI ni moja. Labda ungelalamikia huduma mbovu hapo ungeeleweka kidogo, lkn kwa hili la gharama umepotea njia, tena huenda gharama za hapo mloganzila ziko chini kdg.

Unforgetable
 
yaan kumpeleka mgonjwa wako pale ni bora umpeleke kwa mganga wa mitishamba anaweza pona, sisi wenyewe marehemu alikuwa hataki kabisa tumpeleke pale
Na ni kweli watu wa bagamoyo kwa mitishamba hamjambo. Mnaendaga hospitali too late baada ya kuhangaika huko na huko na kushindwa ndipo mnaenda hospitali.

Unforgetable
 
yaan hospital za serikali mnaweza kuuza Nyumba kugomboa maiti kwasasa
Dada nlikuwa nakuona mtu mwenye akili kumbe zero kabisa.

Kwamba hospitali za serikali mnaweza kuuza nyumba kukomboa maiti?. Like seriously? Are you sane?

Naomba nikuulize swali dogo tuu, kwa nini msilipie gharama za matibabu kabla hajapatiwa huduma? Kwa nini msubiri mpaka wakati wa kuruhusiwa au mpaka afariki ndipo muanze kujenga picha ya kulipishwa maiti wakati kiuhalisia mnalipia huduma alizotumia ndugu yenu kabla hajafa?.

Unforgetable
 
Huduma zikosekane serikali ikiwa wapi, watu kila siku wanalipa kodi.

..........Laki saba ni gharama ndogo? Hivi unajua kuna mtu hawezi hata kupata Milo mitatu kwa siku na akiumwa anatakiwa apate matibabu mtu wa aina hiyo ataweza kulipa laki saba kweli?
Samahani ndugu ,mimi nilikuwa naongelea gharama za matibabu, siyo umaskini wa watanzania. Laki saba ni gharama ndogo sana kwa huduma husika kwa mgonjwa husika, kumbuka siyo kwa wagonjwa wote na huduma yoyote. Naongelea mgonjwa husika. Kodi ina kazi zake, huduma za afya kwa sehemu kubwa zinaendeshwa na michango ya wahisani na uchangiaji kutoka kwa wananchi na ruzuku kidogo ya serikali(kodi). Na vya kwanza viwili ndio vinachukua zaidi ya 95% ya gharama. Swala hapa ni kupambana kuondoa umaskini na kuongeza kipato ili watu waweze kuchangia huduma. Tujiunge na bima za afya
 
Safi.

......... Subiri yakukute.
 
mnapenda sana kulalamika...hivi vifaa vlivyotumika toka mzee wetu kafika hospitali mpaka mauti yakamkuta analipia nani?aliyemhudumia mnadhani mshahara wake unatoka wapi?hata kama ni mtumishi wa serikali hamjui hizi pesa mwisho wa siku zinamlipa mshahara?tukate bima jamani hata kama sio nhif basi hata chf iliyoboreshwa.....30000 watu kumi kweli inatushindwa kwa mwaka???apumzike kwa amani mzee wetu
 
Habarini wapendwa,

Wiki hii mzee wetu alikuwa anaumwa Hernia, tarehe 07/11/2019 tukampeleka Mloganzila hospital akitokea hospitali ya Bagamoyo, kufika kule usiku akafanyiwa upasuaji, saa kumi alfajiri akafariki. Sasa tarehe 08/11/2019 tukaenda ili kuchukua mwili wa marehemu akazikwe.

Kufika pale tunaambiwa marehemu anadaiwa jumla ni Tsh 775,000/= tukalalamika mbona hela nyingi hivyo, wakatuambia nendeni ustawi wa jamii labda wanaweza kuwasaidia mkilalamika kuwa hamna uwezo, kwenda kule tukaambiwa kuwa hata iko kiasi mlichotajiwa kapewa punguzo sababu katokea hospitali ya Serikali kuja hapa, kukosa hivyo ingekuwa mara mbili yake.

Tukasema sawa, ndugu wakachangishana ikafika laki sita na ishirini, kuipeleka kule bado wakagoma, wakasema hadi hela itimie yote isipungue hata mia ndo maiti itatoka, basi tukapigia simu watu baki kuwakopa hela ikatimia tukaenda kupeleka tukapewa mwili wa marehemu. Sasa najiuliza hivi huu utaratibu wa kudai maiti ni haki kweli? Mtu amekufa bado mnamdai, sio laana kweli.

Kuna wapemba tumewakuta wanadaiwa milioni tatu za maiti wao, wameshauriana waende wakafanye kisomo cha kuswalia maiti pale hospitali, wakimaliza waondoke mwili wauache pale pale Mloganzila, wao wataisabu kama ndugu yao amekufia baharini na maiti haikupatikana kuliko kulipa hela hiyo.

Hii ni kweli jamani wala sio jambo la kutunga, marehemu katuachia madeni.

Zaidi, soma:

Sasa rafik Angu Mina Cute ulitaka sisi tupate wapi hela za kununulia Ndege!!???...😌🙄
 
Huduma zikosekane serikali ikiwa wapi, watu kila siku wanalipa kodi.

..........Laki saba ni gharama ndogo? Hivi unajua kuna mtu hawezi hata kupata Milo mitatu kwa siku na akiumwa anatakiwa apate matibabu mtu wa aina hiyo ataweza kulipa laki saba kweli?

Serikali imeshaacha kupeleka ruzuku mahospitalini toka Jiwe akamate nchi... Hospital zinajiendesha
 
Umeombwa mchanganuo wa gharama umeshindwa kuuleta lakini stil unabwabwaja tuu pale hapafai, pale hapafai, pale hapafai.

Package ya gharama MNH,MLOGANZILA,MOI,JKCI ni moja. Labda ungelalamikia huduma mbovu hapo ungeeleweka kidogo, lkn kwa hili la gharama umepotea njia, tena huenda gharama za hapo mloganzila ziko chini kdg.

Unforgetable
katafute bwana kaka, hasira zako usiniletee mimi, maana mkiachwa mnakuwa kama vichaa
 
Back
Top Bottom